Le Mutuz auza sura kwenye Udaku

TIQO

JF-Expert Member
Jan 8, 2011
13,787
2,078
MTOTO.jpg



Na Sifael Paul

WILLIAM Malecela a.ka Le Mutuz ambaye anatajwa kuwa ni mtoto wa mwanasiasa mkongwe Bongo, John Malecela ambaye anadaiwa kuwa ni funga kazi kwa kupenda kupiga picha na wanawake wazuri kila anapokuwa, Amani limemfuatilia hatua kwa hatua na sasa linafunguka.

Kwa mujibu wa ‘mapicha' yake mazuri yaliyopo mitandaoni, asilimia 90 zinamuonesha Le Mutuz akiwa na wanawake wazuri wa kada mbalimbali.

WAMO MASTAA
Mbali na wanasiasa wenzake, Le Mutuz aliyegombea ubunge wa Afrika Mashariki kwa leseni ya CCM hivi karibuni lakini kura hazikutosha, anaonekana kwenye picha nyingi zisizo na idadi akiwa na mastaa mbalimbali wakiwemo waigizaji na wanamuziki wenye majina makubwa Bongo.

NI KILA MAHALI?
Katika picha hizo, Le Mutuz anaonekana akiwa sehemu mbalimbali hasa kwenye kumbi za starehe, baa, migahawani, viwanjani, nyumbani na ufukweni, vyote jijini Dar es Salaam.

ETI NI MAMBO YA ‘KUTOKLEZEA'
Kwa mujibu wa mtu wa karibu wa Le Mutuz, jamaa huyo mwenye ‘sivii' ya kuishi nchini Marekani kwa muda mrefu amekuwa akiwakaribisha warembo hao kwenye mtandao wake (jina tunalo) kwa kutundika picha hizo na kuwataka waingie humo kujiona ‘walivyotoklezea'.

BAADHI YA MASTAA NI HAWA
Baadhi ya mastaa wanaoonekana na ‘mutu mukubwa' huyo na kusababisha minong'ono kwa kuwa zina mapozi tata ni pamoja na Wema Isaac Sepetu, Jacqueline Wolper Masawe, Jokate Mwegelo, Miss Tanzania 2011, Salha Israel, Judith Wambura Mbibo ‘Lady Jaydee' na warembo wengine ‘kibwena' wasiokuwa na majina.

WAMO MARAFIKI WA FACEBOOK
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, inaelezwa kuwa, Le Mutuz huwa anawasiliana na warembo ambao ni marafiki zake katika mtandao wa kijamii wa Facebook ambapo hukutana nao na kupiga picha ili kuziweka mtandaoni kwake.

MSHANGAO!
Kwa mujibu wa maoni ya watu wanaotembelea mtandao wake wanashangazwa na ishu hiyo huku wakihoji mbona anafanya na mademu tu, tena wazuri?

LENGO NI NINI?
Ili kupata undani wa kwa nini Le Mutuz anafanya hivyo, Amani lilifanya jitihada za kupata kupitia kilongalonga chake cha kiganjani lakini hakupatika, hata hivyo jitihada za kumpata zinaendelea.
 
Muongezeeni promo, ndicho anachopenda na mnampa kitu roho yake inapenda. Let him be, ni loss yake kama at all kuna loss!

Anapotakaga ushauri si huwa anaomba?
 
huyu ndio kiongozi wa anayejiamini wa jumuiya ....

Nimewahi kusikia kitu kuwa ukiruka development stage or milestone utotoni au ujanani, lazima uzirudie uzeeni.

Duh, huwezi jua ndugu yangu, usikute labda hiyo ndo staili yake pendwa ya upigaji picha manake naona kama staili zote zinafanana! Nadhani ataingia tu hapa kutoa ufafanuzi kwa ile staili yake ya kuchanganya lugha tofauti tofauti kwenye andishi moja.
 
Nimeona kwenye GPL wameamua kumuanika Le Mutuzz, angalia picha za aliyepaswa kuwa mwakilishi wetu EA!!
 

Attachments

  • MTOTO.jpg
    MTOTO.jpg
    87.9 KB · Views: 1,285
Tulimpa ushauri akatupuuzia..alikuwa anataka umaarufu..umri wake hauendani na mambo.anayofanya...huyu mtu ni hopeless kama CCM ndo ina watu wa hivi bac mwisho wake umefika.
 
hivi ana mke na watoto?amepataje huo uongozi jumuia ya wazazi kata kigamboni?maana hafananii kuwa mzazi
 
eti mjumbe wa ccmabwepande wazazi dar,kwa tabia hii ni kwamba amemrithi Babake.Mzee Malecela alikuwa mto mkali kwa watumishi wa ikulu kama arusha,Mwanza, na zingine.Alipokuwa akienda ziara mikonani wakati huu akiwa PM wale wahudumu wa ikulu ni chakula yake na wengi kawatia mimba sana na kumbukeni kipindi kile viongozi walikuwa wakisafiri bila kuwa na wake zao ana.Mtoto wa nyoka ni nyoka ni sawa wote tu na Lusinde wa mdomo dampo.
 
Huyu jamaaa alipewa ushauri na wana jf lakini kichwa chake kinaonekana ni kigumu!

Mtu kama huyu inaonekana alicho taka ni kutolewa kwenye magazeti na amefanikiwa!
Hongera lem
 
Nilishawahi kusema hapo nyuma kuwa huyu jamaa ni msanii hawezi lolote zaidi ya kupenda sifa tu. Na hapo ukute yeye ndie kawatafuta waandishi wa habari wamtoe. Nilikuwa nashangaa eti watu wanamwambia aje CDM. CDM kuna watu wa style hii kweli??
 
Back
Top Bottom