LAPF na Clouds FM mbona mnadanganya umma?

LAPF na Clouds FM mbona mnadanganya umma?

chema chajiuza kibaya chajitembeza hii nguvu mnayotumia kuiponda LAPF mngeitumia kuboresha mifuko yenu iliyo katika hali ya kufa.. kuliko kujitekenya hapa na kucheka wenyewe... hebu uliza Tanzania ni mfuko upi unaongoza kwa mafao bora na kanuni bora ya kukotoa.... acheni majungu mmekula maharage ya wapi nyie pspf? na mkome!!! wiwiwiwiwiwiwi!
 
Nimefuatilia sana mjadala wenu nyie watu wa PSPF mmetumwa LAPF bado ni mfuko bora nyie wenye ripoti ya SSRA ambayo ina unqualified opinion ya deficit mnapinga nyama mnatoa mafao ya uzazi mkibanwa mnasema mnaanza kutoa 2016 toka 2010 mm naajiriwa kwenye ualimu mlikuwa mkidanganya akina Dada ss hv mmekuja na style mpya ya uongo kuwa mafao hayo mnaanza kuyatoa 2016 lakini kwenye media hamsemi kuna Dada yangu anakuja kuwafungulia kesi ya kusema uongo.....
 
Mbona kwenye website ya PSPF mnayojinasibu hakuna hayo mafao ya kujikimu wapuuzi nyie mkopo wa kujikimu mnauita fao? Acheni ukazwazwa nyie someni sheria za mifuko muelewe maana mfuko wenu ndo mabingwa wa uongo na mna kesi nyingi sana SSRA walimu walienda kuwashtaki wakaambiwa wanawasaidia mpate wanachama LAPF bado ni mfuko bora nitaendelea kuwashawishi watanzania wauchague maana ndo mfuko bora Tanzania hata Mh. Zitto akiwasilisha report ya PAC bunge la January alithibitisha hilo njooni na facts acheni upumbavu
 
Hapo umesema ukweli mkuu.
Nilifanya uchunguzi kupitia SSRA pdf documents (available online) nika gundua nilifanya kosa kubwa mno!

Na nimewahi kuwa tumia email SSRA kutaka kuhama mfuko ndio wakanipa ufafanuzi kuwa haiwezekani!

Wakibadili tu sheria , Kesho nahamia PSPF.
Mm najuta kujiunga PPF.

Mfuko bora kuliko zote ni PSPF basiiiii!

Mkuu, nikukumbushe kitu,PSPF ina Actuarial Deficit ya 7 trillion, yaani uwezo wao wa kulipa wanachama wao ni negative..!! Walichonacho kinaweza kulipa wanachama waliopo kwa miaka saba tu ijayo. Na hiyo ilikuwa ni 2010..so 2017 chali.

Wanakusanya Bilioni 400 wanalipa Bilioni 600. Unaweza kwenda huko usipate mafao yako. Oooh. Wameishiwa kabisa wale, wanapewa BLN 50 kila mwaka na serikali ili kuwasogeza sogeza na hiyo deficit. Mfuko umeoza kabisa ule.

Nenda NSSF ndio mpango mzima. Wanakusanya 600Bln wanalipa 200bln. Na actuarial report inasema wanaweza kulipa wanachama wao for next 50 years. Na ndio mfuko pekee wenye mafao lukuki ya muda mfupi ambayo utapata ukiwa kazini yasiyo na longo longo..alafu wapo ISO 9001:2008 Certified. Daah, nafasi ya kuwasifia haitoshi hapa.
 
Hawa LAPF mwaka jana walikuwa wanaadhimisha miaka 70 toka kuanzishwa kwake. ukiangalia ukongwe wake na position yao kisekta hawakupaswa kudanganya umma, maana miaka 70 si haba ni umri wa mtu anayesubiri siku zake za mwisho wa uhai wake :lol::lol::lol::lol:

kwahiyo wameanza kabla tanzania haijapata uhuru? Hii nayo skendo, wachunguzwe washenzi hawa walipata wapi kibali?
 
Kwa muda mrefu sasa katika kipindi cha Jahazi cha Clouds FM, Mfuko wa LAPF wanatoa tangazo linaloelezea kwamba wanatoa fao la kujikimu jambo ambalo sio kweli kabisa kwa maana wasimamizi wa Mifuko hawajatoa ruksa kwa LAPF kutoa fao hilo, huu ni uhuni wa hali ya juu kwa LAPF kudanganya umma na pia ni hatari kwa kituo makini kama Clouds FM chini ya Kamanda Ruge kutoa matangazo yanayopotosha kama hayo. Kama wameruhusiwa kutoa fao waoneshe barua kutoka kwa msimamizi wa Mifuko hiyo.

Pia kuna jamaa zangu huku Ipinda, huku Mbeya wamenieleza kuwa LAPF wamefulia kwa maana hivi sasa hawana tangazo katika TV yoyote ile, sasa hii maana yake wamejitoa katika ushindani au wameishiwa fedha. LAPF ni tatizo kubwa kwani wakiwa wananadi sera zao huwa wanatumia muda mwingi kuponda mifuko mingine, ushahidi ni hivi karibuni wakati wa usajili wa wafanyakazi wapya wa TRA, jamaa walipewa onyo na mdhibiti na mtumishi wao mmoja kafungiwa kujihusisha na masuala ya usajili.

na bado tu LAPF itawanyima usingizi naona nyie PSPF kila tangazo ni kwa hisani ya Postal Bank yani ndio inayotoa mkopo wa elimu, inatoa mkopo wa kujikimu ambao haujulikani ni shilingi ngapi, inaonyesha ni kwa kiasi gani mnazidi kudidimia acheni kuwarubuni watumishi wa ajira mpya sustainability yenu inamiaka mitano mbele tu.Leo mnajilinganisha na LAPF yenye sustainability ya zaid ya karne nzima(miaka 100). Wastaafu huu ni mwezi wa kumi hawajapewa pesheni zao ooh jamani ni BORA UPANGWE KITUO KIBAYA CHA KAZI KULIKO KUJIUNGA NA PSPF..
 
LAPF Staafu kwa Ufahari. best awarded kwa miaka mitano mfurulizo kwa utunzaji bora wa pesa za wanachama wake, mfuko unaokupa mafao yako jana na ww unastaafu leo... na mwaka huu ajira mpya za waalimu LAPF itazidi kuwashangaza nyie mifuko mingine sabab kizur chajiuza tu nyie kahongeni tu kama kawaida yenu ili mpate mteremko na support kutoka kwa ma HR, LAPF itazid kumwaga seraaaaa kama kawaida na kama hutajiunga ww basi tunajua mbeleni utamshauri mwanao au ndugu yako ajiunge na Mfuko wa LAPF sababu utakoma kujiunga pengine
 
Mkuu, nikukumbushe kitu,PSPF ina Actuarial Deficit ya 7 trillion, yaani uwezo wao wa kulipa wanachama wao ni negative..!! Walichonacho kinaweza kulipa wanachama waliopo kwa miaka saba tu ijayo. Na hiyo ilikuwa ni 2010..so 2017 chali.

Wanakusanya Bilioni 400 wanalipa Bilioni 600. Unaweza kwenda huko usipate mafao yako. Oooh. Wameishiwa kabisa wale, wanapewa BLN 50 kila mwaka na serikali ili kuwasogeza sogeza na hiyo deficit. Mfuko umeoza kabisa ule.

Nenda NSSF ndio mpango mzima. Wanakusanya 600Bln wanalipa 200bln. Na actuarial report inasema wanaweza kulipa wanachama wao for next 50 years. Na ndio mfuko pekee wenye mafao lukuki ya muda mfupi ambayo utapata ukiwa kazini yasiyo na longo longo..alafu wapo ISO 9001:2008 Certified. Daah, nafasi ya kuwasifia haitoshi hapa.

Daah! Yamekuwa haya tena?

Ila kwa ulipaji wa Final retirement benefit wao ndio bora licha ya changamoto hizo.

Tatizo la NSSF& PPF ni moja. Wanapenda sana kuwekeza hela za members wao ktk miradi mikubwa kama Madaraja, Vivuko, Reli, Bandari, Majumba, nk lakini gawio lina bakia ktk capital tu, members kiduchu!

Pia wanatoa meaningless benefits Kwa mwanachama. Mfano Fao la kifo ( mazishi) huu ni ujin.ga hadi ufe?
Fao la kujitoa. SSRA kwa sasa hawaruhusu haya madudu!

Pitia SSRA website kuna pdf ina comparable benefits. Mafao ya PPF+ NSSF kwa mtu mmoja = na ya mtu mmoja wa PSPF
 
Hiyo Final Retirement Benefit hawaringi nayo tena kwa wanachama wapya coz mwaka jana SSRA ilitoa formula ambayo ilileta harmonization. So, for retirement benefit mifuko yote ni sawa. Hii propaganda kwisha habari yake.

Umeongelea kuinvest kwenye majengo etc...can you put PSPF aside on this??. Come on brother. By the way, kuinvest ni moja ya kazi tulizowapa ili hela zetu zizalishe sawa sawa.

Kuhusu meaningless benefits hata sikuelewi..labda ukasome upya ILO convention. Hilo la Funeral Grant limewekwa kati ya yale tisa, na lina maana yake. Nafikiri ni njia nzuri ya kusaidia familia ya mfiwa apart from Survivors Benefits..

By the way, mke wangu mwka jana amekula 4.5 Million kutoka NSSF baada ya kujifungua kupitia fao la Maternity...yaani alipata 3 times ya mshahara wake, na hii hela haijapunguza balance yake.. akijifungua tena atavuta mkwanja mara tatu ya mshahara wake. Humwambii kitu kuhusu NSSF.

Above all tuna jirani yetu hapa anafanya kazi kwenye kampuni ndogo tu ya usafi kwenye maofisi mjini huko, michango yake inaenda NSSF, and because of that anatibiwa yeye na familia yake yenye watoto wanne kupitia fao la SHIB.

Unataka nini zaidi ya hayo mafao safi kabisa ya muda mfupi?. Upo kazini lakini bado unaendelea kunufaika.

Kuhusu Fao la kujitoa, halipo kwenye ILO na hata Sheria ya NSSF/PPF, ni siasa za bongo tu. Hawa watu wanojitoa watakuja kuidai serikali baadaye (kama wanaakili hizo). Mimi sijitoi ng'ooo mpaka nizeeke nile pensheni ng'wanawane.

NSSF Mpango mzima ndugu yangu. Imekamilika kila eneo.
 
Mkuu, nikukumbushe kitu,PSPF ina Actuarial Deficit ya 7 trillion, yaani uwezo wao wa kulipa wanachama wao ni negative..!! Walichonacho kinaweza kulipa wanachama waliopo kwa miaka saba tu ijayo. Na hiyo ilikuwa ni 2010..so 2017 chali.

Wanakusanya Bilioni 400 wanalipa Bilioni 600. Unaweza kwenda huko usipate mafao yako. Oooh. Wameishiwa kabisa wale, wanapewa BLN 50 kila mwaka na serikali ili kuwasogeza sogeza na hiyo deficit. Mfuko umeoza kabisa ule.

Nenda NSSF ndio mpango mzima. Wanakusanya 600Bln wanalipa 200bln. Na actuarial report inasema wanaweza kulipa wanachama wao for next 50 years. Na ndio mfuko pekee wenye mafao lukuki ya muda mfupi ambayo utapata ukiwa kazini yasiyo na longo longo..alafu wapo ISO 9001:2008 Certified. Daah, nafasi ya kuwasifia haitoshi hapa.

Ongea yote ila hakuna mfuko Bomu kama NSSF. Huo uwezo wa kulipa ni kwa vile tu watu wengi walijiunga na mfuko huu kipindi kile ilikua ni ukiritimba lazima private sector wawe huku, otherwise nao wangekua na deficit tu.

Ukidai hela yako kama ni nyingi lazima wakusingizie sababu lukuki ili kukuzungusha. Kuna watu wamekaa ki roho mbaya roho mbaya tu ofisini, hawaoni tabu kukupiga kalenda ya wiki nzima kwa kitu kidogo tu!
 
Mkuu, nikukumbushe kitu,PSPF ina Actuarial Deficit ya 7 trillion, yaani uwezo wao wa kulipa wanachama wao ni negative..!! Walichonacho kinaweza kulipa wanachama waliopo kwa miaka saba tu ijayo. Na hiyo ilikuwa ni 2010..so 2017 chali.

Wanakusanya Bilioni 400 wanalipa Bilioni 600. Unaweza kwenda huko usipate mafao yako. Oooh. Wameishiwa kabisa wale, wanapewa BLN 50 kila mwaka na serikali ili kuwasogeza sogeza na hiyo deficit. Mfuko umeoza kabisa ule.

Nenda NSSF ndio mpango mzima. Wanakusanya 600Bln wanalipa 200bln. Na actuarial report inasema wanaweza kulipa wanachama wao for next 50 years. Na ndio mfuko pekee wenye mafao lukuki ya muda mfupi ambayo utapata ukiwa kazini yasiyo na longo longo..alafu wapo ISO 9001:2008 Certified. Daah, nafasi ya kuwasifia haitoshi hapa.

Nakuunga mkono kwa 100%. NSSF ndo mchumba wangu ninayetarajia kuja kufunga ndoa naye
 
LAPF ndio mfuko bora msidanganyike na daladala zinazokatisha ruti ukajuta kutoa nauli yako..na kwa walimu watakao pangiwa mbeya pm hapa nikujuze zaidi
 
mkuu inaonekana una chuki binafsi na LAPF. mbona hutaji huko ulipo ili na sisi tujue ubovu wake? (uliposema, ningekuwa na uwezo nongejitoa huku nilipo nijiunge PSPF). mm nipo LAPF na cjaona mtu aliyecomment matatizo yake hapa kunishawishi kuwa niko mfuko mbaya, zaidi naona mnaponda tu
 
team LAPF tupoooooo! waache kuponda bila kuleta facts. alafu hawa ni watu wa PSPF wanaponda tu humu. hatudanganyiki na wala hatuchepukiiii. LAPF inawakimbiza hadi ndimi zinawatoka.
 
Mnachekesha kweli unaongea kuhusu LAPF we kweli chizi

Fao la uzazi
Fao la elimu

Haya nimeyaonja mimi tena kwa uharaka sana hao pspf siwajui kwanza hwasomeshi wameenda jamaa zangu pale wakaambiwa unatakiwa uwe umechangia miezi 12 kwa ajili ya elimu yaani apart na makato yale yao ya kawaida kwa maana nyingine ukiwa na mpango wa kusoma uwaambie mapema 12month before ili waanze kukukata ili ukija ndio wakupe,,

Lapf nimewafata Friday wakanipa form nikaipeleka kwa afisa utumishi na barua kuruhusiwa kusoma jtano nkawapa next Monday wakalipa ada chuoni

Sweety alijifungua nkajaza form yake nkawapelekea akalamba 1.3 million ya martenity tena wala hakatwi its free

Kati ya mifuko bora LaPf wako vizuri

Kajipange jombaaaaaa
 
chema chajiuza kibaya chajitembeza hii nguvu mnayotumia kuiponda LAPF mngeitumia kuboresha mifuko yenu iliyo katika hali ya kufa.. kuliko kujitekenya hapa na kucheka wenyewe... hebu uliza Tanzania ni mfuko upi unaongoza kwa mafao bora na kanuni bora ya kukotoa.... acheni majungu mmekula maharage ya wapi nyie pspf? na mkome!!! wiwiwiwiwiwiwi!

LAPF ni janga la kitaifa. hakuna mfuko wa kipuuzi na wa kipumbavu kama huu.
 
Inaonekana huyu jamaa aliyeanzisha uzi huu anajua mambo ya katika hii Mifuko, sasa Ruge na team nzima ya Clouds, The Peoples station, kuweni makini na ikibidi hao jamaa wa Mifuko wawe wanawaonesha barua kutoka kwa msimamizi wao, au msimamizi ajitokeza na aseme ukweli juu ya LAPF na pia GEPF nao wanafanya kosa kama hilo la kutangaza vitu ambavyo hawajapatiwa ruksa na msimamizi wao. Clouds ni redio makini na wengi tunaikubali hivyo tusaidieni kwa kurusha matangazo ya ukweli.

Mtoto wangu alikwenda Makao Makuu ya LAPF baada ya kusajiunga nao na alipoulizia mkopo wa kujikimu maafisa wa LAPF hawakumpatia jawabu la maana na waliishia kusema na wao wanasikia tangazo redioni na hawajui kwanini wakubwa wao wanatoa tangazo hilo.

Ruge asipokuwa makini ataharibu credibility ya redio yake. kwanini anaruhusu tangazo la kitapeli kama hilo? anajishushia heshima yake kwa kiwango kikubwa sana.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom