Ebwana ndiyo,
siasa za mbeya kweli tamu saaana.
kama huu mwongozo ndiyo anautegemea kwa ajili ya kumng'oa Mwakyembe, atakuwa amechemsha vibaya mno.
Halafu huu mbona sio mwongozo! haya ni majungu tu mbona hakuna chochote cha maana!
Kama hii ndiyo hekima ya Mwakipesile basi Mbeya bado safari ndefu sana kupiga hatua za kimaendeleo, ndio maana hata miradi mikubwa na mizuri kama uwanja wa ndege wa Songwe upo upo tu kama kambi ya wakimbizi.
Halafu kusema kweli hata kama mwakalinga ni mwenzetu hapa JF na tunahitaji kumuunga mkono ili afanikiwe kuingia mjengoni, sharti ajiepushe na watu wachafu.
Hakuna namna yeyote ataweza kusimamia maslahi ya watu wa kyela na Tanzania kwa ujumla kama nyuma yake ana support ya mafisadi.
Kila siku hapa tunamnyoshea vidole JK ameshindwa kuwachukulia hatua mafisadi kwa kuwa ndio waliombeba hadi kuingia magogoni, kwahiyo hatuwezi kutegemea lolote jipya toka kwa Mwakalinga kama anabebwa na fisadiz.
Tatizo wabaya wake ndio wanamwandalia waraka na kuuza hapa jf harafu wanajifanya ndio waraka wake.
Kwanini kuchafuana lakini? wapigane kwa hoja kama kweli wanaona uchungu wananchi wanavyoteseka.