Hili la Kulazimisha Mwili wa Marehemu uingie Ndani Kwake ni Takwa la Kiimani au ni Upuuzi Wetu tu Wapuuzi?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,689
109,119
Hivi inaingia Akilini Kweli Marehemu ameishi ndani ya hiyo hiyo Nyumba kwa Miaka 50 na Nature ya Milango ya Nyumba yake mnaijua halafu Amefariki mnauleta Mwili wake Nyumbani Kwake hapo na Kulazimisha uingie Ndani na Kuanza kuwa kama Panya Road na Kuvunja Mlango na hata kuharibu Miundombinu ya hiyo Nyumba yake.

Kwani Marehemu huo Mwili wake ukiletwa na ukakaa tu kwa Nje sehemu iliyopangiwa haitoshi? au hapo Nje siyo sehemu ya Nyumba yake?

Kuna muda GENTAMYCINE huwa nawaza ni nani Katuroga Akili Sisi Waafrika ( japo tupo Wachache ) Wenye Akili Kubwa hadi kufanya huu Upuuzi?

Kuna Nyumba tokea tumalize Maziko ya Mpendwa Wao Jumatatu hadi leo hii Ijumaa naandika huu Uzi Wafiwa Wanahangaika Kuchangishana Pesa ili aitwe Fundi autengeneze Mlango uliovunjwa ili Marehemu ( Mwili wake) ulio katika Jeneza uingie Ndani.

Na cha Kusikitisha zaidi hiyo Familia ina Maisha Duni ( ya Kimasikini ) kama niliyonayo GENTAMYCINE lakini kutokana na Upuuzi Wao sasa wana Majukumu Mawili moja la Kumtafuta Fundi awajengee upya Mlango wao na lingine ni la kutafuta Hela ya Kula.

Na hapa wala GENTAMYCINE nisizunguke huu Upuuzi nauona sana na mno Kwetu Sisi Wakristo na sijui una Tija gani na Utaratibu huu unatoka katika Kitabu gani cha Biblia Takatifu, Sura ya Ngapi na Mstari upi. Kwa Ndugu zetu Waislamu sijaona japo yawezekana kuna baadhi labda wanafanya ila nimehudhuria Misiba yao mingi sijawahi kuona.

Hofu yangu Kubwa GENTAMYCINE ni kwamba Upuuzi huu usipobadilika na Wapuuzi Kubadilika ipo Siku hamtaishia tu Kulazimisha Miili ( Majeneza ) ya Marehemu Iingie Ndani Mwao ( Majumbani ) ball mtalazimisha Majeneza yao yapitishwe hadi Vyooni, Jikoni na Stoo kisha ndipo muitoe Nje iendelee Kuombolezwa.

Na wakati mwingine utakuwa 75% ya hao Wapuuzi wanaolazimisha Miili ya Marehemu ( Majeneza ) yaingie Ndani kwa Kubomoa Milango wakati Marehemu anaugua hawakutoa Mchango wowote au hata tu kwenda Hospitali Kumtembelea.

Tubadilike na tuacheni huu Upuuzi.
 
Culture is the totality of society's ways of life, and variation in terms of individual differences is of great importance and should be appreciated, nothing can be good for everyone.
 
Tafuta hela ukifa uingizww kwenye nyumba yako,roho lazima ikudunde kama unakaa uswazi nyumba ya kupanga.
 
Back
Top Bottom