LATRA ajali za usiku zisiwafanye mbadili maamuzi, wapeni madereva muda wa kuzoea safari za usiku

fazili

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
13,824
18,568
Uhuru wa abiria kusafiri usiku ni muhimu mno kwa maendeleo yetu. Unatoka Arusha saa 10 jioni unafika Dar saa 10 asubuhi. Unafunga mzigo wako mchana jioni saa 10 unakamata BM unarudi Arusha asubuhi saa 10 upo Arusha. Biashara inaendelea.

Madereva wa mabasi wanahitaji muda kidogo kuweza kuzoea kuendesha usiku.

Nawashauri LATRA msibweteke na ajali za mabasi usiku kwani ni suala la muda tu ajali hizo zitapungua na kuwa kiwango cha kawaida. Tunahitaji sana usafiri wa usiku kufanikisha mambo yetu watanzania.
 
Kesho akifa ndugu yako urudi hapa kuendelea kuwasisitiza.

Huwa inauma sana ajali ya kizembe inapoondoa uhai wa baba wa mtu,mke wa mtu anayeacha watoto wadogo mayatima.
 
Ajali za bodaboda zilikuwa nyingi mwanzoni karibu serikali ingepiga marufuku biashara hii ila sasa zimepungua sana.
 
Bro usiseme zimepungua sema ni kwa sababu wewe taarifa huzipati au hajaguswa mtu wako unaemjua.

Mwezi jana nimezika jamaa zangu wawili walikanyagwa na kichanja zile lorry za kupakia container pale Uhasibu juzi jumatano nimezika mwengine amefia Kibanda cha Mkaa ajali zipo siyo jambo la masihara kinasikitisha zaidi mtu anakufa anaacha watoto aged 2&4½.
 
Uhuru wa abiria kusafiri usiku ni muhimu mno kwa maendeleo yetu. Unatoka Arusha saa 10 jioni unafika Dar saa 10 asubuhi. Unafunga mzigo wako mchana jioni saa 10 unakamata BM unarudi Arusha asubuhi saa 10 upo Arusha. Biashara inaendelea.

Madereva wa mabasi wanahitaji muda kidogo kuweza kuzoea kuendesha usiku.

Nawashauri LATRA msibweteke na ajali za mabasi usiku kwani ni suala la muda tu ajali hizo zitapungua na kuwa kiwango cha kawaida. Tunahitaji sana usafiri wa usiku kufanikisha mambo yetu watanzania.
Na madereva nao waache mawenge.Waimarishe afya zao kwa kula vyakula bora,kupumzika na kuondokana na misongo ya mawazo/ulevi.Waimarishe uoni/macho yao kitaalamu/milo hitajika kulikabili giza.
 
Madereva hawaba nidhamu, wanakimbia usiku kama vile ni mchana...
 
Back
Top Bottom