Lazima Lowassa ashitakiwe kwa Ufisadi!!

Lazima Lowassa ashitakiwe kwa Ufisadi!!

Lowassa amezoofisha msukumo wa maendeleo tz kwa kupitia madaraka alio kuwa nayo kwa kujinufaisha yeye na familia take Anastahili kuwa wa kwanza kuzindua mahakama ya mafisadi kama fisadi

Sent from my TECNO H5 using JamiiForums mobile app
 
Kiashiria cha udhaifu kwa binadamu wakati mwingine ni pale anaposhindwa kulifikisha mwisho jambo la muhimu analotakiwa kulikamilisha. Sisi kama taifa tumekuwa tunatangatanga na Jambo lililosababishwa na mtu mmoja tu na sisi kama taifa tumeshindwa kufikia mwisho wake.

Tarehe 7/2/2008 aliyekuwa Waziri wa Mkuu wa Tanzania wakati ule, Edward Ngoyai Lowassa alijiuzulu wadhifa wake baada ya kutuhumiwa kuingilia mchakato wa Zabuni ya Ufuaji Umeme iliyosababisha kuletwa kwa Kampuni ya Ufuaji Umeme ya Richmond nchini. Tangu kujiuzulu kwa Lowassa mpaka sasa imeshapita miaka zaidi ya 8 na miezi kadhaa, lakini bado suala la sakata la Richmond halijaisha

Mitambo iliyoletwa na Kampuni ya Richmond ambayo bado ipo Pale Pale ilipofungwa na Kampuni ya Richmond, imeshabadilishwa umiliki wake mara mbili. Imetoka kwa Richmond ikanunuliwa na Dowans na sasa inamilikiwa na Kampuni ya Symbion ya Marekani. Lakini sisi kama taifa tumeachwa pale pale tulipokuwa Mwaka 2008.

Kwa kuwa kuna Mahakama ya Mafisadi inaundwa na sisi kama taifa tunayumbishwa na suala la mtu mmoja tu, ambaye si kiongozi wa serikali kwa sasa, nashauri Kesi ya Kwanza kwenye Mahakama ya Mafisadi iwe ni hii ya "Ufisadi" wa Edward Ngoyai Lowassa kuhusu Ufisadi wa zabuni ya ufuaji umeme iliyosababisha Sakata la richmond.

Ni lazima Lowassa ashitakiwe ili kama yeye anao ushahidi tofauti na ule ambao wapinzani wake wanao aje nao mahakamani ili upimwe kwenye mizani ya kisheria tujue nani mkweli kati yake yeye na wapinzani wake.

Haiwezekani mitambo ile iliyoletwa na Kampuni (Feki?) ya Richmond bado ipo nchini mwetu, inafua umeme, Tannesco wanalipa Capacity charges tanesco wanauziwa umeme kutokana na mitambo ile ile iliyokuwa ya Richmond, mkataba ule ule wa kati ya Richmond na Tannesco ndiyo umekuwa ukihuhishwa na Dowans na sasa Symbion, lakini sisi kama taifa bado tunakumbushana mambo ya mwaka 2008.

Kuukata Mzizi wa fitina ni lazima Lowassa na kama wapo na wengine waliohusika na sakata la Richmond wafikishwe kwenye Mahakama ya mafisadi mara tu Mahakama hiyo itakapoanza kazi. Tunataka Kesi ya kwanza kwenye mahakama hiyo iwe dhidi ya Lowassa na wenzake waliohusika na suala la Richmond.

KESI YA LOWASSA ISIPOKUWA YA KWANZA KWENYE MAHAKAMA YA MAFISADI NITASHANGAA KWELI KWELI!!
Msiba wa wengi harusi.
Utasubiri Sana

Haukumiwi mtu hapa.
 
Mnaongea sana Na hamjui nini sababu..... TATIZO NI KATIBA ikibadilishwa halo ndipo ataweza kushitakiwa. kwani mpaka Sasa jamuhuri inamlinda Na kumlipa Waziri mkuu mstaafu yeyote. we we unasema umshitaki MTU kwa mlinzi wake wapi uliiona hiyo.
 
Huu uzi ni wa kujikomba kwa watawala na ndo maana akaweka ID na picha wamfikirie.
Angalia hili shimo unalochimba lisikumeze wewe na wa kwenu.
 
aiiiiiiiiiiiiiiiiiii lowasa akipelekwa nahakamani wafu wote wajiandae kufufuka Siku hiyo nani ana ubavu huo??? nani akubali kuumbuka? akipelekwa ccm watakuwa wanamsema nani? tumieni vichwa kuwaza hii ni siri nzito na hiyo mahakama haipo labda yesu arudi kabla ya mda alohaidi, hiyo mahakama itamwacha nani katika ccm? escow ccm Richmond' ccm ,nyumba za serikali ccm nyamazeni hii siri ni nzito,
 
kwa hii serikali dhaifu ya ccm usitegemee kitu kama hicho. afu sasa cha ajabu utaendelea kuishabikia hiyo serikali wakati haiwezi kuchulia hatua za kisheria watuhumiwa, sasa sijui utakuwa mtu wa aina gani?!
Ucfikilie sheria,fikilia tufanye non nchi iendlee,co kuwa mnatupigia kelele kwenye majukwaa alaf hakuna kinachofanyika....
 
Ufisadi gani alioufanya lowassa,
Hivi inawezekana mtoto ndani ya nyumba akafanya jambo bila baba yake kujua kweli.

Aanze kustakiwa baba kwanza, halafu mtoto atafuata kutoa ushahidi.
 
Ucfikilie sheria,fikilia tufanye non nchi iendlee,co kuwa mnatupigia kelele kwenye majukwaa alaf hakuna kinachofanyika....

kwa huu mwandiko wako, nchi hii kuendelea ni nguma kama wananchi wenyewe ni wa aina yako
 
kwa huu mwandiko wako, nchi hii kuendelea ni nguma kama wananchi wenyewe ni wa aina yako
Pengne unachokisema ni sahihi kwa kufikilia kwako,lakin ili nchi hii iendlee lazm watu wa type yako ya kushabikia siasa bila kufikilia maendleo hakuna kitu mtafanya,.
 
Pengne unachokisema ni sahihi kwa kufikilia kwako,lakin ili nchi hii iendlee lazm watu wa type yako ya kushabikia siasa bila kufikilia maendleo hakuna kitu mtafanya,.

wrong, uwepo wa watu wenye akili finyu kama wewe hudumaza nchi kuendelea, mleta mada anataka lowassa ashtakiwe, nami nikamjibu 'kwa serikali hii dhaifu ya ccm asitegemee lolote' nawe ukakurupuka tokea wapi sijui! au ulitaka nimjibuje? ndiyooooo kama wabunge wa ccm!
 
Baada ya miaka mingi huko mbeleni hili swala likawekwa wazi kabisa kama yale ya kipindi cha mwalimu yalivyo wekwa wazi, tuombe uzima wandugu
 
Back
Top Bottom