Dr.Mbura
Senior Member
- Jun 30, 2009
- 196
- 128
Kwa muda mrefu sasa katika kipindi cha Jahazi cha Clouds FM, Mfuko wa LAPF wanatoa tangazo linaloelezea kwamba wanatoa fao la kujikimu jambo ambalo sio kweli kabisa kwa maana wasimamizi wa Mifuko hawajatoa ruksa kwa LAPF kutoa fao hilo, huu ni uhuni wa hali ya juu kwa LAPF kudanganya umma na pia ni hatari kwa kituo makini kama Clouds FM chini ya Kamanda Ruge kutoa matangazo yanayopotosha kama hayo. Kama wameruhusiwa kutoa fao waoneshe barua kutoka kwa msimamizi wa Mifuko hiyo.
Pia kuna jamaa zangu huku Ipinda, huku Mbeya wamenieleza kuwa LAPF wamefulia kwa maana hivi sasa hawana tangazo katika TV yoyote ile, sasa hii maana yake wamejitoa katika ushindani au wameishiwa fedha. LAPF ni tatizo kubwa kwani wakiwa wananadi sera zao huwa wanatumia muda mwingi kuponda mifuko mingine, ushahidi ni hivi karibuni wakati wa usajili wa wafanyakazi wapya wa TRA, jamaa walipewa onyo na mdhibiti na mtumishi wao mmoja kafungiwa kujihusisha na masuala ya usajili.