Lazima Lowassa ashitakiwe kwa Ufisadi!!

Lazima Lowassa ashitakiwe kwa Ufisadi!!

Natamani sana kuiona hiyo siku ambayo Lowassa anapanda mahakamani maana tutajua nani na nani walikula hela yetu usijekushangaa hata wale ambao waliokuwa wakidhaniwa kuwa wasafi nao wamo.......
 
Kiashiria cha udhaifu kwa binadamu wakati mwingine ni pale anaposhindwa kulifikisha mwisho jambo la muhimu analotakiwa kulikamilisha. Sisi kama taifa tumekuwa tunatangatanga na Jambo lililosababishwa na mtu mmoja tu na sisi kama taifa tumeshindwa kufikia mwisho wake.

Tarehe 7/2/2008 aliyekuwa Waziri wa Mkuu wa Tanganyika wakati ule, Edward Ngoyai Lowassa alijiuzulu wadhifa wake baada ya kutuhumiwa kuingilia mchakato wa Zabuni ya Ufuaji Umeme iliyosababisha kuletwa kwa Kampuni ya Ufuaji Umeme ya Richmond nchini. Tangu kujiuzulu kwa Lowassa mpaka sasa imeshapita miaka zaidi ya 8 na miezi kadhaa, lakini bado suala la sakata la Richmond halijaisha

Mitambo iliyoletwa na Kampuni ya Richmond ambayo bado ipo Pale Pale ilipofungwa na Kampuni ya Richmond, imeshabadilishwa umiliki wake mara mbili. Imetoka kwa Richmond ikanunuliwa na Dowans na sasa inamilikiwa na Kampuni ya Symbion ya Marekani. Lakini sisi kama taifa tumeachwa pale pale tulipokuwa Mwaka 2008.

Kwa kuwa kuna Mahakama ya Mafisadi inaundwa na sisi kama taifa tunayumbishwa na suala la mtu mmoja tu, ambaye si kiongozi wa serikali kwa sasa, nashauri Kesi ya Kwanza kwenye Mahakama ya Mafisadi iwe ni hii ya "Ufisadi" wa Edward Ngoyai Lowassa kuhusu Ufisadi wa zabuni ya ufuaji umeme iliyosababisha Sakata la richmond.

Ni lazima Lowassa ashitakiwe ili kama yeye anao ushahidi tofauti na ule ambao wapinzani wake wanao aje nao mahakamani ili upimwe kwenye mizani ya kisheria tujue nani mkweli kati yake yeye na wapinzani wake.

Haiwezekani mitambo ile iliyoletwa na Kampuni (Feki?) ya Richmond bado ipo nchini mwetu, inafua umeme, Tannesco wanalipa Capacity charges tanesco wanauziwa umeme kutokana na mitambo ile ile iliyokuwa ya Richmond, mkataba ule ule wa kati ya Richmond na Tannesco ndiyo umekuwa ukihuhishwa na Dowans na sasa Symbion, lakini sisi kama taifa bado tunakumbushana mambo ya mwaka 2008.

Kuukata Mzizi wa fitina ni lazima Lowassa na kama wapo na wengine waliohusika na sakata la Richmond wafikishwe kwenye Mahakama ya mafisadi mara tu Mahakama hiyo itakapoanza kazi. Tunataka Kesi ya kwanza kwenye mahakama hiyo iwe dhidi ya Lowassa na wenzake waliohusika na suala la Richmond.

KESI YA LOWASSA ISIPOKUWA YA KWANZA KWENYE MAHAKAMA YA MAFISADI NITASHANGAA KWELI KWELI!!

inawezekana mkuu, sema CCM hawawezi kufanya hivo kwa vile Richmond ni kokoro...hadi Obama ndani!
 
Huwezi kuniambia inapotajwa Tanzania sio lazima ihusishe Zanzibar ,kwani Tanzania ilipatikanaje ?? Tanganyika+ Unguja + Pemba=Tanzania

Hilo la kudhulumiwa ni swala lingine kabisa anzisha thread yake

Wewe una uhakika gani Waziri mkuu hana mamlaka na mambo ya Zanzibar ? Wanapokula viapo vya kutotoa siri wewe unafikiri ni siri zipi hizo ??
Wala tusibishane. TFF kirefu chake ni Tanzania Federation of Footbal, unadhani TFF inawakilisha na Zanzibar pia?
 
Hotuba ya Mheshimiwa Edward Lowassa aliyotoa Bungeni wakati anajiuzulu Uwaziri Mkuu.

Nakushukuru mheshimiwa Spika kwa kunifanya msemaji wa kwanza katika hoja hii. Lakini la pili nimpongeze Dr. Harrison Mwakyembe Mwenyekiti wa Kamati teule,kwa kuwasilisha kwa mbwembwe nyingi sana taarifa yake, mbwembwe zilikuwa nzuri sana.Kwa kazi nzuri kwa maoni yao na wameiwasilisha vizuri.Lakini Mheshimiwa Spika, nimesimama kuweka kwenye Kumbukumbu kutokuridhika kwangu na jinsi kazi hiyo ilivyofanywa.

Mhesimiwa Dr. Harrison Mwakyembe ni mwanasheria tena daktari alikuwa anafundisha wanafunzi Chuo Kikuu. Moja ya vitu alivyokuwa anafundisha ni Natural justice. Wewe pia Mheshimiwa Spika ni Mwanasheria, unafahamu suala la Natural Justice. Kwamba katika Kamati Teule, imesikiliza watu wengine wote, pamoja na waliowaita minong’ono ya mitaani. Wamesafiri mpaka Marekani kutafuta mashahidi, lakini mimi ambaye ni mmoja katika watuhumiwa mle hawakunihoji hata siku moja!

Mheshimiwa Spika. Nimesimama kueleza masikitiko yangu. Ofisi ya bunge mpaka ofisini kwangu hata wangeniita ningeenda kwa mguu kama hamna gari. Na nilikuwa tayari kufanya hivyo.Hawa ni watu makini sana, siwezi kuamini kwamba wanaweza kufanya Oversight kama hiyo. Kwa sababu katika kila hoja walizojenga, walisema Waziri Mkuu ilikuwa hivi, kulikuwa na shida gani kuja kuniuliza, Waziri Mkuu wanasema ulitoa dokezo hili ni sawa sawa ni kweli? Kulikuwa na shida gani kwa mfano Mheshimiwa Spika, kufuata utaratibu wa Westminster kuthibitisha hapo unaposema, wenye Richmond nifulani uka- table Record na ushahidi kwamba ni fulani.

Mheshimiwa Spika Taifa letu ni taifa changa, lakini chombo hiki ndiyo mahali pa Demokrasia pa kubwa katika nchi yetu pote, hapa ndipo penyewe. Kama katika chombo hiki haki haitaonekana kutendendeka, Mheshimiwa Spika nchi haitakwenda vizuri.

Hapa ndipo tunategemewa kuonyesha umakini, umahiri wetu katika mambo ya Demokrasia. Kwa hiyo nilichofanyiwa Mheshimiwa Spika napenda kuweka kumbukumbu sahihi…sawa. Kwamba naona si sahihi, na nimefadhaika sana, nimedhalilishwa sana na nimeonewa sana katika hili. Maana zimechukuliwa tuhuma zikaja kuelezwa hapa kwamba hivi ndivyo ilivyo, mimi sijaulizwa. Kulikuwa na shida gani kuniuliza. Kwa nini muamini minong’ono ya mitaani kuliko maelezo yangu?

Sisi wote hapa ni wanasiasa, tukianza kuamini minong’ono ya mitaani, niambieni mwanasiasa atakayesimama. Hatuwezi… Tume wamepewa muda wa kutosha kabisa, lakini inashindwa kumuona mtu ambaye wanamtuhumu na wanamsema kwa kirefu sana.

Lakini mheshimiwa Spika, hata pale uliponinong’oneza ukaniambia “una ushahidi wowote”? Nilikupa ushahidi huo wa maandishi. Katika taarifa yao hakuna hata moja ya ushahidi ambao umetoka Ofisi ya Waziri Mkuu, hata mmoja! Lakini kitabu cha Majedwali kimejaa majedwali meengi pamoja na Magazeti mpaka ya Udaku, lakini maelezo ya Waziri Mkuu hakuna hata moja.

Mheshimiwa Spika. Mimi naamini ingekuwa ni heshima wangeliweka halafu wakasema tunakataa kitambulisho hiki kwa sababu hii na hii na hii na hii. Mimi nadhani ingejengwa hoja. Lakini kujenga hoja na kuja hapa bungeni, tunahutubia nchi nzima na kusema Waziri Mkuu amefanya hiki, amefanya hiki, amefanya hiki bila kumsikiliza, nachelea kuuliza, hivi watu wa chini itakuwaje?

Lakini Mheshimiwa Spika nimetafakari kwa makini sana jambo hili, nikajiuliza, hivi hasa kulikoni. Mpaka watu wazima wenye uwezo wao, watu maarufu, wenye heshima zao. Mpaka wafike mahali waache jambo la msingi kama hilo, kulikoni?

Mimi nadhani, they have a wish which I am going to grant, ni Uwaziri Mkuu. Nadhani tatizo ni Uwaziri Mkuu. Kwamba ionekane Waziri Mkuu ndiye amefanya haya, ionekane Waziri Mkuu amefanya haya, tumuondolee heshima au tumwajibishe. Mheshimiwa Spika. Nimetafakari sana, kwa niaba ya chama changu, kwa niaba ya serikali yangu, nimeamua kumwandikia Rais barua ya kumwomba niachie ngazi.

Nafanya hivyo kwa moyo mweupe kabisa, kwa moyo mweupe kabisa ili kuonyesha dhana ya uwajibikaji lakini na kutokukubaliana na utaratibu uliotumika kusema uongo ndani ya bunge wa kunisingizia.

Mheshimiwa Spika nitumie nafasi hii kumshukuru sana Rais kwa heshima aliyonipa ya kutumikia nchi hii kwa Uwaziri Mkuu kwa miaka miwili, namshukuru sana mheshimiwa Rais. Nakushukuru wewe, nawashukuru Mawaziri na Manaibu Mawaziri, nawashukuru waheshimiwa Wabunge, na wanachama wa CCM tuliosimamia Ilani ya Uchaguzi ya Chama chama Mapinduzi. Baada kusema hayo nakushukuru Mheshimwa.
Uteuzi umeshaisha dogo labda usubiri uteuzi wa watendaji wa vijiji
 
--kiulize chama kipenzi cha moyo wako kinaifahamu Richmond kwelikweli!.
 
Baada ya UKUTA, UKUMAWA ifuate.

Umoja wa Kuhimiza Mafisadi Washitakiwe.
 
Ndiyo maana sisi wengine ambao tunaiona hii serikali ni Imara tunaihamasisha wampeleke Lowassa kwenye Mahakama ya Ufisadi, kinyume cha hapo wakae kimya!!
Hawana mawakili wakuendesha kesi. Naambiwa wnunuzi wa viungo vya albino hajafikishwa mahakamani hata mmoja. Hofu ni kwamba labda dola ni yao.
 
Lowassa is out of date.....tuangalie wanasiasa vijana wenye maono mapya
 
Wala tusibishane. TFF kirefu cha Tanzania Federation of Footbal, unadhani TFF inawakilisha na Zanzibar pia?
Ushatoka kwenye mada unaniletea habari za TFF ,

Unaposema waziri mkuu hana mamlaka na yanayotokea Zanzibar kwa sababu kuna waziri kiongozi

Hivi Kitwanga alipoenda Zanzibar wakati wa marudio ya uchaguzi ,report yake anaipeleka wapi ? Achilia mbali hiyo ni wizara iliyopo ndani ya muungano ,unataka kuniambia Kitwanga ataishia kwa waziri kiongozi tu na Majaliwa hatafikishiwa hiyo report ??
Ushaona uhusika wa waziri mkuu mpaka hapo ??


Hakuna waziri mkuu wa Tanganyika ,tuna waziri mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania full stop

Siku njema
 
Back
Top Bottom