Latest: Asha-Rose Migiro the new UN Deputy General Secretary

Kwa mujibu wa Uhuru habari hiyo hii hapa...

Asha-Rose Migiro bosi UN
Ateuliwa Naibu Katibu Mkuu

Na Mwandishi Wetu
KATIBU Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amemteua Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania, Dk. Asha-Rose Migiro (50), kuwa Naibu Katibu Mkuu wa umoja huo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mwandishi wa Habari Msaidizi wa Rais, Maura Mwingira, uteuzi wa Dk. Asha-Rose ulifanywa na kutangazwa jana katika kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa huko New York, Marekani.

Dk. Asha-Rose anachukua nafasi ya Mark Malloch Brown wa Uingereza aliyekaa katika wadhifa huo tangu Aprili, mwaka jana. Kabla ya Brown, nafasi hiyo ilikuwa ikishikwa na mwana mama Louise Frechette wa Canada.

Kutokana na kuteuliwa huko, Rais Jakaya Kikwete, alisema hiyo ni heshima kwa Tanzania na Afrika kwa jumla kwa sababu ni mwanamke wa kwanza kushika wadhifa huo tangu kuanzishwa kwa umoja huo mwaka 1945.

Rais Kikwete alimsifu Dk. Asha-Rose kwa kusema anajua ameteuliwa kwa sababu ana uwezo wa kushika wadhifa huo na kutekeleza dhamana aliyopewa.

Kufuatia kuteuliwa katika wadhifa huo mpya, nafasi ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa aliyokuwa akiishikilia, sasa inabaki wazi.

Uteuzi huo unaweka historia mpya kwa Tanzania na nchi za Afrika Mashariki, Kati na Kusini katika Umoja wa Mataifa kwa kutoa mtu wa kushika wadhifa huo.

Kabla ya uteuzi huo, Dk Asha pia alikuwa ameweka historia ya kuwa mwanamke wa kwanza kushika wadhifa wa waziri mwenye dhamana ya mambo ya nje nchini tangu kupatikana kwa uhuru mwaka 1961.

Dk. Asha-Rose Migoro alizaliwa mwaka 1956 na kupata elimu ya msingi Mnazi Mmoja, Dar es Salaam kuanzia mwaka 1963 hadi 1966 na baadaye kuendelea na elimu hiyo katika shule ya Korogwe kati ya mwaka 1967 hadi mwaka 1969.

Baada ya hapo aliendelea na masomo ya sekondari katika shule ya Weruweru mkoani Kilimanjaro mwaka 1970 na kuhitimu mwaka 1973. mwaka uliofuata alijiunga na shule ya sekondari ya Korogwe kwa masomo ya kidato cha tano na cha sita ambapo alihitimu mwaka 1975.

Mwaka 1977, alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa masomo ya shahada ya kwanza ya sheria ambayo alitunukiwa miaka mitatu baadaye.

Alijiunga na chuo hicho hicho mwaka 1982 kwa shahada ya pili ya sheria na kuhitimu mwaka 1984. Mwaka 1988, alihitimu shahada ya uzamivu (Ph.D) katika sheria kwenye Chuo Kikuu cha Konstanz nchini Ujerumani.

Kwa upande wa ajira, aliajiriwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akiwa mkufunzi msaidizi mwaka 1981 na baadaye kupanda katika ngazi za mhadhiri msaidizi, mhadhiri hadi mhadhiri mwandamizi, cheo alichokuwa nacho mpaka mwaka 2000 alipoingia kwenye siasa.

Katika mwaka huo, aliamua kuingia kwenye siasa na kugombea ubunge wa Viti Maalum kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa upande wa taasisi za elimu ya juu.

Baada ya kumalizika kwa uchaguzi, aliteuliwa na Rais wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa kuwa Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, nafasi aliyoishika hadi mwaka 2005.

Januari, mwaka huu, aliteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa hadi kuteuliwa katika wadhifa wake mpya kwenye Umoja wa Mataifa.

Vile vile, Dk. Asha-Rose kisiasa ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) na Katibu wa Idara ya Siasa na Ushirikiano wa Kimataifa ya NEC. Kwa nafasi hiyo ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM.
 
Huenda Balozi Seif Iddi akaingia, na Mahiga anaweza kupigwa na ubunge na hapo hapo kuwa naibu waziri mambo ya nje.
 
Jasusi,
Si unaona mwenyewe, matunda ya mzee wetu kunyamaza sasa hivi, dada zake wanaendelea kupeta tu, ni mambo ya mlo tu haya...
 
Kwani vipi Alhaj Balozi Kagasheki (MB) wa Bukoba Mjini umri wake unamruhusu kuweza kupata ulaji kwa mara nyingine pale foreign?
 
Waziri wenu mpya wa mambo ya Nje..... Dr. Emmanuel Nchimbi... aliyesoma.... bla bla bla blah.. na kupata shahada yake ya udaktari toka .....
 
Badala ya huyo doktari, si bora EL ndiyo achukue hiyo nafasi...JK atumie mwanya huu kufanya mabadiliko ya waziri mkuu na amtose rafikiye kiaina hasa kwa kuzingatia kuwa ameanza kunyemelea hiyo nafasi ya raia namba moja, na kwa vile naye anapenda sana kusafiri nje ya nchi!
 
sidhani kuchaguliwa kwake kutatusaidia kwa lolote na haswa kwa wanaojua inner working of UN

Ni nzuri kwa sababu ya career development kana career diplomat but not otherwise

wasi wasi wangu ni kuwa if she will live up to MARK MALOCH BROWNS interllectual and personal charisma in an era which UN is more popular as alame oranisation infested with their blue helmet peace keepers who double as rapists and issues such as ongoing genocide in Darfur,conflicts in Iraq and somalia
 
Kweli rushwa ni kubwa sana .Yaani Ban na Kora kusini wameumua kulipa takrima. Ndiyo maana nasema pomgezi kwa Mama ni sawa lakini kumbuka huu ni mchoro wakati wa kumpa Moon kura za kumuunga Mkono UN.
 
Mafuchila,
kwi!kwi!kwi. Sasa imebaki zamu ya Mdosi. Naye kisharudi kimya kimya.
Dr WHO,

Kuchaguliwa kwa Asha Rose kutasaidia. Atakuwa na nafasi ya kuchagua Watanzania katika kundi la wasaidizi wake. Mtanzania anapoukwaa najihisi na mimi nimeukwaa. Kwa hiyo kutasaidia.
 
Natoa pongezi za dhati kwa dr mama Migiro,... ametupa heshima na amechaguliwa kwa kuwa anaweza, Tanzania ni nchi inayoheshimika sana kwenye anga za kimataifa. Heshima imerudi tunapompongeza mama Migiro, tuwakumbuke wana wa Tanzania kama Salim Ahmed Salim [aliyepikwa na mwalimu na kukaribia kuwa katibu mkuu akakosa kwa sababu ya veto ya marekani, enzi ya vita baridi] Getrude Mongela[mama beijing] , balozi Mahiga , Anna Kajumulo Tibaijuka[un undersecretary based in NAIROBI] naamini kabisa utendaji wa watanzania hawa ndio umechangia kiasi kikubwa nchi yetu kuendelea kuheshimika kimataifa.

Kama ingekuwa mimi ni mshauri wa JK ningemuomba amchague dr Maiga Augustine, anao mchango mkubwa kwa taifa na usalama kwa ujumla, pia amefanya kazi kubwa security council, alitoa mchango mkubwa kuzima mapinduzi ya 1983,,, ni assset, jana naibu waziri wa mambo ya nje[Afrika] aliambatana na Maiga kwenye mkutano wa amani wa Somalia uliofanyika mombasa.... if we are serious as region diplomatic and strategic centre lets settle for Maiga,,...
 
Hii si Takrima ? Huyu kachaguliwa ama kateuliwa ? Hongera sana Migiro ila mambo ya Takrima hadi UN ?
 
Lunyungu

Hapa tena mzee hapana unavuka mpaka; Ameteuliwa kutokana na sifa ndugu yangu - sasa hata kazi za UN tusizipate? Hili swali ndugu yangu sio hapa Uzalendo uko wapi?
 
Asha Rose si anatoka CCM, CCM haina viongozi wazuri, viongozi wote wazuri wako upinzani!! ama....Wacha lazima uelewe motivation za watu hapa. Hata kikipendeza vipi hawakisifii, wanatafuta kuona doa liko wapi!
 
Nimeuliza hivi baada ya kuona watu wanavuka mipaka na kuanza kusema Hongera JK japokuwa ndiye head stat na najua CCM watachukua issue kuwa ya mafanikio kwa CCM kuturubuni lakini ukweli ni kwamba Mama ana uwezo sawa lakini si Takrima hii ?


Tanzania hongera siachi kusema hongera na uzalendo ni huo lakini ukweli wa takrima tutaukimbia vipi ? Maana mchoro uko wazi how it started na Ban alisema atalipa fadhila akiwa Dar .Je si ukweli ?
 
Lunyungu, hiyo inaitwa siasa! politics, Umoja wa Mataifa ni sehemu ya siasa pia! Kama tulimpigia kura, na yeye akatukumbuka hakuna ubaya! ni sehemu ya siasa. Deal za namna hiyo zinafanyika kila siku katika kumbi za siasa duniani. Wapinzani wangekuwa na wabunge wengi Bungeni wangelielewa hili.
 
Kwa kweli inasikitisha kwani hizi habari kwa watanzania wengi wanaotembelea kijiwe hiki imekuwa ya kwanza kutoa habari hii - Nafikiri hata vyombo vya habari vya bongo vingi wamekuja hapa kwanza. Angalia BBC, CNN na SKY News nimesearch hawajaiweka lakini angekuwa ni raia wa UK au US ungeiona.

Credibility ya hiki kijiwe inaharibika kwa mambo ambayo hayani kichwa wala mkia. tunafahamu USA wana ubavu mkubwa tu pale UN hupiti mpaka wakubali, wale ambao wanakumbuka Salim Ahmed Salim jinsi USA walivyomkataa, leo hii dada yetu amepata basi imekuwa nongwa tena i.e. Takrima. I don't have any words for it.

Kama mtanzania atachaguliwa popote pale ulimwenguni hata kwa njia ambazo hazikubaliki mimi binafsi nitamsupport maana nchi za magharibi ndio wametuibia vya kutosha hivyo inabidi tuanze kurudisha mali walizoiba. Na wao ndio chanzo kikubwa cha rushwa zinazoendelea.
 
Hongera Migiro. Tanzania juu lakini kuna hatari kubwa inakuja kisiasa Tanzania . Watu wameanza kusema utendaji wa JK umempa nafasi Waziri wake . Mimi ndicho nimepinga . Narudia tena Hongera sana lakini wa CCM msije na hoja za kutuonyesha Ubora wa CCM hadi Migiro kapatikana maan tunajua kilicho endelea. Nitakuwa blunt na nasimamia maamuzi yangu . Nasema Hongera lakini .................................
 
Hii itatusaidia sana katika kuitangaza Tanzania. Fikiria kila atakaedeal na DR Migiro atakuwa anajua tanzania ipo wapi as a courtesy, tumeshatoa wanawake vichwa na wametusaidia katika medani ya kimataifa kama vile MAMA TIBAIJUKA, MAMA MONGELLA NA Sasa Mama Migiro.

Kuna mmoja kahoji ina maana ile minong'ono ya rushwa ni kweli?! Kwamba huu uteuzi ni ''hongo'' kwa vile tuliipigia debe Korea kupata kiti hicho....well basi hii ni rushwa nzuri na tuzipokee kwa wingi....

Ama kuhusu nani wa kumrithi Foreign, my answer is there are plenty,tuna rasilimali ya vichwa vizuri tanzania ni position inayohitaji umakini fulani...na pili haitojazwa haraka haraka kwa vile sasa hivi kuna nafasi mbili katika baraza la mawaziri zipo Vacant...ya marehemu akukweti na hii ya mama Migiro.

Pia kuna nafasi mbili za ubunge.....
 
Back
Top Bottom