Kwimba: Taasisi ya Alicia Keys yawasili nchini kushiriki uzinduzi wa jengo la watoto njiti

Kwimba: Taasisi ya Alicia Keys yawasili nchini kushiriki uzinduzi wa jengo la watoto njiti

Pfizer

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2021
Posts
726
Reaction score
953
Timu ya Wawakilishi kutoka Taasisi ya Keep A Child Alive ya Msanii maarufu wa Marekani, Alicia Keys, imewasili nchini Tanzania kupitia uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwl.Julius K. Nyerere tayari kwa ajili ya kwenda Wilayani Kwimba Mkoani kwenye uzinduzi wa jengo la kisasa la kuhudumia Watoto njiti lililojengwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kwimba.

Timu hiyo baada ya kuwasili Airport imeelekea hadi Hospitali ya Amana na kuwajulia hali Wagonjwa kisha kuwapa zawadi pamoja na kujionea mazingira ya huduma kwa Watoto njiti ambapo wameahidi kuendelea kutoa misaada mbalimbali ikiwemo ya miundombinu na vifaa tiba.

Kiongozi wa Wawakilishi hao, Antonio Ruiz-Gimenez, ameelezea historia yake fupi ya namna alivyopata Mtoto njiti na hivyo anaguswa kuwasaidia Watoto njiti nchini Tanzania akishirikiana na Serikali na Wadau mbalimbali wakiwemo Doris Mollel Foundation (DMF).

Jengo la kuhudumia Watoto njiti lenye viwango vya Kimataifa limejengwa Kwimba na Taasisi ya Doris Mollel (@dorismollelfoundation) chini ya Mkurugenzi Mtendaji wake Doris Mollel (@dorismollel) na linatarajiwa kuzinduliwa leo February 28,2026.
 
Hongera kubwa sana kwa hili. Watoto wote wanaozaliwa wana haki ya kukua na kustawi vizuri no matter walizawa wakiwa njiti au

Big up to the Team
 
Team imewasili nchini Tanzania kupitia uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwl.Julius K. Nyerere

was this necessary au bado unauchanga kwenye uandishi
 
Hivi hapa tz kuna msanii ana taasisi ya kushughulika na masuala ya jamii kama afya, elimu, mazingira, uchumi, michezo na burudani? Au wao wanamiliki lebo zao tu?
 
Ehe wasanii wenu huko maarufu washafanya nini?
Kurudisha kwa jamii

Ova
 
Hivi hapa tz kuna msanii ana taasisi ya kushughulika na masuala ya jamii kama afya, elimu, mazingira, uchumi, michezo na burudani? Au wao wanamiliki lebo zao tu?
Wao kazi yao ni kutuonesha wanawake zao wenye makalio makubwa tu

Ova
 
Back
Top Bottom