LATRA yaokoa jahazi abiria wa Rombo

Jun 20, 2023
54
51
Kama mnavyojua ndugu zetu wachaga wanavyosifika kurudi makwao mwishoni mwa Mwaka au "kwenda kuhesabiwa"kama inavyojulikana na wengi,basi idadi ya mabasi ya kuwasafrisha huwa inazidi namba ya abiria.
Kutokana na Hilo,Maofisa wa Mamlaka ya udhibiti wa usafiri wa ardhini(LATRA)katika mkoa wa kilimanjaro walilaziklmika kupiga kambi kwenye stendi kuu ya mabasi mjini Moshi lengo ni kuhakilisha abiria wote wanapata usafiri na bila kulanguliwa na wenye mabasi.
LATRA kupitia Afisa mfawidhi wake mkoa wa Kilimanjaro,Paul Nyello,walilazimika kutoa vibali vya kusafrisha abiria kuelekea wilaya ya Rombo na maeneo mengine,Marangu,Mwika,Mkuu Hadi Tarakea Kwa Coaster za kukodi ziitwazo "Special Hire"ambazo zimekuwa maarufu sana katika siku za hivi karibuni.
Paul amezungumza na waandishi wa habari na kueleza kuwa,walifanya ukaguzi wa njia zenye uhitaji mkubwa wa abiria pamoja na kuchukua hatua Kwa mabasi yaliyobanika kuvunja sheria Kwa kuzidisha nauli.
Anasema tangu Desemba 23 kulikuwa na mahitaji makubwa ya usafiri kutokana na idadi kubwa ya watu waliokuwa wanasafiri kutoka Mjini Moshi kwenda wilayani.
"Kama mnavyojua mwisho wa Mwaka wananchi wengi wanasafiri kwenda makwao hivyo kuwepo na mahitaji makubwa ya usafiri yanayotokana na ongezeko kubwa la abiria"
"Tangu jumamosi ya Desemba 23 njia kama ya Moshi mjini kuelekea Marangu,Mwika,Mkuu Hadi Tarakea wilaya ya Rombo kulikuwa na abiria wengi sana hivyo LATRA ikazungumza na wenye coaster za kukodi "Special Hire "ili kupeleka abiria kwenye maeneo hayo Kwa nauli rafiki bila kuwaumiza abiria"
"Yapo pia mabasi makubwa yalitoa huduma ya kusafrisha abiria kwenda wilayani hasa Tombo na tushirikiana na wenzetu wa usalama barabarani kuhakikisha abiria wote wanapata usafiri"
"Ninyi waandishi wa habari ni mashahidi,mmeona jinsi abiria walivyokuwa wengi,hivyo mnawajibu wa kutoa taarifa sahihi Kwa kuwasiliana na LATRA ili kuepuka upotoshaji"
Wilaya ya Rombo pekee inatajwa kuwa na mabasi makubwa zaidi ya 15 yanayoanzia safari zake katika mji wa Tarakea kuelekea maeneo mbali mbali ya nchi kutokana na kuwa na idadi kubwa ya abiria.
 
Back
Top Bottom