LATRA yawataka wenye mabasi ya abiria kuanza kutumia tiketi za mtandao, watakaoshindwa kufanya hivyo kufutiwa leseni

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,730
218,299

Mamlaka ya Usafiri wa Ardhini ( LATRA ) imetangaza kwamba hadi kufikia January 6 mwaka 2021 mabasi yote yawe yameanza kutumia tiketi za mtandao, vinginevyo watafungiwa kutoa huduma hiyo .

Bado haijajulikana sababu hasa za wenye mabasi ya abiria kulazimishwa kufuata utaratibu huu mpya huku wakitozwa kodi lukuki ambayo wanailipa bila mizengwe yoyote

Tahadhari: kama una safari ya muhimu ni bora ukafanya hivyo kabla ya tarehe hiyo, maana lolote la kukukwamisha laweza kutokea .

Nakulilia Tanzania

===============

 
Sasa mtu wa buchosa ndani ndani akitaka ticket na kwenye mambo ya kutumia mtandao yuko chini inakuwaje hapo

Ova
Moja ya sifa kubwa ya serikali ya Tanzania kufanya maamuzi kwa kushtukiza, bila kushirikisha wadau au kufanya pilot study. Na maamuzi yao siku zote yanakuwa ni amri zinazotolewa on short notice. Hili agizo halitekelezeki kirahisi na litaleta shida kubwa.
 
Wao wanafikiri kila mtu ana accses ya kutumia mtandao ....

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
 
Nakwenda ARK tokea Mlandizi....vipi kuhusu hiyo tiketi ya mtandao
Bus limeharibika njiani tunahitaji refund tuendelee na safari itakuwaje wakati pesa yoote iko kwa mtandao
Bonge la point, ila serikali inataka makusanyo hata kwa miguvu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…