Lahaja gani rasmi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lahaja gani rasmi

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by TWANJUGUNA, Jun 11, 2010.

 1. T

  TWANJUGUNA Member

  #1
  Jun 11, 2010
  Joined: Jun 6, 2010
  Messages: 27
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Huku wanasiasa wakitusukumilia jumuiya ya afrika mashariki ni lahaja ipi yastahili kutumiwa rasmi. kuna kiswahili cha mwambao - cha dar na mombasa; kunacho cha mijini - km nairobi kuna sheng; kunacho cha bara - ambacho kina maneno ya ki-bantu chungu nzima; kisha kunacho cha 'mbali' - kilichoingiliana na ki-ganda, ki-nyarwanda na ki-lingala.
  Nakumbuka katika miaka ya sabini kulikuwa na mradi wa kuki-standardize kiswahili katika university of dar es salaam.
  Sijui juhudi hiyo iliafikia yapi.
  Napendekeza kuwepo jopo-kazi katika jumuiya ya kukiangaza kiswahili. na kuwa jf iwe mstari wa mbele.
   
 2. d

  damn JF-Expert Member

  #2
  Jun 11, 2010
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 585
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  The best ni cha bara, ndicho kinafurahiwa na wengi ktk east africa. cha unguja utata mtupu. fikiria mkokoteni unaitwa lori na lori utaliitaje, water tape (bombani kwenye maji) kunaitwa mferejini.......
   
 3. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #3
  Jun 12, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Kiswahili kimepatikana kwa namna au lahaja mbalimbali. Wakati wa ukoloni wa Uingereza azimio lilitolewa kutumia Kiswahili cha Unguja kuwa Kiswahili rasmi katika Tanganyika, Kenya na Zanzibar. Waingereza walikitumia pia kama lugha ya polisi na jeshi katika Uganda.

  Kati ya lahaja za Kiswahili ni zifuatazo:

  * Kiunguja: kisiwani Unguja (Tanzania) - kimekuwa msingi wa Kiswahili cha Kisasa.

  * Kimrima: eneo la Pangani, Vanga, Dar es Salaam, Rufiji na Mafia kisiwani (Tanzania)

  * Kimgao: eneo la Kilwa (Tanzania)

  * Kipemba: kisiwani Pemba (Tanzania)

  * Kimvita: eneo la "Mvita" au Mombasa (Kenya). Zamani ilikuwa lahaja kubwa ya pili pamoja na Kiunguja.

  * Kiamu: eneo la Lamu (Kenya)

  * Kingwana: Kiswahili cha Kongo

  * Shikomor: Kiswahili cha Komoro

  * Shimaore: Shikomor cha Mayotte (Mahore)

  * Shindzuani: Shikomor cha Anjouan (Komoro)

  * Shingadzija: Shikomor cha Komoro Kuu

  * Kimwani: Kaskazini ya Msumbiji na visiwa vya Kerimba

  * Chimwiini: eneo la Barawa, kusini ya Somalia

  * Sheng: Kiswahili cha mtaani Nairobi (Kenya) chenye maneno mengi ya asili ya Kiingereza, Gikuyu na lugha zingine za
   
 4. T

  TWANJUGUNA Member

  #4
  Jun 12, 2010
  Joined: Jun 6, 2010
  Messages: 27
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Ufafanuzi wako bwana, jinsi ulivyo-classify zile lahaja, lakini naona hasa pale unapoanza....SHIKOMOR kama kwamba ni academic. Sina habari kunayo lahaja ya kiswahili kusini ya msumbiji - na ikiwepo, ni kiasi gani cha msamiati na sarufi ya kiswahili, na pia asili yake.
  Bila shaka kila lugha ya ki-bantu ina angalau maneno kadha yenye asili yake kiswahili. lakini si nguzo tosha kuiita kuwa lahaja - ni lugha kamili.
   
 5. Kipala

  Kipala JF-Expert Member

  #5
  Jun 12, 2010
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 3,537
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145
  Shikomor inahesabiwa na wataalamu kati ya lahaja za Kiswahili. Mahali pake si kusini ya Msumbaji bali upande wa mashariki wa Mtwara (kidogo kusini yaani sawa na kaskazini kabisa ya Msumbiji).

  Mifano kadhaa ya maneno yake:

  Kiswahili - Shikomori
  nchi - ntsi
  mbingu - wingu
  maji - maji
  moto - moro mro
  mwanaume - muntru baba mwanamume
  mwanamke - muntru mama mwanamushe
  kula - hula
  kunywa - hunwa
  kubwa - huu mhu'you
  dogo - -titi m'titi
  usiku - uku massihu
  mchana - mtsana
  Kifaransa - shizungu
  mtoto - mwana
  kazi - hazi
  asubuhi - a subuhi
  jioni - djioni
  nyama - niama


  Maneno mengi unaweza kutazama hapa: SHINGAZIDJA
   
 6. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #6
  Jun 12, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,200
  Trophy Points: 280
  Kiswahili kilizaliwa Unguja, kikakulia mwambao wa bara, kikapata utu uzima Kenya, kuzeekea Uganda na kufa Congo.

  Kiswahili hasa, kwa kufuatia chimbuko lake na wataalam walivyotafiti katika kuandika kazi za misamiati na kamusi za kwanza kabisa, ni cha Unguja.
   
 7. Kipala

  Kipala JF-Expert Member

  #7
  Jun 12, 2010
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 3,537
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145
  Kweli? Ukiwa na ushahidi naomba utuonyeshe.
  Maana yote niliyoona mimi hadi sasa ni Kiswahili kilianza mahali mbalimbali pa pwani kama kundi la lahaja zilizoendelea kuathiriana - na kikasanifishwa na Waingereza wakati wa ukoloni waliochagua Kiunguja kama msingi wa Kiswahili sanifu (kuna Wamvita - wa Mombasa- wanaoendelea kulialia juu ya hatua hii hadi leo).
   
 8. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #8
  Jun 15, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Kiswahili cha kibarawa.

  Jia lako nani = Inayo naáni?

  Naitwa Omari = Inaya ni Omari

  Jina langu linaandikwa hivi = Inaya handikowa jisiyi.

  Mimi natoka (Barawa) Mini = Mi ni munthu wa Mini.

  Sisi ni watu wa Mini = Si ni wamthu wa Mini.

  Anatoka Mini = ile ka Mini.

  Wanatoka Barawa (Mini) = Wa ile ka Mini.

  Mimi ni mtu wa Mini = Mi ni munthu wa Mini.

  Sisi ni watu wa Mini = Si ni wanthu wa Mini.

  Mimi ni mfanyabiashara = Mi ni menye biyanshara.

  Mini ni karani = Mi ni karani.

  Mimi ni mtalii = Mi ni turista.

  Mimi ni mgeni = Mi ni marti.

  Mimi ni Muguzi = Mi ni farmariyeri.

  Mimi ni Daktari = Mi ni dakhtari.

  Mimi ni rafiki wa Omari = Mi ni menza wa Omari

  Nimekuja hapa kusoma = Mi nile apa khsoma.

  Nimekuja hapa kusomesha = Mi nile apa khsomesha.

  Nimekuja hapa kufanyakazi = Mi nile apa khfanya kazi.
   
 9. T

  TWANJUGUNA Member

  #9
  Jun 16, 2010
  Joined: Jun 6, 2010
  Messages: 27
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Jamani, tutambue kiswahili sawa na lugha zingine zi na ufupisho. hata katika braille zaitwa contractions. kote uswahilini neno mimi hufupishwa kuwa mi, neno nini - kwa mfano, pilipili usoila yakuwashiani? - hutamkwa 'ni'. majungu pia humezameza baadhi ya silabi. isn't it?
  Tofauti za matamshi kutokana na asili ya kiswahili uarabuni - habari, khabari; asante, akhsante; tarehe, tariki, tarikhi....nk.
  Ufupisho na maendelezo tofauti si nguzo wala singizio kutafutilia eti lahaja!
  Kiswahili tayari chaogopewa na wengi - vipi mwaongeza kero?
   
 10. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #10
  Jun 16, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,200
  Trophy Points: 280
  Karibu nusu ya maneno ya Kiswahili ni derivative za maneno ya kiarabu.Ukielewa hili na kuelewa jinsi gani Unguja ilivyokuwa gateway na centre ya waarabu East Africa wala hutashangaa Kiswahili kuwa kimeanzia Unguja.
   
 11. Kipala

  Kipala JF-Expert Member

  #11
  Jun 16, 2010
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 3,537
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145
  Mkuu nimeshawahi kuuliza kama una ushahidi ya Unguja uwa chanzo cha Kiswahili. Kutokana na yote ninayojua haikuwa vile. Maana haiwezekani kusema hapa au pale yaani Sawahil = pwani za Afrika Mashariki zote zilikuwa mlango wa kukutana. Naona - kwa kutazama ramani - Lamu zaidi kuliko Unguja maana hapa Waarabu wengi kutoka kaskazini watapita kwanza - pia hapa walipata yale waliyotafuta tangu kale maana miti ya mikoko kwa ujenzi.

  Lakini kwa jumla hao jamaa walielekea kusini tu na kuona wapi biashara nzuri. Shauri ya mwendo wa upepo kwenye Bahari Hindi walipaswa kusibiri hadi upepo unageuka na kuelekea kaskazini tena - mahali pa kusubiri paliendelea kuwa miji ya kwanza ambako hawa wageni na wenyeji walikaa pamoja kwa muda na kupeana athira pamoja na kukuza lugha.
   
 12. T

  TWANJUGUNA Member

  #12
  Jun 16, 2010
  Joined: Jun 6, 2010
  Messages: 27
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Basi kulingana na logic yako ni sawa kusema kuwa kule waarabu walipokaa wakisubiri upepo ndiko walipata wanawake wa kibantu na vile vitoto vikaiga lugha kwanza za kibantu kisha upepo ulipowapepepusha mwambao na kukikuza kiswahili. itakuwa unreasonable kutarajia kiswahili kiwe sawia kote afrika mashariki. kiamu na kiunguja kina maneno ya kiarabu kiingi ilhali kile cha maeneo ya wa-midzi kenda (kenya), na wa pare kwa mfano kinacho ubantu mwingi. kumbuka pia kipare na ki-midzi kenda vina tofauti. kwa hivyo the only common denominator ni yale maneno ya ki-arabu. kila mmoja atadai kuwa lahaja yake ndiyo!
   
 13. Kipala

  Kipala JF-Expert Member

  #13
  Jun 16, 2010
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 3,537
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145

  Nadhani tuko pamoja. Unasema kweli kuna tofautitofauti kati ya lahaja za Kiswahili maana tumeshaona katika mifano hapo juu.

  Nakubali kabisa ya kwamba kile cha kuunganisha kilikuwa athira ya Kiarabu - pamoja na hali ya kuwa Waafrika kote pwani walikuwa Wabantu wenye lugha za karibu (lakini sijui mifano ya kile Kiswahili cha Somalia kilichokuwepo zamani huko kaskazini, nasikia tu habari zake).

  Mijikenda nasikia Kiswahli chao si sawa na Mvita yaani Mombasa kisiwani lakini sijui kwa undani.

  Kwa historia nadhani ni kweli ya kwamba Lamu palikuwa na Waarabu wengi maana pia historia ya Lamu iliandikwa kwa Kiarabu miaka 600 iliyopita. Sijui Ungnuja ilikuwa na Waarabu wengi nadhani labda hii imeanza tu karne ya 19 wakati watawala wa Omani walihamia Zanzibar.
   
 14. T

  TWANJUGUNA Member

  #14
  Jun 16, 2010
  Joined: Jun 6, 2010
  Messages: 27
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Basi yaelekea kila lahaja ina dai halali kuwa yao ndiyo....ndicho kiswahili halisi- wanachuoni watuamulie. kwanza waeke nguzo tutakazo fuata.
  Kiswahili ni nini? lugha halisi ni nini? nini uhusiano wa lugha bayana tamaduni? je, idadi ya waneni ni hoja? kazi kwetu wanaJF.
   
Loading...