Lazima Lowassa ashitakiwe kwa Ufisadi!!

Lazima Lowassa ashitakiwe kwa Ufisadi!!

EL alisema hakula hata senti tano ya Richmond.



Tangu siku hiyo simuamini mtu anayesema mzee ni Fisadi.
Kama vip aende
Mahakamani. Stop bitching.

Mbowe alipohojiwa kwanini kamleta mtu ambaye atashtakiwa soon.?

Alijibu.

HAWAJAKuRUPUKA

Wakati ccm wanamalizia mkutano wa kampeni mwanza.

Mkwere alithubutu kusema Richmond ni ya EL.
Kwa bahati mbaya Sana alilisema mwishoni, na hatukua na muda wa kujadili hili tena.

Muda ushapita.

Mwenye wivu ajinyonge.
 
Mi nawaambia Lowasa ashtakiw kwa lolot yet macho magsi waga anaongea tu litakalo toka mdomoni wake akiamuka tu vzr utasikia hv akiamuka vbya utasikia vile halaf baada ya sk mbili tatu kasha sahau alicho kisema
 
wanajua lowasa ni nan na ndio maana wana msakama maana tang kipind kile ni lowasa mpka kesho lowasa kwan hakun vitu vya ku discuss .
 
Tuna tatizo kubwa sana kwenye suala la uelewa miongoni mwa watanzania, hali hii inanitisha sana. Freeland umekiona kitu ambacho wengi hawajakiona!!
 
Mi nawaambia Lowasa ashtakiw kwa lolot yet macho magsi waga anaongea tu litakalo toka mdomoni wake akiamuka tu vzr utasikia hv akiamuka vbya utasikia vile halaf baada ya sk mbili tatu kasha sahau alicho kisema
Huu mwandiko wako huu..... Km wa... Hihihii
 
Ndiyo maana sisi wengine ambao tunaiona hii serikali ni Imara tunaihamasisha wampeleke Lowassa kwenye Mahakama ya Ufisadi, kinyume cha hapo wakae kimya!!
1470948791931.jpg
utakuwa unaota ndugu huo uimara wake Hebu thibitisha kwa
 
Kiashiria cha udhaifu kwa binadamu wakati mwingine ni pale anaposhindwa kulifikisha mwisho jambo la muhimu analotakiwa kulikamilisha. Sisi kama taifa tumekuwa tunatangatanga na Jambo lililosababishwa na mtu mmoja tu na sisi kama taifa tumeshindwa kufikia mwisho wake.

Tarehe 7/2/2008 aliyekuwa Waziri wa Mkuu wa Tanzania wakati ule, Edward Ngoyai Lowassa alijiuzulu wadhifa wake baada ya kutuhumiwa kuingilia mchakato wa Zabuni ya Ufuaji Umeme iliyosababisha kuletwa kwa Kampuni ya Ufuaji Umeme ya Richmond nchini. Tangu kujiuzulu kwa Lowassa mpaka sasa imeshapita miaka zaidi ya 8 na miezi kadhaa, lakini bado suala la sakata la Richmond halijaisha

Mitambo iliyoletwa na Kampuni ya Richmond ambayo bado ipo Pale Pale ilipofungwa na Kampuni ya Richmond, imeshabadilishwa umiliki wake mara mbili. Imetoka kwa Richmond ikanunuliwa na Dowans na sasa inamilikiwa na Kampuni ya Symbion ya Marekani. Lakini sisi kama taifa tumeachwa pale pale tulipokuwa Mwaka 2008.

Kwa kuwa kuna Mahakama ya Mafisadi inaundwa na sisi kama taifa tunayumbishwa na suala la mtu mmoja tu, ambaye si kiongozi wa serikali kwa sasa, nashauri Kesi ya Kwanza kwenye Mahakama ya Mafisadi iwe ni hii ya "Ufisadi" wa Edward Ngoyai Lowassa kuhusu Ufisadi wa zabuni ya ufuaji umeme iliyosababisha Sakata la richmond.

Ni lazima Lowassa ashitakiwe ili kama yeye anao ushahidi tofauti na ule ambao wapinzani wake wanao aje nao mahakamani ili upimwe kwenye mizani ya kisheria tujue nani mkweli kati yake yeye na wapinzani wake.

Haiwezekani mitambo ile iliyoletwa na Kampuni (Feki?) ya Richmond bado ipo nchini mwetu, inafua umeme, Tannesco wanalipa Capacity charges tanesco wanauziwa umeme kutokana na mitambo ile ile iliyokuwa ya Richmond, mkataba ule ule wa kati ya Richmond na Tannesco ndiyo umekuwa ukihuhishwa na Dowans na sasa Symbion, lakini sisi kama taifa bado tunakumbushana mambo ya mwaka 2008.

Kuukata Mzizi wa fitina ni lazima Lowassa na kama wapo na wengine waliohusika na sakata la Richmond wafikishwe kwenye Mahakama ya mafisadi mara tu Mahakama hiyo itakapoanza kazi. Tunataka Kesi ya kwanza kwenye mahakama hiyo iwe dhidi ya Lowassa na wenzake waliohusika na suala la Richmond.

KESI YA LOWASSA ISIPOKUWA YA KWANZA KWENYE MAHAKAMA YA MAFISADI NITASHANGAA KWELI KWELI!!
mzee naona bagi zimekuzidi naona hakuna kiongozi wowote wa ccm aliyekuwa sio mwizi na mla rushwa
 
Na hao mafisadi wote walio kwenye ccm mtawapeleka wapi? Ama ndio hao ambao watalindwa na Rais?
 
Aliye ccm na akawa safi atupe jiwe la kwanza la kumponda Mzee wetu Lowassa kichwa tumwone.
 
Nataka Lowassa apelekwe mahakamani. .full stop.
This is strange kwa sababu JPM kaanzisha mahakama ya mafisadi sasa kigugumizi cha kumpeleka lowassa mahakamani kama ushahidi upo kinatokana na nini?? Hata wewe kama law abiding citizen unaweza kufungua kesi ya ufisadi dhidi ya lowassa kama ushahidi unao nobody is above the law
 
Back
Top Bottom