Mkuu maharage yanalipa kwa sababu unaweza ukayakausha na kusafiirisha kiangazi,njegere mbichi ni ugonjwa wa moyo. Halafu hiyo shaba naiogopa kama ukoma. Mimi nacheza na vitu vya kawaida sana,havina BP wala nini. Ni nguvu zako tu. Kibakwe imekosa barabara,kuna utajiri ile mbaya. Turudi ktk hoja, kule nilikosema mwanzo,siwezi kufuga mbuzi? Tamaa yangu nifuge mbuzi kule Itigi/Chunya na nyuki kwa wingi na nilime alizeti. Ukanda ule bado fresh au unasemaje mkuu?
Malila
Kikubwa hapa ni ubora wa mbuzi, ninavyoona mimi na kwa vile nimeshafanya na kufanikiwa ni kuweza kupata eneo kubwa karibu na Dar hata kama ni kibaha kwa ajili ya mradi wa kuboresha mbuzi, soko la mbuzi ni kubwa sana Dar, kinachotakiwa ni kuleta mbuzi kutoka Singida, Shiyanga na Tabora halafu ukawaweka katika intermediary ranch/farm, hapo wakifika una wapa na kuwapiga sindano za dawa ya minyoo (deworms), unawaogesha na deep, una wapa multi vitamins pamoja na kuwapa antibiotics (OTC) kwa magonjwa mbali mbali, zaidi unajitahidi kuwapa grains (pollards, pumba za mahindi) na health value ingridients kama mashudu ya pamba na alizeti na majani kama luceni
mkuu.... baada ya mwezi mmoja utaona product hiyo ya mbuzi itakuwa na kiwango kikubwa sana, kwanza wataongeza uzito, pili watakuwa katika hali ya usafi, tatu watakuwa na uwezo mzuri wa kuzaliana
kikubwa ni kujaribu kuchagua mbuzi wengi wa kike tena wenye mimba pale unapokua unanunua hawa mbuzi mnadani au kwenye maboma ya watu, jitahidi kuwa castrate madume na ubakize machache, kuna kifaa maalum cha kufanya hiyo kazi kinaitwa badizzo kiko kama mkasi hivi
tengeneza banda la mabanzi ambalo ni suspended na flooryake iwe ni ta mabanzi ambayo inatengenezwa in treli like (kama chaga za kitanga, yaani inakuwa na gaps kila baada ya banzi na banzi) ili kuruhusu vinyesi kupita,
ku control stock tumia ear tags zenye namba au alama fulani na kila unapouza una itoa na ku stock out kwenye kitabu chako cha stock .......mbuzi hawa watazaliana kwa wingi kila mara na pia utakuwa ukiendelea kununua stock mpya kila baada unavyo uza stock yako,
amini mkuu.... soko la mbuzi ni kubwa na lilinishinda, nilifanya kama hobby au part time lakini sikutegemea inaweza kuwa project per se katika kashamba kangu bagamoyo ..... watu wengi hupenda kununua mbuzi ambao wanafugwa kwa style ya livestock farming (goat meat farming) na siyo mbuzi wa machungani kama wa masai na wasukuma
nilijaribu mbuzi wa maziwa ambao stock yeke ilitoka Uingereza walioletwa kwa mradi wa kusaidi waathirika kibaha .... du nilichemsha ... yaani wapo delicate vibaya sana
Malila ... wazo lako la project ya mbuzi wa nyama ni zuri sana