Lawrence Mafuru aliewahi kuwa MD wa NBC Bank na Msajili wa Hazina ateuliwa kuwa Kamishina wa Sera Wizara ya Fedha

Mkuu The Underboss , naielewa concern yako, lakini ukweli ni kuwa japo tuna Watanzania wengi wenye sifa na vigezo vya kwenye macheti tuu, lakini the people who can delivery ni wachache, ukiwabaini huwezi kuzuia recycling them, huyu ni one of them, he is good na hapo ni just a stepping stone kwenye bouncing back nafasi yake halisi bado.

Mafuru ni Mmoja wa Mashujaa wa Taifa Hili, Kwa Kuwa Mkweli Daima, Jee Kupangiwa Kazi Muhimu Zaidi?.
P
Acha zako P. Kwani akina Mafuru (sio zile samaki zenu za kubanika kanda ya ziwa) wana makaratasi yasiyo vyeti? Hao wenye vyeti wenyewe wanapewa wapi nafasi kupractise ili wawe competent na.wawe hazina ya nchi baadae...matokeo yake hawapewi nafasi zinafichwa wanapigwa vita na nafasi wanazungushiana wao kwa wao ndani kwa ndani kimtandao na kujuana vizazi na vilinge.

Sent from my SM-G9350 using JamiiForums mobile app
 
Mafuru huyo huyo mwezi mmoja uliopita aliteuliwa na January Makamba kuwa mjumbe wa bodi ya Tanesco.

Kipindi cha Magufuli, huyu Mafuru alitimuliwa kutoka serikalini kwa kashfa za kifisadi, na sasa anarejeshewa vitu vyote vinono.

Tutaonana mengi sana chini ya CCM.
ufisadi upiii, sema alimshauri jiwe kupitia clouds tv masuala ya sera za uwekezaji na mitaji kipindi jiwe anafrustrutisha wawekezaji jiwe akamfurusha, brain kama kina mafuru ni mali ya rais ana haki ya kuwatumia pale wanapohitajika, nchi ina watu wengi lkn wataalam wabobezi ni wachache, si kila post unachukua kila mtu, watu kama kina mafuru unawachukue waweze kunoa au kuandaa wengine watakaokuja, siyo mafuru tu, maserikalini watu wngi wanastaafu na wanaongezewa mikataba ya kuendelea kuhudumu kwa sababu ya taalumana ubobevu wao,cha muhimu acha makasiliko watakie watu heri, ridhki zao haziwez kukwamisha ridhki yako wewe!!
 
Ndugu Laurence Mafuru Ambae amewahi kua mkurugenzi Mkuu wa NBC Bank na Msajili wa Hazina ameteuliwa kua kamishna wa Sera wizara ya fedha.

Hakuna mahala uteuzi huo umetangazwa ila nimebahatika kuona tangazo kutoka kwenye taasisi yake ya Bankable Institute kwamba amejiuzuru majukumu ya mshirika mtendaji (managing partner) kutokana na kuteuliwa kua kamishna wa sera wizara ya fedha.

Sina tatizo na uteuzi wa Mafuru, najua ni mtaalam mbobezi, mjuzi, ana uzoefu maarifa makubwa lakini swali langu ni kwa nini watu ni wale wale.

Kwamba nchi hii mtandao ni ule ule ndio unatakiwa kula keki ama neema ya nchi hii, watu wale wale. Nilishangaa juzi Balozi Batrida anateuliwa katibu tawala wa mkoa baadae mkuu wa mkoa, unajiuliza mtu amekua hadi balozi bado hawezi kuishi bila kuajiriwa?

Mafuru ana taasisi yake ya Bankable Institute, ambayo bado kama atahitajika kusaidia taifa basi ni rahisi kumpata ama kupata ushauri wake kupitia hiyo taasisi na akaendelea kuneemeka na mema ya nchi hii.

Sijawahi kusikia mtu kutoka taasisi ama sekta binafsi amepewa nafasi serikali akaikataa, sijawahi kusikia, simaanishi hawapo ila sijawahi kusikia.

Hii inatupatia picha kwamba kujiajiri bado ni changamoto ndio maana watu watazuga wamejiajiri ila ikitokea ofa za serikali hawawezi kuzikataa, kwa maana kwamba maisha ya utumishi serikalini ni mazuri na matamu kuliko kujiajiri.

Hii nchi ina watu milioni 60, kwa nini kila siku ni wale wale tu, wanatoka hapa wanaenda pale, wanatoka huku wanaenda kule.

CCM wametemgeneza mfumo wa hovyo sana wa nchi hii.

View attachment 1996590
Mzee Mwinyi Amekua Rais wa Zanzibar kisha Tanzania na sasa anamshuhudia mwanae akiwa Rais wa Zanzibar hata mimi Mwalubadu Mang'ombe alikua fundi muashi na leo hii anamshuhudia mwanae akiwa fundi muashi.

Wivu humuua mtu mjinga kijana.
 
Mkuu The Underboss , naielewa concern yako, lakini ukweli ni kuwa japo tuna Watanzania wengi wenye sifa na vigezo vya kwenye macheti tuu, lakini the people who can delivery ni wachache, ukiwabaini huwezi kuzuia recycling them, huyu ni one of them, he is good na hapo ni just a stepping stone kwenye bouncing back nafasi yake halisi bado.

Mafuru ni Mmoja wa Mashujaa wa Taifa Hili, Kwa Kuwa Mkweli Daima, Jee Kupangiwa Kazi Muhimu Zaidi?.
P
You mean PST!!!? Time will tell
 
Back
Top Bottom