Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 15,544
- 19,404
Wakati Nyerere akiwa hai alikuwa hapendi jina lake kutumika katika landmarks mbalimbali. Uwanja wa Nelson Mandela kule Sumbawanga ulikuwa umejengwa kama uwanja wa Nyerere lakini alipokwenda kuufungua akaubadilisha jina na kuuita Nelson Mandela. Siku za hivi karibuni kumekuwa na landmarks nyingi sana zilizopewa majina ya Nyerere lakini naona kama kuna viongozi wanaosahauliwa kabisa.
Karume (Muasisi wa Zanzibar ya leo) zaidi ya kuwa na ule uwanja wa Karume ambao zamani ulikuwa uwanja wa Ilala, na mitaa midogomidogo na shule za msingi huko mikoani, sidhani kama kuna landamark kubwa ya kumuenzi. Kwa vile huyu alikuwa baharia, ningeshauri mojawapo ya bandari zetu iitwe Bandari ya Karume
Aboud Jumbe (huyu alikuwa makamu wa rais effective sana ila alikosea kidogo tu) hana landamark yoyote ya kumkumbuka. kwa vile yeye alitumia sehemu kubwa sana ya maisha yake Kigamboni, ningeshauri lile jimbo la kigamboni liitwe Kwa Jumbe
Mwinyi (Rais wa ruksa) amewekwa kwenye barabara ile iliyokuwa ikiitwa Bagamoyo road, na labda uwanja wa mpira wa mkoa wa Tabora tu. Hizo landmarks siyo kubwa sana kwa hadhi yake, na hivyo ningeshauri aongezewe kwenye list. Kwa vile yeye alihimiza sana biashara kwa kutumia falsafa ya Ruksa, ningeshauri jengo la wizara inayohusika na biashara hapo Dodoma liitwe Mwinyi House.
Angalu jina la Mkapa liko kwenye landamark kubwa mbili- daraja kubwa sana la Rufiji na stadium kubwa sana Tanzania; hakuna ulazima wa kuongeza landmark nyingine kwa jina la Mkapa.
Kikwete anaenziwa labda na taasisi ya Moyo ya Kikwete hapo Muhimbili, lakini nadhani anastahili kueziwa zaidi hasa katika jithada zake za kusambaza elimu nchini chini ya sera za sekondari za kata na UDOM. Ningeshauri kile chuo Kikuu cha Dodoma alichokiasisi yeye kiitwe Kikwete University of Dodoma (KUDOM).
Halafu tuwe na sheria inayoweka limit ya kutumia jina moja kwenye major landmarks; yaani jina moja lisitumike katika landmarks kubwa zaidi ya tatu au nne hivi. Mitaa midogo midogo pamoja majina ya vitongoji na shule za msingi siyo landmarks kubwa; hivyo havitaguswa na sheria hiyo.
Mengine yataongezewa kadri muda na matukio yanavyoruhusu