Mie moyo wangu una kisebengo, hata mtu anitende vipi, nitamsamehe tu kwa moyo mmoja. Najua kulia mimi jamani, but Nikimaliza tu nashusha pumzi "Mungu Ahsante kwa yote", afu namalizia kale kamsemo kangu "I don't lose people, people lose me" lol.
Ntakuwa tu na hasira wiki za kwanza, hapo mtu asinitafute sio kwa hilo povu ntakalomtolea, but huyo baadaye nasamehe na kusahau. Kukaa na kinyongo moyoni kunaniumiza zaidi mimi mwenyewe na hakuna kitu nachovalue kama my peace of mind, siruhusu mtu au kitu kiniharibie furaha yangu, Never. And thank God moyo wangu una space tu kwa ajili ya Mungu na kwa ajili ya watu wachache ninaowapenda sana. No space kwa ajili ya chuki au kinyongo
So tujifunze tu kusamehe hata bila kuombwa msamaha.
1. Ili tusizuie baraka zetu
2. For your peace of mind. Kwa nini mtu mwingine akukoseshe amani? She/he isn't that much worth. Afu imagine kuishi juu juu kusubiri mtu aanguke, bahati mbaya kuna muda kila unavyosubiria aanguke ndo yeye anazidi kubarikiwa na msamaha hakuombi hahaha
3. You have learnt your lesson. Kuna muda we learn some lessons in a very hard way, kiasi kama ingekuwa unaambiwa tu kwa maneno bana kuna A, B, C usingeelewa hadi yakukute. Despite maumivu na Kila kitu, lakini kila mahusiano yana somo nyuma yake. Shukuru Mungu umepata somo lako mapema, litumie vizuri.
Mnaotenda wenzenu, endeleeni tu... mtakipata