Ukiwa unataka kununua PC, lazima uwe specific unataka kuitumia kwa kazi ipi? kusema matumizi ya kawaida tu bado ni general sana, nina uhakika watu wengi huwa wanatumia neno kawaida kwenye kazi ambazo si za kawaida.
watu wengi hudhani kucheza game, kuedit video au kufanya simulations ndio kazi ngumu, Hapana ,watu wengi hawajui hatakuangalia muvi ni kazi ngumu kwa baadhi ya PC, nitoe mfano hapa, mtu ambaye anatumia computer yenye processor ya core 2 duo kutazama movie yenye quality ya 1080p au iliyokuwa encoded kwenye HEVC (H265) ni kazi ngumu sana.
Unapotaka computer ni vyema kusema specific programs unazotaka kurun na wingi wa data unazotaka kuzichakata.
Mfano processor za intel i3 haijarishi ni kizazi gani zimetengenezwa kwa matumizi ya nyumbani, biashara ndogo na zakati, lengo kuu la processor hizi ni kutunza nishati na kutotoa joto kali, kwa watu wenye ulewa wa processor jinsi zinavyofanyakazi wanajua kabisa kuwa kadri processor inavyotumia watt nyingi ndio inakuwa na nguvu, na hapa ndipo baadhi huwa tunaziover clock hizi Processor, kitu tunachokifanya ni kuongeza wattage limit kwenye processor ili iweze kuperform zaidi, kiufupi kwa i3 zimeundwa zitumie nishati ndogo ndio maana laptop nyingi ambazo ni low end huwa zinatumia i3.
Kama swala na nishati kwako si la umuhimu kuliko kutoa pesa nyingi iliupate latest generation ni bora urudi hata vizazi vinne( 4) nyuma unanue upper class yake.
mfano kama ikitokea natafuta PC ambayo sina uhakika nitaitumi kwenye nini, kuliko kununua PC yenye i3 1Oth generations let say Intel Core i3-10110U @ 2.10GHz nitanunua PC yenye intel i5 6th generation let say Intel Core i5-6600 @ 3.30GHz, hapa nitaenjoy Class benefits kwa kuwa i3 imeundwa inferior to i5 na kwa gap la vizazi vinne bado i5 itakuwa inamaintain status quo.
kwa maana 10th and 6th generation zote zinatumia Lithography moja ni 14nm haziwezi kupishana idadi ya transistors zilizotumika kuunda hizo processor.
ukitazama hii picha hapa chini utaona performance comparison
Sababu ingine nitakayo iconsider ni Heat resilience, i3 zote hazina uwezo wa kuwithstand prolonged heat, Ukienda kwa mafundi PC utakuta kuna PC wanakwambia zimekufa board, ukichunguza hizo PC utakuta 9 kati ya 10 ni i3, nimesha shuhudia zaidi ya mara 6 pc za i3 zikifa wakati wa windows installations, huwa zina freez na ukirestart ndio kwaheli, ukimpa fundi atakwambia "haipandishi kioo bodi imekufa"
Sasa kama haujui matumizi specific ya PC ni bora kustay safe.
Pia budget, ukienda kariakoo, utasikia mtu anakuuzia PC anakwambia hii 10th generation na bei itaanzia 1 point M, sababu za msingi ukimuuliza hana yeye anang'ang'ana 10th generation tu, hakikisha anakwambia specific CPU performance , lazima akwambie vitu kama L3 smart cache size na Bus speed kama upo interested na performance mfano hizo CPU za hapo juu i3 ya kizazi cha 10 ina L3 cache ya MB 4 na Bus speed ya 4 GTs wakati i5 kizazi cha 6 ina L3 smartcache ya MB 6 na bus speed 8 GTs (
clarification GTs= Gigatrabsfer per second)
Pia swala la muda wa matumizi, PC nyingi za i3 huwa recommended running time at full load ni ndogo sana, i3 nyingi huwa haziwezi kustastain more than 5 hours full load running bila ya kuwa na thermo solutions ita shutdown au itakufa kabisa, i5 zenyewe zina sustain muda mlefu sana kabla ya kuauto hibernate kama joto ni kali sana. sasa kama hata kama unadeal na spreadsheet za data chache kwa PC ya i3 itakuwa na muda mchache wa kuishi,
Kuna mtu amesema kuwa i3 unaweza kuchezea game kwa kuwa hizi sasa zina graphic cards zenye nguvu, kwanza kabisa intel huwa hawaweki graphics kwa lengo la kuchezea game, huwa zinawekwa kwaajiri ya kupower high resoulution display na media decoding ndio maana series zake huwa zinatumia majina yanayo endana na media quality kama utakuwa unafuatilia development zake utaona kipindi cha core 2 duo 1st gen kulikuwa na
Intel®
Graphics Media Accelerator series na kipindi cha intell i series 1st gen wakaja na intel HD graphics series na sasa wanatumia inte UHD graphics series, hizi zote si kwaajili ya games na sabubu kubwa nikuwa huwa zinatumia Open CL na si Open GL na pia hazina shaders kubwa kama dedicated, huwa zina dedicated memory ndogo sana mfano latest intel card huwa zina MB 168 na mara nyingi zina rely kwenye RAM kupata shared memory ambayo in games ni nothing.
Kuna mtu hapo juu ametaka kufananisha performance ya decated cards na na hizo integrated cards za intel, mzee hakuna muda ambapo intel graphics zime perform better than decated, dedicated cards ni kama jina lake lilivyo, zimeundwa kwa special task za kurender games na kusustain long running time.
Ukitazama hii picha utaona kuwa hakuna hata low end dedicated card ambayo intel UHD graphics imecache up with, graphics cards ambazo intel anatengeneza kwa lengo la kucheza games ni intel iris plus ambazo not for hardcore gaming.
Swala la kusema kuna card ya intel itakayo perfom better kama Nvidia 2080 ni ndoto za mchana, mimi natumia Nvidia GTX 1080Ti kwa sasa ni moja ya medium level graphics card lakini ni powerful mara 460 zaidi ya intel iris plus XE ambayo ndio latest card ya intel kwa sasa.
Mtu anapotaka ushauri kuhusu PC ya kununua tusimrecommend tu kununua latest generations, kwa sababu most services that come with this latest CPUs si kitu kwetu zaidi ya marketing words, kitu cha kuzingatia ni actual manufacturing advantages na performance interms of number, nitakushangaa kama utakimbilia efficiency instead of performance wakati hapo nyumbani unawasha fridge masaa 24 ili maziwa yako mtindi ya 2k yasiharibike.
Kama budget ni ndogo opt older generations and benefit performance ukinunua computer ya generation ya juu kisa wameweka Control Flow Enforcement Technology (CET), sijui intel optane H10 au kisa ina 10nm SuperFin technology utakuwa ni mjinga maana hizi feature hautabefit potential zake leo wala kesho, ni ucheshi sana kununua PC yenye processor ambayo ni Optane H10 enabled wakati kwenye PC yako bado unatumia HDD ya 72k RPM au SSD ya M.2 SATA ni sawa na kufunga injini ya v12 kwenye Raum.
Get the old thing to benefit performance.