Last night at KFC mikocheni

UrbanGentleman

JF-Expert Member
Jun 19, 2016
2,590
2,000
Salaam waungwana vipi ma saga ya serikali mnayaelewa!! ? Hahaha msivunjike mioyo ishu ni kufocus kwenye mambo yetu muhimu

Well Jana usiku nilitoka kumeet na one of my family friend alipatwa na matatizo sasa wakat narudi kwangu Mke Wangu akashauri tupitie KFC pale mikocheni ili tupate dinner ndio turudi sikumpinga nilipofika nikaingia kushoto tukaenda kula pale

Wakati tuko pale nakula chakula sababu Mimi nilikaa yeye akaenda kutoa order alivyo rudi ndio akawa ananiambia kuna mdada yuko pale ananiuliza kua yule mkaka ni Mume wako wife akashangaa akamwambia ndio vipi unamfahamu? yule binti akamwambia nahisi namfananisha.

Sasa kumbe Mke Wangu hakutaka mengi akamwambia njoo unaweza kuja kumsalimia kama unfahamu basi yule binti akaja pale.

At first nikawa namkumbuka ila sio kivile akaja yuko ulisoma mlimani UDBS? nikamwambia ndio akanikumbusha tukakumbukana tukawa tunacheka nikamwambia karibu tukae hapa Niko nimekuja Mara moja tuu huyu ni Mke Wangu akaniambia nimehisi hata hivyo hongera kwa Mke mzuri huku akamwambia Mke Wangu hongera kwa mume mzuri basi tukawa tunaongea tunakumbushana miaka hiyo huyu yuko wapi yule nani yah it was funny

Sasa wakati tunaendelea kula baada ya dakika kama kumi akaingia jamaa amemshika binti was kidar es salaam kuanzia mavazi mpaka muonekano wale mabinti mimi huwa nawaitaga mapython yani wezi wa wame za watu nikiwa nastaajabu huku naangalia hee yule binti tuliye kuwa nae akawa haelewi anajisemesha nimemkosea nini Mungu!? Mke wangu akamuuliza vipi uko sawa kama amejawa na hasira ghafla nikawa namuita vipi unatatzo lolote?

Yuko yule ni Mme Wangu mi na Mke Wangu tukawa tunaangaliana tunashangaa sabu ilikua kama filamu nikataka kumuuliza sasa unafanyaje akanyanyuka anataka kuwafata walipokaa nikamwambia ngoja hiyo sio njia sahihi kua muungwana uobserve angalia what is he into wanaweza kua marafiki japo walivyoingia wameshikana ilikua ni wazi wapenzi lengo langu ilikua kumpunguza jazba japo sikufanikiwa.

Alisogea mpaka pale akwamwagia vitu sasa cha ajabu yule Python yaani mchepuko akawa anaongea maneno ya kishenzi kwa mwenye Mme wake mpka nikajisikia vibaya yule binti akawa anasema sitaki maneno mengi tuachane niache na maisha yangu ata kama sijajaaliwa mtoto na wewe lakini not to this extent umenikosea sana we mwanaume .

Ikabidi nimzuie nimtoe nje nikamwambia Mke Wangu kaa nae kurudi ndani nakuta lijamaa limebaki linagombezwa na mchepuko nikajisikia vibya nikamfata yule binti nikamwambia hapa ni sehemu ya biashara after all yule ni mke wake jaribu kustaarabika huku nikimuonesha ishara ya kucalm japo hakuelewa kabisa nikamgeukia jamaa namwambia kaka mambo kama haya yanapotokea tunakua upande wa wake zetu sio hawa wakuokoteza hata hivyo pole na samahani sijui what is in yo marriage lakini nashauri mfate Mke wako muzungumze

Yule binti nikaona ametoka anaondoka jamaa nae akatoka anamuita yule binti aliekua amekaribia getini akampakia wakaondoka, yani sikuelewa sasa yule rafiki angu akawa Analia kwa uchungu mpaka unaona hii sio kawaida ameumia saaana nikamwambia twende tukupeleke nyumbani kama haukuja na usafiri akasema hataki tena kulala home anaitaji kuwa in a hotel apumzike mi nilipinga wazo lake nikasema nenda nyumbani piga simu ukweni eleza kilichotokea

Mke Wangu akajitahidi kumbembeleza sana akawa sasa at list namuona yuko kimya lakini Kwi Kwi haziish tukamsindikiza mpaka kwake tukamtia moyo hatukuingia ndani tukamuacha getini tukaondoka na Mke Wangu tunashangaa uku tumeguswa na kilichotokea

Sina mda mrefu nimeoa ila yesterday heart break ilikua touching sana nishauri tu guys tuwe makini tunapochagua wake tusiwatese watoto za watu hivi sio sawa kabisa sio sawa fikiria we we ndio umefanyiwa hivi na Mke wako wa ndoa pengine alafu yeye ndio chanzo cha tatizo lakini bado anakufanyia mambo ya ajabu. Ufike wakati tuheshimu wake zetu.
 

Chakorii

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
11,074
2,000
Dah!!!aiseeh kuna wanaume wana roho za kikatili jamni.badala ya kumtetea mke yeye anamtetea mchepuko!!kha!!nisamehe Mungu maana kwa ninavyojijua lazima ningemmwaga mwanaume damu japo kidogo.

Siezi shughulika na mchepuko hata robo maana kama si mwanaume huyo mchepuko asingepata jeur ya kumkoromea mke wa ndoa
 

UrbanGentleman

JF-Expert Member
Jun 19, 2016
2,590
2,000
Heeee
Kumbe Urban Gentlemen Umeooooaa? !
Du
Na kunisumbua kote kule mpaka nikaku block, kweli leo nimekamata mwizi!

Shame on u!
[HASHTAG]#PYTHONWAKIUMEAU?![/HASHTAG]
Maisha baada kabla ya kuoa its totally different ukioa nyumbani unarudi saa mbili ukichelewa unakuwa na sababu za kueleza why late

Ukiwa bachelor unajiamulia unakua dictator wa maisha yako

Nina like miezi tangu niwe mume and proud of it
 

Junior. Cux

JF-Expert Member
Feb 3, 2011
5,329
2,000
Dah!!!aiseeh kuna wanaume wana roho za kikatili jamni.badala ya kumtetea mke yeye anamtetea mchepuko!!kha!!nisamehe Mungu maana kwa ninavyojijua lazima ningemmwaga mwanaume damu japo kidogo.

Siezi shughulika na mchepuko hata robo maana kama si mwanaume huyo mchepuko asingepata jeur ya kumkoromea mke wa ndoa
Huyo mwanaume katisha... hata kama limbwata hiyo imepita kiwango!!!

Sio mambo ya kumfanyia mke hayo
 

shatisuruali

JF-Expert Member
Jul 28, 2016
615
1,000
Was it a coincidence kukutana pale na mme wake?? Inaonekana ni kiwanja ambacho jamaa anapenda kuwapeleka mabinti! na mkewe pia kapelekwa mara kadhaa. Sasa mke ameamua kwenda kujichana mwenyewe, mume nae kaja na mchepuko wake. Nhaaaa.:(

Nkajua mwisho wa stori classmate nae atachepuka na jamaa.
 

UrbanGentleman

JF-Expert Member
Jun 19, 2016
2,590
2,000
Was it a coincidence kukutana pale na mme wake?? Inaonekana ni kiwanja ambacho jamaa anapenda kuwapeleka mabinti! na mkewe pia kapelekwa mara kadhaa. Sasa mke ameamua kwenda kujichana mwenyewe, mume nae kaja na mchepuko wake. Nhaaaa.:(

Nkajua mwisho wa stori classmate nae atachepuka na jamaa.
Haha pole
 

platozoom

JF-Expert Member
Jan 24, 2012
8,807
2,000
Siku moja nipo pub moja maarufu along Sam Nujoma road. Akaingia jamaa na Wanawake wawili, mmoja mchepuko mwingine rafiki wa mchepuko. Baada ya bia mbili tatu (waliingia tayari wameshachangamka) mchepuko ukaanzakumponda
Mke wa jamaa! Baada ya dakika kama tatu jamaa akakasirika na kuondoka. Mchepuko ukawa unabembeleza lakini hakutaka
kumsikiliza. Hata bill aliwaachia!!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom