Laana ya mwanamke

Laana ya mwanamke

Nimekumbuka mbali sana Mungu nisaidie...nakumbuka jamaa alinichumbia na ujauzito juu...nililia sana aliponiambia sikupendi nimepata mwungine hapo kwake anitaki nyumban naambiwa nenda kwa aliekupa ujauzito...hakuna kipindi kugumu nilichopitia katika maisha yangu kama kile asante Mungu kwakua kila jaribu ulipa mlango wa kutokea sasa hv ukimuona du mwacheni Mungu aitwe Mungu
 
Hizi laana zitaendelea sana kutupata kwani wanawake bila kudanganywa aisee hupati kitu, ukisema ukweli utazungushwa balaa kama kwenda ofisi ya uma kupata huduma bila kuwa hata na hela ya rushwa kidogo.
Habari za wakati huu ndugu na marafiki wapendwa wa JamiiForums....

Ni siku nyingine tena tulivu ikiambatana na manyunyu ya hapa na hapa pale kwa sisi wakazi wa Dar......

Leo ningependa kuwashirikisha katika jambo muhimu sana ndugu zangu ambalo hata mimi binafsi ninaweza kuwa shahidi kabisa....

Kuna kipindi nyakati za nyuma kidogo nilitokea kumtamani binti fulani hivi ambaye tulikuwa tukiishi nae karibu na nilipokuwa nikiishi mimi kusema ukweli huyu mimi sikumpenda isipokuwa nilikuwa namuhitaji kwa ajili ya kukidhi matakwa yangu ya kimwili, kutokana na ushawishi mkubwa nilifanikiwa kumnasa yule binti na tukaanza kushiriki ngono huku yeye akijua kuwa mimi ndiye mumewe mtarajiwa yule binti alikuwa ni binti mwenye kujitegemea maana alikuwa anafanya kazi kwenye kampuni fulani kubwa hivi ya kigeni kwa hiyo suala kipato alikuwa tatizo kwake alichokuwa anakihataji ni mapenzi au mume ambaye aliamini kuwa ameshampata.....

Baada ya kukidhi haja zangu nikaanza kumkwepa kwa maana nilimuona kama ni kero vile kwangu, yule dada nilimpa wakati mgumu sana kwa mabadiliko yale na alikuwa akilia mbele yangu mara kwa mara akinisihi nisimuache lakini mimi sikuelewa lolote lile,yule mwanamke akakata tamaa na akaamua kuachana na mimi lakini alinitamkia maneno mazito sana kuhusu maisha yangu ambayo nilianza kuyaelewa maana yake baada ya mwezi kupita tangu kukata mawasiliano naye......

Niliona ghafla mambo yangu yanabadilika na kuwa mabaya kabisa biashara zangu nyingi sana zilikwama mpaka nikawa nakosa hata hela ya kula ile hali ikanishtua sana maana haikuwa kawaida ikabidi kuahangaika katika mambo ya kiswahili ndipo wataalamu waliponifunulia kuwa kuna mtu ana kinyongo na wewe kwa hiyo unatakiwa ukamiombe msamaha maana ndio njia pekee ya wewe kuondokana na mikosi hiyo maana hakuna aliyeniroga.....

Ikanibidi kwa unyonge kabisa nijipendekeze kwa yule binti na kuanza kujenga naye ukaribu upya na kuomba misamaha mingi sana....

Baada ya muda nikaona mambo yanaanza kubadilika na kuwa kama kawaida.....

N:B Dhumuni la mimi kushare kisa hiki ni kuwaasa vijana kuwa kama mwanamke huna mipango naye ya muda mrefu basi usimpotezee muda wake bure maana utamuacha na sononeko ambalo litakuletea mikosi kwenye maisha yako wapo vijana wasomi wanaohangaika kutafuta kazi takribani miaka kumi wapo vijana wanaojaribu kuanzisha biashara zao lakini huwa zinakufa wapo vijana wanaofukuzwa kazi katika mazingira ambayo hata yeye hawayaelewi hizi ni moja ya athari za watu waliokuwa na vinyongo na wewe.....

Shtuka kijana
 
Yalinikuta kwa hiyo siwezi kubisha chochote. Kuna huyu mwanamke nilimzalisha na sikuwa tayari kuishi naye, alilalamika sana. Balaa nilililopata baada ya siku chache tu, itachukua years to recover.

Pamoja na ubishi wangu nilijipeleka kanisani mwenyewe na ndio kwa mbaaali mambo yakaanza kuwa easy na sasaivi naongea na yule mwanamke na ikiwezekana ntaenda kumchukua tuishi wote japo saivi mtoto ni mkubwa tu
 
Hii thread naondoka nayo, Huyu mama nanihii kumbe nisimuache eeh, maana toka niko nae sijawahi kupata shida duh, noma sana!
 
Ni kweli usemayo,hakuna kitu kinauma kama kupotezewa muda jamani, umejitunza na kuwakataa wengine wenye nia afu mtu anakuacha hewani gafla,uwiii.... Mungu niepushie isinitokee tena
Vale inaonyesha uliumizwa sana coz umerudia tena kauli hii, pole sana
 
Dah! Sijui huyu mwanamke wangu nimuache vipi maana kiukweli anamapenzi makubwa sana juu yangu ila sina hata future naye maskini!
 
Hakuna kitu kinauma kama kupotezewa Muda, Ex wangu hadi leo pamoja na kuwa na kazi nzuri maisha yake hayaeleweki, kwenye mahusiano ndo usiseme, nabado napiga goti kwa Mungu siku atakayorudi kuomba msamaha kwakunikosea ndo amwachilie.
wewe ni kabila gani?
 
Hata sisi huwa tuna laana....ila hapa nimeongelea wanawake kwa kuwa ndio wahanga wakubwa sana kwenye mahusiano kwa kuwa vijana wanatumia muda mwingi kumuaminisha mwanamke kuwa yeye ni wake wa milele ili hali kwenye nafsi yake haipo hivyo.....ndipo laana zinapoanzia hapo....
usipomuaminisha haupati Free papuchi,sasa nani anataka kugharamia?
 
Hakuna kitu kinauma kama kupotezewa Muda, Ex wangu hadi leo pamoja na kuwa na kazi nzuri maisha yake hayaeleweki, kwenye mahusiano ndo usiseme, nabado napiga goti kwa Mungu siku atakayorudi kuomba msamaha kwakunikosea ndo amwachilie.

Toa msamaha, utakuwa huru pia.
 
Yalinikuta kwa hiyo siwezi kubisha chochote. Kuna huyu mwanamke nilimzalisha na sikuwa tayari kuishi naye, alilalamika sana. Balaa nilililopata baada ya siku chache tu, itachukua years to recover.

Pamoja na ubishi wangu nilijipeleka kanisani mwenyewe na ndio kwa mbaaali mambo yakaanza kuwa easy na sasaivi naongea na yule mwanamke na ikiwezekana ntaenda kumchukua tuishi wote japo saivi mtoto ni mkubwa tu
Nasikia wakwe wamekuambia ulipe faini ya kukulelea mwanao kwa miaka hyo tisa..polee sana
 
Vale inaonyesha uliumizwa sana coz umerudia tena kauli hii, pole sana
Ndio maisha ndugu yangu, tunapata wasiotambua thamani zetu hili ni pande zote... Kikubwa ni kusonga mbele na tunajifunza kutokana na makosa ili ikitokea anaekuthamini usimuache zaidi ya kumtendea vema...
 
Ndio maisha ndugu yangu, tunapata wasiotambua thamani zetu hili ni pande zote... Kikubwa ni kusonga mbele na tunajifunza kutokana na makosa ili ikitokea anaekuthamini usimuache zaidi ya kumtendea vema...
Wanaume kiujumla tumeumiza wengi, hili ni tatizo sana kwani limeleta madhara makubwa, ninapoona mabinti wanajiuza naumia sana coz wengi waliumizwa sana then wakakosa imani na wanaume wote wakijua na kuamini hakuna waoaji au wanaume waaminifu na ndipo wakajirahisisha japo sio wote.
Wanaume baadhi wamesababisha machokoraa kwa kuwatelekeza wanawake na kushindwa kulea watoto hatimaye wako mitaani kuokota vitu vya kuuza, sio hivyo wamesababisha vifo kwa wadada kwani waliwapa ujauzito na kuwakana na wakaamua kutoa ndipo kifo kikawapata. Wanaume wenzangu tubadilike tumeumiza wengi, na wengi wanalia kwa ajili yetu kwanini mabaya yasitupate?
Tuwe wakweli mbona dada zetu ni waelewa tu?
Mwambie aina ya urafiki uutakao kwake naye atakuelewa. Mtusamehe sana dada zetu
 
Ndio maisha ndugu yangu, tunapata wasiotambua thamani zetu hili ni pande zote... Kikubwa ni kusonga mbele na tunajifunza kutokana na makosa ili ikitokea anaekuthamini usimuache zaidi ya kumtendea vema...
Usife moyo utapata atakayekufanya usahau magumu yoote
 
Kusamehe napo ni mtihani,sio rahisi kama mkosaji anavyofikiria tena makosa ya makusudi yanaumaga balaa ni basi tu We love God so kupenda watu wake (wema kwa wabaya) ni amri otherwise walioniumiza wote acid zingewahusu,kama sio sumu,au kuchoma nyumba zao,achilia mbali kuwatengenezea ajali au hata kuwakodia majamaa wawageuza nyuma na picha juu kubandika mji mzima angalau tujumuike pamoja ktk maumivu.





Tuwatendee wenzetu tunayopenda kutendewa,tuwe wakweli ili mwenzio ajue atajiweka position ipi kwako,au aamue kuliwa kwa kupenda ye mwenyewe na sio kwa uwongo wako....
 
nimesoma huu uzi na comments. nimeona wanaoathirika sana ni wanaume kutokana na kuacha wenza wao. pia kuna wanawake ni wagumu kusamehe

mimi nimeachwa zaidi ya mara tatu na wanawake ila wanadunda tu na maisha yao.

Hisia sio kitu cha kuchezea kabisa. Hebu tujiepushe na haya mambo ya kuendekeza tamaa za mwili wakati huku unajua unaumiza wengine.

Heshima na upendo vituongoze sisi sote
 
Hii kitu ni atar sana kwaafya na mustakabali wa maisha kwa ujumla tujiepushe jaman me yashanikuta lakin nashukuru mungu nilichomoka salama
 
Mleta mada, mimi siamini kuwa machozi yake(yao) yatanipa laana, kwa sababu;
1. Mbele za M/Mungu tulifanya dhambi ya uzinzi, ngono na uchafu ambao Mungu hapendi.
2. Tulitenda dhambi ya uongo wote (mimi nilimdanganya, nae kadanganya kwa Mungu)
Hayo yaliyokupata ni sehemu ya maisha tu (ups and downs) na wala haihusiani na kumdanganya au kuchezea mwili na hisia zake. Mwanamke wa kweli hachezewi mwili coz anaitambua thamani ya mwili wake, the worst you can do ni kuchezea hisia. Mwanamke/mwanaume anayechezewa mwili ni mjinga mjinga tu..
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom