Lazima Lowassa ashitakiwe kwa Ufisadi!!

Lazima Lowassa ashitakiwe kwa Ufisadi!!

Chadema haiwezi tena kua chama cha upinzani..kitabaki tu kua chama cha maandamano na fujo za kutafta kick mtaani
au dampo la kupokea uchafu wa ccm.lazma ashitakiwe mbivu na mbich zijulikane..
 
Chadema haiwezi tena kua chama cha upinzani..kitabaki tu kua chama cha maandamano na fujo za kutafta kick mtaani
au dampo la kupokea uchafu wa ccm.lazma ashitakiwe mbivu na mbich zijulikane..

Umeingia mzima mzima ,sasa utajitetea vipi !!!..
 
MANENO YA MWAKYEMBE ALIPO HOJIWA KUHUSU SAKATA LA RICHMOND
July 21 2016 Waziri wa katiba na sheria, Dk. Harrison Mwakyembe alikuwa akihojiwa katika kipindi cha Clouds 360 cha clouds TV na kujibu maswali mbalimbali yanayohusu katiba na sheria na hili sakata la Richmond likagusiwa.

Mtangazaji wa clouds TV, Hudson Kamoga alimuuliza Waziri mwakyembe kuhusiana na sakata la Richmond wakati akiwa mwenyekiti wa kamati iliyokuwa inachunguza sakata hilo ambapo walikuja na ripoti ambayo ilipelekea aliyekuwa Waziri mkuu kwa wakati huo, Edward Lowassa kujiuzulu. Hudson ametaka kujua kama kuna mambo ambayo watanzania hawakuyajua kuhusu sakata la Richmond

Waziri Mwakyembe amesema ….>>>‘kesi ya Richmond tuliifanya kwa roho safi na kwa kupiga magoti kwa Mungu na tuliifanya haki kwa kila mtu tulichoamua hata tuamue kesho asubuhi nirudie tena hata koma haitabadilika itakuwa vilevile na mimi nitafurahi sana’

>>>’chini ya kanuni tunaruhusiwa kuifufua tena Richmond ili ichunguzwe upya na ninaaapa wanaweza wote wakahama wakaniacha peke yangu na uhakika mimi mwenyewe nilichonacho nitajenga hoja sidhani kama kuna mtu hata mmoja atasalimika kwenda jela‘
Maneno yako matamu sana mkuu..keep it up! Napena mtu anapoongea awake REF ..sio mtu anajrna hoja kutokea kwenye nywele

Sent from my TECNO-Y3+ using JamiiForums mobile app
 
Kujifanya kwenu kujua kumesababisha mitambo isiwe ya kwenu,muliambiwa nunueni mudai mitumba,marekani wameweka mkwanja,umeme ni kwa mizani tu mtanunua.
 
Kiashiria cha udhaifu kwa binadamu wakati mwingine ni pale anaposhindwa kulifikisha mwisho jambo la muhimu analotakiwa kulikamilisha. Sisi kama taifa tumekuwa tunatangatanga na Jambo lililosababishwa na mtu mmoja tu na sisi kama taifa tumeshindwa kufikia mwisho wake.

Tarehe 7/2/2008 aliyekuwa Waziri wa Mkuu wa Tanzania wakati ule, Edward Ngoyai Lowassa alijiuzulu wadhifa wake baada ya kutuhumiwa kuingilia mchakato wa Zabuni ya Ufuaji Umeme iliyosababisha kuletwa kwa Kampuni ya Ufuaji Umeme ya Richmond nchini. Tangu kujiuzulu kwa Lowassa mpaka sasa imeshapita miaka zaidi ya 8 na miezi kadhaa, lakini bado suala la sakata la Richmond halijaisha

Mitambo iliyoletwa na Kampuni ya Richmond ambayo bado ipo Pale Pale ilipofungwa na Kampuni ya Richmond, imeshabadilishwa umiliki wake mara mbili. Imetoka kwa Richmond ikanunuliwa na Dowans na sasa inamilikiwa na Kampuni ya Symbion ya Marekani. Lakini sisi kama taifa tumeachwa pale pale tulipokuwa Mwaka 2008.

Kwa kuwa kuna Mahakama ya Mafisadi inaundwa na sisi kama taifa tunayumbishwa na suala la mtu mmoja tu, ambaye si kiongozi wa serikali kwa sasa, nashauri Kesi ya Kwanza kwenye Mahakama ya Mafisadi iwe ni hii ya "Ufisadi" wa Edward Ngoyai Lowassa kuhusu Ufisadi wa zabuni ya ufuaji umeme iliyosababisha Sakata la richmond.

Ni lazima Lowassa ashitakiwe ili kama yeye anao ushahidi tofauti na ule ambao wapinzani wake wanao aje nao mahakamani ili upimwe kwenye mizani ya kisheria tujue nani mkweli kati yake yeye na wapinzani wake.

Haiwezekani mitambo ile iliyoletwa na Kampuni (Feki?) ya Richmond bado ipo nchini mwetu, inafua umeme, Tannesco wanalipa Capacity charges tanesco wanauziwa umeme kutokana na mitambo ile ile iliyokuwa ya Richmond, mkataba ule ule wa kati ya Richmond na Tannesco ndiyo umekuwa ukihuhishwa na Dowans na sasa Symbion, lakini sisi kama taifa bado tunakumbushana mambo ya mwaka 2008.

Kuukata Mzizi wa fitina ni lazima Lowassa na kama wapo na wengine waliohusika na sakata la Richmond wafikishwe kwenye Mahakama ya mafisadi mara tu Mahakama hiyo itakapoanza kazi. Tunataka Kesi ya kwanza kwenye mahakama hiyo iwe dhidi ya Lowassa na wenzake waliohusika na suala la Richmond.

KESI YA LOWASSA ISIPOKUWA YA KWANZA KWENYE MAHAKAMA YA MAFISADI NITASHANGAA KWELI KWELI!!
Umeandika ukiwa umetawaliwa na chuki binafsi,we umemuona ENL peke yake,umemuacha aliyekua na mamlaka juu zaidi na ambae ndie aliipokea Symbion,JK.Mtaumbuka wenyewe

Sent from my TECNO-J7 using JamiiForums mobile app
 
Labda iwe matumizi ya mahakama hiyo yaanze kutumika tangu kuanzishwa kwake kwa kuangalia makosa ya kuanzia utawala wa aliyeianzisha.... Maana kama itaangalia makosa yote hata yaliyotokea kabla ya kuanzishwa mahakama hiyo.. Basi kuna kundi kubwa sana hapo litaunganishwa.... Maana ufisadi wa nchi hii unafanywa kwa teamwork..... Ngoja tuone..

Sent from my HUAWEI G750-U10 using JamiiForums mobile app
 
Kwani hii nchi tangu imeanza fisadi wa kwanza ni lowassa mpk aanze yeye kupelekwa mahakamani?????au kwa sababu amehama chama???kwani ndani ya ccm mafisadi hakuna mpk leo????
 
Unawatafutia matatizo wale unaodhani wapo salama kwa hli zakumuandama EL. Kabla hujaropoka muulize mzee wa msoga kwanin amelikalia kimya hili jambo, jibu utakalo pata utaomba upewe uhamisho ukakae sayari nyingine.
 
Hakuna wa kumpeleka mahakamani,,kwa sababu hawana hoja za msingi ingekuwa ni fisadi sasa hivi angeshawajibishwa.
 
Nyie mnaolopoka vile mna ushahidi au mnajifurahisha tu we ni mtanzania chukua jukumu LA kumshtaki utasikilizwa unawategemea wampeleke wameshindwa mpelekeni nyie sasa.....tulizeni munkari sidhani kama mnajua hii issue kwa undani.
 
Kumbe unashauri? Sasa unashauri na kichwa cha habari kinasema NI LAZIMA? umejitahidi kiasi kuandika lakn ni upuuzi mtupu! Kuna mafisadi papa na bado wapo kila kona ya nchi, hujawasemea! Mnamwogopa sana lowassa nyie ccm!! Zamu hii mtaisoma namba!!! Tanzania bora inakuja!
 
Huyu jamaa afikirii na hajui kma casa ni uchawi so acha kurudisha mmbo yalio pita
 
Back
Top Bottom