Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 117,778
- 218,404
Baada ya kufichuka kwamba Watendaji wa Halmashauri ya Mbeya ni wezi na kuthibitika kuwa , wamechepusha mapato ya halmashauri na kugawana wanachochepusha (yaani Pasu pasu) , Nakuomba sana Mh Samia uimurike Halmashauri ya Kyela .
Halmashauri ya Wilaya hii hakuna anayeiamini tena baada ya KUGAWA SOKO LA WILAYA YA KYELA BURE KWA CCM , Soko hilo ambalo ndio lilikuwa Chanzo pekee cha Uhakika cha Mapato ya Halmashauri hiyo limegawiwa katika mazingira ambayo yamegubikwa na giza nene , Wananchi wengi wanaamini kwamba ccm inasingiziwa tu , Wanahisi kwamba soko hilo limemilikishwa kwa baadhi ya Vigogo wa ccm wilayani humo .
Wakati soko hilo inanyang'anywa Halmashauri na kupewa kinachoitwa CCM , Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo aliitwa HUNTER MWAKIFUNA , aliyekuwa Diwani wa Kata ya Ipinda , Mbunge aliitwa Dkt Harrison Mwakyembe , sikumbuki DED aliyekuwepo .
Kwa ujumla Halmashauri ya Wilaya ya Kyela imekabidhi maeneo yote ya wazi na club za Pombe za kienyeji , ambazo wazee walikuwa wanajiburudisha mida ya jioni kwa ccm , Naweza kuthibitisha kwamba Club cha kienyeji kinachoitwa MKIBHEGE cha kijiji cha Bondeni , eneo la wazi ambalo wananchi walijenga mabanda ya kuuzia UBWALWA imekabidhiwa kwa ccm na wanachukua kodi .
Swali letu ni hili imekuwaje Halmashauri ya Kyela imejinyang'anya mali na kuipa ccm ? Je ni kweli jambo hili au wako Watumishi kama wale wa Mbeya wamejichepushia Mambo haya ili Wajilie Mali ya Umma ?
TUNAKUOMBA MH RAIS UIMULIKE HALMASHAURI HII KWA DARUBINI KALI