Kwenye misiba tunafanya nini hasa, kuaga mwili wa marehemu au kumuaga marehemu? Kutoa heshima kwa mwili wa marehemu au kutoa heshima kwa marehemu?

fazili

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
13,819
18,563
Kifo ni fumbo. Ni nini hasa hutokea mtu anapokufa? Je binadamu ni nini hasa mwili au pumzi ya uhai ndani ya mwili au vyote? Je ni sahihi kusema tunaaga mwili wa marehemu au tunamuaga marehemu?

Je hata wale wasioamini maisha nje ya mwili hufanya nini mbele ya miili ya marehemu? Kuheshimu, kuaga, kuomboleza, kuona, kusali au hufanya nini hasa?
 
Ni matakwa tu ya kibinadamu ila haibadilishi chochote kuwa huyo ni mfu, amekufa, hajui lolote, uage, utoe heshima, usindikize nk vyote yeye hajui.

Ni heshima tu kuwa huyu alikuwa binadamu mwenzetu, hakuna lingine. He's dead, he knows nothing na ndio maana anapigwa chepe, thamani yake duniani haipo tena...ukitaka kuthibitisha hilo, muache nje for three days, hakuna atakayeweza kuishi mazingira hayo.
 
Kumbe tunazika kwa faida yetu ,na sio kwa faida ya alie kufa, huwa nashangaa sana mtu asipo enda kanisani hawa wakristo wanatishia eti hautazikwa na mchungaji au padri ,alafu watu wanaogopa kabisa🤔🤔
 
Marehemu azikwe au asizikwe yeye anajua nini mkuu? Ule ubinadamu, ile heshima ya utu wake ndio vinafanya tuchimbe shimo na kufukia mzoga wake huko. Otherwise, wanyama wanakufa na kuliwa na ndege au wanyama wenzao na hakuna tofauti.

Hapa swala sio ukristo au dini yoyote, tunazika kwa kanuni tulizojiwekea wenyewe ili kuheshimu binadamu mwenzetu aliyetangulia. Kuomba/kutoomba having msaada wowote, coz uombe au la yule marehemu hatasikia wala kuona unachoomba. Baadhi yetu tunaamini zile ni ibada kwa waliopo hai, merehemu haombewi.
 
Wengi wanafuata misosi tu na kuuza sura hasa hii misiba ya watu maarufu.

Mfana Monduli kwa leo kumejaa wadangaji, machawa wa kutafuta connection, wanasiasa wanafiki wa kutafuta political mileage.

Kwa ufupi kinachoagwa ni kumbukumbu ya marehemu ila ikiwa marehemu alikuwa maarufu basi kinachofutwa msibani ni kiki tu.
 
Kifo ni fumbo. Ni nini hasa hutokea mtu anapokufa? Je binadamu ni nini hasa mwili au pumzi ya uhai ndani ya mwili au vyote? Je ni sahihi kusema tunaaga mwili wa marehemu au tunamuaga marehemu?

Je hata wale wasioamini maisha nje ya mwili hufanya nini mbele ya miili ya marehemu? Kuheshimu, kuaga, kuomboleza, kuona, kusali au hufanya nini hasa?
Kuna kupita kando ya jeneza la marehemu
Kutoa heshima za mwisho (hufanywa na askari na baadhi ya raia kwa kuinama)
 
Kila mtu ashinde mechi zake ,kila jamii ina taratibu zake nenda hapo Ghana utaona maajabu maiti anawekwa kweny kiti kabisa .
 
Binafsi naona kila mmoja yupo sawa tu , uage usiage ,afe uzike leo au baada ya siju 10 ,utoe uchafu tumboni usitoe yote sawa tu , uliwe na fisi ama uzikwe ,wa kufa ameshakufa tu ,kote huko ni kujilisha upepo tu.
Hawa waislam wanajiona wako smart sana wakat ndio mashetani wenyewe
 
Kila mtu ashinde mechi zake ,kila jamii ina taratibu zake nenda hapo Ghana utaona maajabu maiti anawekwa kweny kiti kabisa .
Rafiki yangu mghana alifiwa na baba yake mwezi wa saba, wakaja kuzika December. Nilishangaa sana, taratibu za mazishi kwao ni kitu nyingine kabisa. Maiti kukaa mortuary kwa miezi mitatu ni kawaida sana.
 
Ghana msiba kama sherehe watu wanafurahia kabisa acha tu hii dunia ,kila mtua ana imani yake.
 
Marehemu azikwe au asizikwe yeye anajua nini mkuu? Ule ubinadamu, ile heshima ya utu wake ndio vinafanya tuchimbe shimo na kufukia mzoga wake huko. Otherwise, wanyama wanakufa na kuliwa na ndege au wanyama wenzao na hakuna tofauti.

Hapa swala sio ukristo au dini yoyote, tunazika kwa kanuni tulizojiwekea wenyewe ili kuheshimu binadamu mwenzetu aliyetangulia. Kuomba/kutoomba having msaada wowote, coz uombe au la yule marehemu hatasikia wala kuona unachoomba. Baadhi yetu tunaamini zile ni ibada kwa waliopo hai, merehemu haombewi.
Wengine wanachoma kabisa hizo maiti
 
Rafiki yangu mghana alifiwa na baba yake mwezi wa saba, wakaja kuzika December. Nilishangaa sana, taratibu za mazishi kwao ni kitu nyingine kabisa. Maiti kukaa mortuary kwa miezi mitatu ni kawaida sana.
na wajaluo pia
 
Ni matakwa tu ya kibinadamu ila haibadilishi chochote kuwa huyo ni mfu, amekufa, hajui lolote, uage, utoe heshima, usindikize nk vyote yeye hajui.

Ni heshima tu kuwa huyu alikuwa binadamu mwenzetu, hakuna lingine. He's dead, he knows nothing na ndio maana anapigwa chepe, thamani yake duniani haipo tena...ukitaka kuthibitisha hilo, muache nje for three days, hakuna atakayeweza kuishi mazingira hayo.
Au ikitokea akafariki ndani ya safari,abiria watataka marehemu awekwe kwenye buti kama mzigo tu.na ukimuacha kwenye kiti abilia watagomea safari.
 
Marehemu azikwe au asizikwe yeye anajua nini mkuu? Ule ubinadamu, ile heshima ya utu wake ndio vinafanya tuchimbe shimo na kufukia mzoga wake huko. Otherwise, wanyama wanakufa na kuliwa na ndege au wanyama wenzao na hakuna tofauti.

Hapa swala sio ukristo au dini yoyote, tunazika kwa kanuni tulizojiwekea wenyewe ili kuheshimu binadamu mwenzetu aliyetangulia. Kuomba/kutoomba having msaada wowote, coz uombe au la yule marehemu hatasikia wala kuona unachoomba. Baadhi yetu tunaamini zile ni ibada kwa waliopo hai, merehemu haombewi.
mkuu ulishawai kufa ukapata uhakika ya kuwa aliyekufa haoni wala kusikia?
 
Back
Top Bottom