lakini binti alia, aachwe tu wabanane.............

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
216,365
2,000
Hivi sijui tatizo liko wapi kwa huyu kinda hata aachwe?
Hivi ni uhaba kweli wa madume au papara zake tu?
Hivi kiu yake ni mlo au na uvivu umetuwama pia kwake?
Huyu binti ni kinda kiukweli-ukweli siyo masihara hataaa?
Miaka yake ni 15-17 na hata kubalehe safari bado mbichi!
Lakini binti alia, aachwe tu wabanane................


Binti adai kubanana ndizo sera za kileo...........
Binti adai kaumwa naye ameng'ata.....
Binti adai yeye sasa ni kibogoyo...........
Binti adai meno yake yamebaki kwa Mr. RIGHT......
Binti adai na huu ukibogoyo atakuwa mgeni wa nani?
Lakini binti alia, aachwe tu wabanane................

Kinda atusihi tuache kumnyanyapaa kwani yeye ni mtendewa tu!
Kinda atusihi tuache ushambenga kwani maumivu siyo yetu!
Kinda atusihi tuache kumbughudhi kete zake hazina dosari!
Kinda atusihi tuache kumzongazonga kama kuumizwa ni yeye!
Kinda atusihi tuache kumsengenya utamu wa kitanda yeye aujua!
Lakini binti alia, aachwe tu wabanane................

Kama wakiafikiana, njemba amevua jiko la kenda.......
Kama wakiafikiana, binti shule sasa tosha..............
Kama wakiafikiana, wazazi wa kinda kuvuna mahari...........
Kama wakiafikiana, kinda kuvikwa taji la uana-mtandao..........
Kama wakiafikiana, kinda kajipanga na karaha za uke wenza...........
Lakini binti alia, aachwe tu wabanane................

Mara atakapotimuliwa, kiguu kwa njia kurudi kwetu!
Mara penzi litakapoota mbawa, karaha zake kutuvisha!
Mara atakapobabuliwa, gharama za tiba kutusukumia!
Mara mambo yatakapokwenda kombo, sisi ni dugu moja!
Mara atakapoelemewa, atakuja juu akidai ana kwao!
Lakini binti alia, aachwe tu wabanane...................
 

Ndallo

JF-Expert Member
Oct 1, 2010
7,623
2,000
Ruta niko busy na shopping za Xmass! Lakini kwataarifa yako mabinti wa sasa hivi wanaBalehe wakiwa na mika 9-10! Merry Xmass and happy 2013!

Miaka yake ni 15-17 na hata kubalehe safari bado mbichi!
 

Mr Rocky

JF-Expert Member
Oct 10, 2007
15,188
2,000
Mr Rocky................................mbona hatuwasiliani, siku hizi.......................kakamatwa lakini naye adai kakamata pema......

Mkuu Rutashubanyuma nipo sana mkuu
Wewe ndo ulisahau tulikotoka
Ukatupa mti na na kila kitu chake
Ukasahau maana ta urafiki
Ukadhani mapito yatakuwepo
Ila mapito yamepotea
bado urafiki upo pale pale
 
Last edited by a moderator:

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
216,365
2,000
Ruta niko busy na shopping za Xmass! Lakini kwataarifa yako mabinti wa sasa hivi wanaBalehe wakiwa na mika 9-10! Merry Xmass and happy 2013!

Miaka yake ni 15-17 na hata kubalehe safari bado mbichi!

Ndallo.....................hao makinda.............ni matunda ya steroids, kuku wa kileo na spices ambazo ni " no name products."...................
 
Last edited by a moderator:

Ndallo

JF-Expert Member
Oct 1, 2010
7,623
2,000
Wapi Ruta! Kutokana na maisha yalivyo magumu mlo wenyewe mmoja kwasiku au hata watu siku nyingine wanatingishia kwa usawa huu wa Baba Mwanaisha hata hiyo inachangia kuharibu mzunguko wa maisha ya binaadamu!

hao makinda.............ni matunda ya steroids, kuku wa kileo na spices ambazo ni " no name products."...................
 

Elli

Platinum Member
Mar 17, 2008
46,051
2,000
Kwa kweli hii tamu sana natamani ningelisoma kipindi kile niko pale shule nafundisha Fasihi, lingenifaa sana, maana vile vitoto vilikua as if vimetia pilpili.....yaaani ni kungonoka kwa kwenda mbele
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom