Lecturer part 2

miss strong

JF-Expert Member
Jul 4, 2012
7,012
3,694
Habari wana JF,poleni na majukumu ya kila siku ya kulijenga taifa letu.

Nashukuru kwa ushauri wenu na maombi yenu juu ya yaliyonikuta kwa huyo lecturer kama nilivyotuma katika huu mtandao wik iliyoisha.
Nilichukua maamuz ya kwenda kwa DS moja kwa moja baada yakutoka kwa HOD,Nilipoonana na DS nilieleza hali halis iliyonitokea na kuniomba nisiogope maana yeye ni baba kwahiyo niwe huru tu.Baada yakuyasikiliza hayo yote ikabidi twende nae kwa mkuu wa chuo.Aliniacha na mkuu wa chuo na nikajieleza kama nilivyofanya kwake.

Mkuu wa chuo aliniomba nimwandikie yeye barua na kuahidi kuwa lazima hilo alifanyie kazi maana kaletwa kwa ajil ya kaz hiyo maana chuo hicho kilikuwa kinanuka tabia hizo na hatamuonea mtu aya maana hakuna mtu anayemjua yeye ni mgeni.Amekiri kuwa huko chini kuna kulindana sana.
Aliomba nimuahid kama nitafanya hivyo maana mimi ndo nitawapa wao nguvu ya kuendesha hiyo kesi....!

Tayari nimeandika barua na nimetengeneza CD ya maongezi yale aliyokuwa ananiambia.
Walikuwa wanaisubiri na kuniambia kuwa walihisi labda nimenunuliwa baada yakuona nimechelewa kurudisha hiyo barua maana kati ya hao wakuu alipoonana na( mwalimu ) hakumchangamkia kama ilivyo kawaida na kuhis kuwa ameshituka au amesikia kuwa mimi nimeenda kushitaki hiyo kesi.
Nimeambiwa hizo nguo ambazo nilizozivaa siku hiyo la tukio nisizifue wala kushikwa na mtu mwingine,na tayar nimefanya hivyo.Tunasubiria maamuz ndan ya wiki hiyo ijayo lakin tayar limeanza kufika kwa wanafunz na kama litacheleweshwa bas nitataja chuo kwenye mitandao nakuomba asasi mbali mbal kunisaidia kwa jambo hilo na pia wanafunzi wenzangu kusaidia hilo kwa maana huyo mwalimu pale ni janga kabisa tayar amewafanyia wengine mambo hayo sana.

HOD nilipoona nae aliniambia ameona habar yangu kwenye mtandao,kwahiyo anasema hata mlengwa atakuwa ameiona.........nikamjibu mm sintojali kuwa ameona au laah coz sijamtukana mtu bali ni ukwel mtupu niliouzungumzia ktk huo mtandao.
Na iman sana na huu uongoz mpya wa chuo kuwa watafanya kitu.
Tayari pia nimewasiliana na watu wa sheria na wao pia wanasimamia hilo jambo

Napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwenu wote..................Mungu awabariki mno!Nahitaj ushaur wenu zaidi na kama kuna kitu nimekosea katika hizi hatua za ss pia mnikosoe.
 
Mrisho nyuma safi,komaa dada huyo pimbi aone cha moto,maana utakuwa umeokoa wengi!
 
kila la kheri kwenye kupata haki yako, udhalilishaji ni mbaya na unastahili kupingwa
 
Umejiandaa kusimama nae mahakamani?

Itakapobidi sina jinsi............na ndio maana wakuu wake wamesema wapo heri hata nguo zipimwe.Si anaweza yy akahisi amedharirishwa?Mzazi wangu pia anasubiria majibu ya chuo.
 
Kwa trend hii, maskini ndugu yangu. Atakuja kusalimika kweli? (Siyo huyo wa kwenu lakini).
Na unapaswa uwaambie wasichana wenzako waache kujirahisi mno! wawe strong kama wewe
 
Hongera dada kwa hatua uliyofikia Mungu azidi kukusaidia na uongozi wa chuo awajalie hekima ya kuamua kwa haki bila upendeleo..afadhali huyo lecturer afukuzwe kazi ili asiendelee kuchafua hali ya hewa hapo chuoni.Mapambano bado yanaendelea songa mbele usiogope haki itatokeza kama vile mapambazuko yatokezapo
 
Kwa trend hii, maskini ndugu yangu. Atakuja kusalimika kweli? (Siyo huyo wa kwenu lakini).
Na unapaswa uwaambie wasichana wenzako waache kujirahisi mno! wawe strong kama wewe

Kwa uwezo wa Mungu watasalimika.
 
Hongera dada kwa hatua uliyofikia Mungu azidi kukusaidia na uongozi wa chuo awajalie hekima ya kuamua kwa haki bila upendeleo..afadhali huyo lecturer afukuzwe kazi ili asiendelee kuchafua hali ya hewa hapo chuoni.Mapambano bado yanaendelea songa mbele usiogope haki itatokeza kama vile mapambazuko yatokezapo

Najua sipo peke yangu ktk hayo mapambano....Mungu ni ngao yangu.
 
mimi sioni ubaya wa kutaja,CHUO KINA MATAWI,kama sio matawi basi kina schools na college,so ni ngumu kubaini ni tawi,ama college ipi,

Nitakapotaja chuo kwa ss italeta taharuki sana na hata wakuu wakashindwa kufanya wanachokikusudia.Ila pale itakapodi kufanya hivyo bas sina jins
 
Ni kweli wamtumainio Bwana hawatatahayirka kamwe.........na wamgejeao Bwana hawataaibika kamwe hata unakosali wachungaji na washirika wote wakusaidie maombi haya dhidi ya huyu Goliathi.HATA SASA BWANA ANATENDA.

Asante kwa kunitia moyo..........najua nae anajiandaa kuniangamiza kwa njia yoyote.Ila acha tu iwe kwa maana hata kama nitatoweka kwa kusema ukwel bas wengine watapona.
 
Sina uhakika na usahihi wa njia unayoitumia kutatua tatizo hili, linaweza kukuleta matatizo zaidi kuliko kutatua. Nadhani kungekuwepo na njia bora zaidi ya kushughulikia swala hili, kila la heri lakini.
 
Back
Top Bottom