Uchaguzi 2020 Kwenye mitandao ya kijamii na mtaani, Membe hakubaliki

Lisu ndo hatari maana akipata hata wafuasi m3 halafu akataa matokeo wakaamua kuingia barabarani tayari ni tatizo. Mgombea anayehitajika ni yule ambaye atasema nimeibiwa kura ila tulieni.
 
Binafsi siwezi poteza kura yangu kwa act, maana hata ujio wake tu umejaa usaliti wa mageuzi halisi.
Membe naye kaenda huko kuangamiza kale kachama sijui sijui ccm wamemwambia kanaelekea kupata nguvu??
Kiufupi membe na zito ni ccm tu, hakuna jipya
 
Membe kama ana nia ya dhati basi aweke form yake uvunguni na akamuunge mkono Lissu/Nyarandu/Msigwa. Ni ufala na dharau kubwa kuwaambia hao aliowakuta eti wamuunge mkono. Huu ni ubinafsi wa kiwango cha juu sana.
 
sio kwamba Membe hakubaliki mitaani bali hajulikani na hazungumziwi kabisa, atumie fursa hii ya uchaguzi kujitangaza na si kushindana!! ila hapa ACT atapaa zaidi kuliko sisiem Mkulu kafunika members wote kule!!
 
Mnanichekesha sana mnaposema leo hii Lowasa aliwaingiza kingi!

Kwahiyo mlipokuwa mnaambiwa mlifikiri mnaonewa wivu au?
Thats the sad truth

Nipo upinzani,simkubali Membe

Ananikumbusha Lowassa nostalgia....Lowassa made all of us look like fools.

We cant take this nigga serious!
 
Lissu anakubalika sana hilo sina ubishi,

Isipokuwa kama Membe akisimama na Magufuli, Magufuli anapigwa asubuhi na mapema.

Watu wana hasira na utawala wa Magufuli zaidi kuliko kutomjua Membe

Nyalandu huyo anashika mkia kwenye kukubalika!
Mungu ndiye anayejua mioyo ya watanzania. Kiukweli wanavooneka sivo walivyo. Wana kitu moyoni na kukiwa utaratibu mzuri na wagombea wazuri bila kujali chama tunaweza kushudia maajabu.

Sent from my Nokia 6.1 using JamiiForums mobile app
 
Msukuma Original,
Lakini sauli aliyebatizwa kuitwa Petro alikuwa farisayo aliyewaua na kuwatesa wakristu, lakini ni huyu sauli ndo kaeneza injili duniania kuliko petro swahiba yake Yesu.
Dogo usikariri
Nashangaa watu walopewa upako wa kuhubir injili wanaweka biblia kando na kubeba ilani. Wanajua kabisa siasa haina kitu maalumu bali huchanganya vyote, haki na dhulma, upendo na chuki, ukweli na uwongo, utu na udhalimu, wema na ubaya
Kazi ya viongozi wa dini kuhusu wanasiasa na siasa ni kukemea mabaya na kuhimiza mazuri katika siasa ili watu waishi vizuri zaidi duniani.


Sent from my Nokia 6.1 using JamiiForums mobile app
 
Utafiti wako ulitumia methodolijia gani?

Membe anakubalika sana, nimefanya utafiti binafsi juu ya hilo!

Wewe umeuliza wakulima wangapi, wafanyakazi wangapi, wanawake wangapi, wanaume wangapi, umeuliza vijana wangapi, wazee wangapi, umeuliza watu mikoa ipi.


Kama kukiwa na uchaguzi huru na haki Magufuli ajiandae kukabidhi Ikulu kwa Membe au Lissu

Ulichokiandika kinafurahisha na kuwapa amani ya matarijio mema na furaha ya muda wafuasi wa upinzani, hasa ujio wake Membe.

Niko mikoani kwa shughuli zangu, tena vijijini, na hata kwao Membe nimepita, wimbo ni Magufuli tu, kuanzia watoto hadi wazee. Hakuna asiyemjua Magufuli kwa sababu ndiye anahusishwa na elimu bure, madawati, barabara zinazopitika majira yote, zahanati, wakulima kutokusumbuliwa wakati wa kusafirisha na kuuza mazao yao, machinga kufanya biashara zao kwa amani bila buguhuza, na kadhalika.

Kuishi kwa matumsini huongeza siku za maisha, bila shaka
 
Back
Top Bottom