thats true, kabsaaaa maana maumiv hupoa baada ya siku nyingi sana kupitaila inauma kujitoa mzima mzima kumbe mwenzio anapita njia ..
Somo kuntuHabari za wakati huu ndugu na marafiki wapendwa wa JamiiForums....
Ni siku nyingine tena tulivu ikiambatana na manyunyu ya hapa na hapa pale kwa sisi wakazi wa Dar......
Leo ningependa kuwashirikisha katika jambo muhimu sana ndugu zangu ambalo hata mimi binafsi ninaweza kuwa shahidi kabisa....
Kuna kipindi nyakati za nyuma kidogo nilitokea kumtamani binti fulani hivi ambaye tulikuwa tukiishi nae karibu na nilipokuwa nikiishi mimi kusema ukweli huyu mimi sikumpenda isipokuwa nilikuwa namuhitaji kwa ajili ya kukidhi matakwa yangu ya kimwili, kutokana na ushawishi mkubwa nilifanikiwa kumnasa yule binti na tukaanza kushiriki ngono huku yeye akijua kuwa mimi ndiye mumewe mtarajiwa yule binti alikuwa ni binti mwenye kujitegemea maana alikuwa anafanya kazi kwenye kampuni fulani kubwa hivi ya kigeni kwa hiyo suala kipato alikuwa tatizo kwake alichokuwa anakihataji ni mapenzi au mume ambaye aliamini kuwa ameshampata.....
Baada ya kukidhi haja zangu nikaanza kumkwepa kwa maana nilimuona kama ni kero vile kwangu, yule dada nilimpa wakati mgumu sana kwa mabadiliko yale na alikuwa akilia mbele yangu mara kwa mara akinisihi nisimuache lakini mimi sikuelewa lolote lile,yule mwanamke akakata tamaa na akaamua kuachana na mimi lakini alinitamkia maneno mazito sana kuhusu maisha yangu ambayo nilianza kuyaelewa maana yake baada ya mwezi kupita tangu kukata mawasiliano naye......
Niliona ghafla mambo yangu yanabadilika na kuwa mabaya kabisa biashara zangu nyingi sana zilikwama mpaka nikawa nakosa hata hela ya kula ile hali ikanishtua sana maana haikuwa kawaida ikabidi kuahangaika katika mambo ya kiswahili ndipo wataalamu waliponifunulia kuwa kuna mtu ana kinyongo na wewe kwa hiyo unatakiwa ukamiombe msamaha maana ndio njia pekee ya wewe kuondokana na mikosi hiyo maana hakuna aliyeniroga.....
Ikanibidi kwa unyonge kabisa nijipendekeze kwa yule binti na kuanza kujenga naye ukaribu upya na kuomba misamaha mingi sana....
Baada ya muda nikaona mambo yanaanza kubadilika na kuwa kama kawaida.....
N:B Dhumuni la mimi kushare kisa hiki ni kuwaasa vijana kuwa kama mwanamke huna mipango naye ya muda mrefu basi usimpotezee muda wake bure maana utamuacha na sononeko ambalo litakuletea mikosi kwenye maisha yako wapo vijana wasomi wanaohangaika kutafuta kazi takribani miaka kumi wapo vijana wanaojaribu kuanzisha biashara zao lakini huwa zinakufa wapo vijana wanaofukuzwa kazi katika mazingira ambayo hata yeye hawayaelewi hizi ni moja ya athari za watu waliokuwa na vinyongo na wewe.....
Shtuka kijana
Pole sana aisee he was playing with UA feeling yani pamoja na kubeba kiumbe chake hakuwa na huruma naweNimekumbuka mbali sana Mungu nisaidie...nakumbuka jamaa alinichumbia na ujauzito juu...nililia sana aliponiambia sikupendi nimepata mwungine hapo kwake anitaki nyumban naambiwa nenda kwa aliekupa ujauzito...hakuna kipindi kugumu nilichopitia katika maisha yangu kama kile asante Mungu kwakua kila jaribu ulipa mlango wa kutokea sasa hv ukimuona du mwacheni Mungu aitwe Mungu
Bora umuache kwa amani tu upunguze mazoea taratibu ila kumuacha kwa kujifanya mjuaji wala ujiandae tafta namna umpe ukweli kuwa huna future nayeDah! Sijui huyu mwanamke wangu nimuache vipi maana kiukweli anamapenzi makubwa sana juu yangu ila sina hata future naye maskini!
Tena bora sisi wanamume ni wachache sana wanaoweza kukutolea kauli hizo wengi hupuuzia na kusahau ila wanawake sio wote bali wengi duh utajuta hapo kasema tu hajaacha shughuli zake na kukuendea kwa matunge(mganga)jasho litakutoka.Pole kwa yaliyokukuta.....i hope ulisamehe....
Umewahi kujiuliza kwanini wajane ni wengi kuliko wagane!nimesoma huu uzi na comments. nimeona wanaoathirika sana ni wanaume kutokana na kuacha wenza wao. pia kuna wanawake ni wagumu kusamehe
mimi nimeachwa zaidi ya mara tatu na wanawake ila wanadunda tu na maisha yao.
Hisia sio kitu cha kuchezea kabisa. Hebu tujiepushe na haya mambo ya kuendekeza tamaa za mwili wakati huku unajua unaumiza wengine.
Heshima na upendo vituongoze sisi sote
Ukarekebishe mkuu kama ulimliza mtoto wa mtuHii mada imenigusa na kunifunza sana.
ni kweli kabisa.Umewahi kujiuliza kwanini wajane ni wengi kuliko wagane!
Ni machozi ya wanawake yanawamaliza wanaume
Kuna wengine hudiriki kusema "MACHOZI YA SAMAKI..!"kweli
si vizuri mtu akatoa machozi kwa sababu yako,iwe ni mahusiano,kudaiana,dhuluma au chochote kile coz machozi ya mtu huwa hayarudi bure, thnx kwa somo
Mwee[emoji126] [emoji126] [emoji125] [emoji125] [emoji125]Hakuna kitu kinauma kama kupotezewa Muda, Ex wangu hadi leo pamoja na kuwa na kazi nzuri maisha yake hayaeleweki, kwenye mahusiano ndo usiseme, nabado napiga goti kwa Mungu siku atakayorudi kuomba msamaha kwakunikosea ndo amwachilie.
Kwani wanaume hatupotezewi muda[emoji15] [emoji15] [emoji15]Ni kweli usemayo,hakuna kitu kinauma kama kupotezewa muda jamani, umejitunza na kuwakataa wengine wenye nia afu mtu anakuacha hewani gafla,uwiii.... Mungu niepushie isinitokee tena