Ladies: Your are very trick when hunting for Men

Ladies: Your are very trick when hunting for Men

Duh! kweli kwenye miti hakuna wajenzi, hizi bahati zinakosea njia aisee, we ni mlokole?
 
Asante mkuu kwa mawazo mazuri, sikuwa nimelifikilia hilo, sasa ngoma ni pale atakapogoma

Mbona hujiamini kaka, iweje mwanamke akuyumbishe hivyo...mpe majibu ambayo hayajengi udadisi au ushawishi.
Kama vipi mwambie aje ofisini akiwa kaivaa hiyo chupi tu asivae surual wala sketi chini afanye kama vile wanawake wakiwa beach.
 
Mithali 6
23 Maana maagizo hayo ni taa, na sheria hiyo ni nuru, Na maonyo ya kumwadilisha mtu ni njia ya uzima.
24 Yakulinde na mwanamke mwovu, asikupate, Na kukuponya na ubembelezi wa mgeni.
25 Usiutamani uzuri wake moyoni mwako; Wala usikubali akunase kwa kope za macho yake.
26 Maana kwa malaya mtu hutiwa katika hali ya kuhitaji kipande cha mkate; Na kahaba humwinda mtu anase nafsi yake iliyo ya thamani
27 Je! Mtu aweza kuua moto kifuani pake, Na nguo zake zisiteketezwe?
28 Je! Mtu aweza kukanyaga makaa ya moto, Na nyayo zake zisiungue?

29 Ndivyo alivyo aingiaye kwa mke wa jirani yake; Kila mtu amgusaye huyo atakuwa na hatia.
30 Watu hawamdharau mwivi, Akiiba ili kujishibisha, iwapo aona njaa;
31 Lakini akipatikana, atalipa mara saba; Atatoa mali yote ya nyumba yake.
32 Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa; Afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake.
33 Atapata jeraha na kuvunjiwa heshima; Wala fedheha yake haitafutika.
 
Aisee hii imenitoa kijasho chembamba, na sikuitegemea,

Ofcn kwetu kuna dada kaumbika kwelikweli na mke wa mtu ( wanaishi ila hawajafunga ndoa), tumezoeana kwa wingi wa utani na huwa ananiita mzee wa viwango kwasababu anajua mademu ninao wazimia (ila siwachukui, nawasifia tu, maana mm nimeoa) huwa anawakubali sana. Anapenda kunishauri sana kuhusu maisha na mambo mengine na mimi pia namshauri.
Kuna siku nilimuudhi my wife, siku hiyo nikawa na mawazo sana maana niliona nimemkosea mke wangu.

Yule dada akaja kunijulia khali maana aliniona nimepoa sana. Nikamwambia nimemkosea mke wangu na hapa nawaza nimpelekee zawadi gani ili aweze kunisamehe. Akaniambia hiyo ni rahisi sana. Tulipotoka kazini jioni akanipeleka maduka Fulani ambayo yanauza zawadi za kila aina. Nilinunua zawadi za wife, wakati tunataka kuondoka hapo dukani akaona CHU..P. akaniambia anazipenda sana ila hana ela ya kutosha. Kidume nikazama kwa wallet, nikachomoa noti nikazilipia. Tumerudi ameshika njia ya kwao na mimi nikasepa kwetu.

Msala wangu na wife ukaisha vizuri tu. After two days akaja kunishukuru kwamba zile Pichu zinamuenea vizuri na zinampendeza. Mimi nikamshukuru pia kwa kunichagulia zawadi nzuri za wife wangu, then nikampotezea.
Sasa leo yamenikuta, katika kutaniana kama kawaida, kaibuka na usemi ambao ameutaja ila nimeshtuka na yeye kashtuka ila naona anaendelea kurudia kila tukianza maongezi. Anasema hivi “ Best zile pichu zilinipendeza sana, sasa utaziona lini ili ushuhudie mwenyewe nikiwa nimevaa????”, Leo pia kanifunulia kitop kidogo ili nione, ila nikamzuia kwa kuwa tuko ofcn.

Je huyu dada si ananiweka katika majaribu???????, Mnaonaje, au anataka kunionyesha tu, na hakuna linguine zaidi???????

nipe mm kama ww umeshindwa
 
safari hii cjui utampa mkeo kitu gani ili akusamehe, unaelekea kufanya kosa kubwa maishani mwako
 
kusoma ujui hata picha hutambui, huyo anataka dushelele na wewe kwa vile unaidhamini ndoa yako kaa mbali naye kwa kupunguza matani kwake na kuwa bize na mambo yako mwenyewe atajishitukia kama alikua anataka roho kitu inapenda ataacha
 
akuna lingine zaidi wewe nenda kamuangalie akiwa amezivaa umuambie ametoklezea.:becky:
 
Eti jamani, hili la kutoa zawadi ili usamehewe na mkeo, mi naliona kama rushwa eti! Sijui wengine mwanalionaje?
 
Si ajabu ana degree. Sasa sisi tusiokuwa na hata certificate sijui tuandike vipi! Kweli dunia uwanja wa fujo.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums

Typing error mkuu, usikariri. Hata mwenye PhD anakosea
 
Eti jamani, hili la kutoa zawadi ili usamehewe na mkeo, mi naliona kama rushwa eti! Sijui wengine mwanalionaje?

Rushwa mbona ziko nyingi tu, hata kuomba msamaa ni kutoa rushwa ili usamehewe. Ilitakiwa usamehewe bila kufanya lolote lile
 
Sasa kaka unamnunulia mwanamke mwingine chupi wakati una mke!Lazima akusumbue kwani waweza kuta jamaa yake hata akiambiwa hizi chupi nimezipenda huwa hamnunulii!
 
Back
Top Bottom