Labda alikuwa changudoa bila mimi kujua

Labda alikuwa changudoa bila mimi kujua

kadovela

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2016
Posts
471
Reaction score
679
Kuna binti nilikuwa nae katika mahusiano ila kwa bahati mbaya siku ya makubaliano ya kupewa mchezo ilikuwa kesho yake anasafiri kwenda nje ya mkoa kufanya kibarua baada kupewa penzi nilimpa kiasi cha pesa kama mkono wa kwaheri japo nahisi mwenzangu aliitafsiri vibaya.

Kila shida akiwa huko lilikuwa jukumu langu, zaidi ya 60 elfu nilimpatia akiwa huko aliporudi tukapanga siku ya kulienzi penzi tukiwa faragha kimbembe kilianza baada ya kutoka guest ile kumshika mkono hataki eti watu wasijue kama wapenzi.

Mara ananiambia tumalizane kabisa nirudi zangu kwetu basi nikatoa jero nikamwambia hii ya vocha kesho mapema nitaweka mambo sawa, eti akaanza kunifokea wewe una akili kweli utanipaje jero?

Nikamuuliza kwahiyo unaniuzia au? mbona mimi nilikuwa nakusaidia hukiwa nje ya mkoa bila kupata penzi kutoka kwako?anasema je wewe ungekuwa msichana ungerizika kweli?.
fedha? au kosa hivi huu ndio utaratibu kweli au huyu wangu anatumia mwili wake kupata langu lilikuwa kumpa hela ile mara ya kwanza ya mkono wa kwaheri?
 
yan baada ya mchezo akadai hela...jibu unalo mwenyewe mkuu
 
Hahahahaa am really sorry nimecheka.ila jero mkuu!!??????????

Anyway, back to your story...ndiyo anajiuza!

Next question please.
husinicheke ndugu hilo jero lilikuwa kama kilinda mfuko baada ya kulipia guest, kwamba nitaombwa hela na mpenzi ambaye akiwa na matatizo namsaidia bila kudai malipo yoyote wala sikuwahi kufikiria. hivi katika hali kama hii usalama upo kweli?
 
Ndiyo maana huwa ninasema, Biblia ilipoandika 'Kila aziniye na mwanamke hana akili kabisa' haikukosea. Kama kweli pesa uliyokuwa nayo ulilipia guest ukabakiwa na shilingi 500, maendeleo kwako yatakuja lini?

Nilishaamua mwaka huu sitamshauri mtu yeyote kwenda kuzini ila kama hata chumba cha kupanga huna kwa ajili ya kukutana na mwenza wako wewe sijui nikushaurije. Acheni zinaa ndugu yangu..fanya mambo mengine ukiona umeshindwa kabisa kujizuia tafuta mmoja uoe. Kila siku utaendelea kuuziwa tu maana hakuna mwanamke siku hizi aliye tayari kukosa vyote. Kwa maelezo yako huna mpango wowote wa zaidi ya mwezi na huyo binti zaidi ya kuzini. Sasa kwa nini asidai malipo yake tu mapema.

Ni kweli alikuwa anakuuzia ila unasahau na wewe ni mnunuzi tu sema hutaki kujikubali.

Ila dah..kweli sitaki kushauri uzinzi, ila hiyo jero imenichekesha sana aisee!!! Jero!????
 
Sorry honey... mambo mengine yanakera matusi hayana budi kuja..

Silali? We umelala au nitoe siri tulikuwa wapi mpk nikawahi kuamka?

hahahhah naona unataka nikosanisha na wifi hapa sky
 
kwa staili hii tutakufa wengi maana ingekuwa nimemkuta barabarani sawa. kweli mapenzi hayana husomi na bachelor yangu naulizwa na binti aliyeishia shule ya msingi una akili wewe utanipaje jero?.

Wewe una akili ya shule, yeye ameishia la saba lakini ni street smart! Ngoma draw! [emoji23][emoji23]
 
Ndiyo maana huwa ninasema, Biblia ilipoandika 'Kila aziniye na mwanamke hana akili kabisa' haikukosea. Kama kweli pesa uliyokuwa nayo ulilipia guest ukabakiwa na shilingi 500, maendeleo kwako yatakuja lini?

Nilishaamua mwaka huu sitamshauri mtu yeyote kwenda kuzini ila kama hata chumba cha kupanga huna kwa ajili ya kukutana na mwenza wako wewe sijui nikushaurije. Acheni zinaa ndugu yangu..fanya mambo mengine ukiona umeshindwa kabisa kujizuia tafuta mmoja uoe. Kila siku utaendelea kuuziwa tu maana hakuna mwanamke siku hizi aliye tayari kukosa vyote. Kwa maelezo yako huna mpango wowote wa zaidi ya mwezi na huyo binti zaidi ya kuzini. Sasa kwa nini asidai malipo yake tu mapema.

Ni kweli alikuwa anakuuzia ila unasahau na wewe ni mnunuzi tu sema hutaki kujikubali.

Ila dah..kweli sitaki kushauri uzinzi, ila hiyo jero imenichekesha sana aisee!!! Jero!????
si kwamba sijapanga la hasha na si kwamba sikuwa na nia nae hapana. kuja kwetu alikuwa anakataa
 
Usiku wa siku hiyo ulikula lakini? Maana ulibaki na jero?!
aah kula nilikula nyumbani kwangu mambo ya mlo si kikwazo kikwazo ni huyu binti anayependa kukutania guest tu
 
Back
Top Bottom