Kwenye mapendekezo 21 ya ripoti ya Kamati ya Professor Osoro, yapi yana ukweli, yapi si ya kweli? Tumeshatekeleza mangapi? Makinikia ilikuwa usanii?

Jamaa David Mwanyika baada ya kubanwa, akamgeuka Tundu Lissu ambaye alimsikitikia kwa makosa ya kubambikiwa! Lakini serikali ikaunganisha na uongo wa kishika uchumba, kwamba Lissu anatetea mabeberu. Serikali yenyewe ikaingia makubaliano na Barrick Gold na sasa Mwanyika ni mgombea ubunge kwa tiketi ya ccm.
Hii ni serikali ya kishetani na kilaghai sana.... ndio maana watz hawaitaki kabisaa.....
 
Wanajamvi, nadhani suala hili, halikuzungumziwa vya kutosha hata kidogo. Lissu yeye alishaumizwa na wengine walitishika kabisa kulizungumzia!

Hata hivyo, bado limezungumziwa sana na makada wa CCM hata humu ndani. Mfano kina Pasco! Lakini kwa namna ya uongo na propaganda nyingi.

Ripoti yenyewe imelalamika zaidi kuhusu kodi, na ikapendekeza uwepo uwajibikaji kwa watumishi mbali mbali wa ngazi tofauti za serikali kutokana na misamaha ya kodi kwa makampuni hayo!

Ya kuhusu makinikia, hapo hakukuwa na lolote! Hata kile ambacho kada maarufu wa chama humu Pascal Mayalla, alikuja na uongo mwingi sana humu kuhusu kile alichokiita “kishika uchumba”. Lakini ukifuatilia kwa makini, utagunduwa kuwa hata hicho kilicholipwa na Barick kwa niaba ya ACACIA, walilipa tu ili thamani ya hisa zao, isiendelee kushuka kwenye soko la dunia, pamoja na gharama zinazotokana na kuzuiwa kwa makontena hayo, habari kuwa yamezuiwa, ni mbaya zaidi kwa uchumi wa kampuni kuliko kuwndelea na kesi MIGA! Lakini hakuna nilichoona kwamba wamekubali kuwa wamefanya chochote kile kinyume na mkataba ambao ni CCM waliusaini.

Sitaki kuzungumza mengi, nitayaleta mapendekezo yote hapa, kisha tuyachambuwe, kwasababu uchaguzi umekaribia, sasa tujulishane ukweli ili tujuwe kama tuwape kura au tuwapumzishe.

Maana mojawapo ya mapendekezo, ni sisi kuifahamu mikataba, na wale walioisaini na kuipitisha, wawajibike, lakini naona usanii tu huku wapinzani wakisingiziwa na Lissu wa watu.

Pia kamati ilipendekeza kuwa “Serikali ifanye uchunguzi na kuchukua hatua za kisheria, dhidi ya waliokua mawaziri,wanasheria wakuu wa serikali na manaibu wao, wakurugenzi wa idara za mikataba na makamishna wa madini, wanasheria wa Wizara ya madini na watumishi wengine wote waliohusika katika kuingia mikataba ya madini.“

Hapo chini, ni kasehemu ka ripoti hiyo ambayo iliitwa “rubbish” ama takataka ya kiprofesa! Ukiisoma kiukweli ni uongo mtupu! Na ndiyo maana tukalipwa kile Pascal Mayalla alichokiita kuwa ni “kishika uchumba”, yani pesa ama gharama za kumzuilia “mwali”, ama mchumba pale bandarini! Ambapo hicho kishika uchumba cha usd 300m, kilitolewa na Barrick, siyo kwasababu eti wamekubaliana na hiyo ripoti, bali ni kwasababu wanaendelea kupata hasara, khasa kwenye thamani ya hisa zao, ambapo wote tunafahamu kuwa taarifa kama hizo huwa zinaathiri thamani yake kwenye soko la dunia! Lakini kama wangelazimishwa kulipa hicho kiasi kilichotajwa, basi ni kweli MIGA ingehusika! Na hapo ndipo point ya Tundu Lissu ilipokuwepo!

Hapo chini ni sehemu hiyo, nimepunguza vipengele vya madini waliyosema yamo ndani ya makinikia! Vipengele hivyo...

“4. Kwa ujumla thamani ya metali/madini yote katika makinikia kwenye makontena 277 yaliyozuiliwa bandarini, ni TZS bilioni 829.4 kwa kutumia viwango vya wastani na TZS bilioni 1,438.8 kwa kutumia viwango vya juu. Kwa kuwa viwango hivi vya thamani havitumiki kukadiria mapato ya Serikali, ni wazi kuwa kuna upotevu mkubwa sana wa mapato kwa nchi yetu.

5. Thamani zote za madini kwenye makinikia yaliyo ndani ya makontena zilizoainishwa hapo juu, zimepatikana kwa kutumia uzito wa wastani wa tani 20 za makinikia kwenye kila kontena. Hata hivyo, katika kupima uzito wa makinikia ndani ya makontena, kuna makontena kadhaa yaliyokuwa na uzito zaidi ya tani 20 za makinikia, kwa mfano makontena yenye namba CAIU 2461301, TCLU 0701267, MRKU 6880530 na MSKU 4280570 yalikuwa na makinikia yenye uzito wa tani 23.1; 22.9; 22.7 na 22.2, kwa mtiririko huo. Hivyo basi, ongezeko hili la uzito linaongeza thamani ya makinikia na hivyo kuongeza upotevu zaidi wa mapato ya Serikali.

6. Pamoja na kuchunguza makinikia, Kamati pia ilichunguza shehena ya mbale za copper ndani ya makontena matano (5) yaliyozuiliwa bandarini. Sampuli za mbale hizo zilipatikana kuwa na viwango vya dhahabu hadi kufikia 38.3 g/t, viwango ambavyo havikuoneshwa kwenye ripoti ya upimaji wa kimaabara wa TMAA, na hivyo kutotumika katika kukokotoa malipo ya mrabaha Serikalini.”
Ripoti ya uchunguzi wa mchanga wa madini. (Ripoti ya Osoro na Mruma)

cc Nguruvi3
Je, wajua kuna uwezekano Barrick wanatuingiza mkenge?!. Hili la kugawana 50/50 ya faida ni kweli au ni changa la macho tu?.

Update: 22/8/2020
Baada ya hotuba hii ya Lissu, sasa nime connect the dots kuwa yote niliyosema ni ya kweli.

Hata hivyo Dkt. Nchemba amesema, serikali ilikubali kupokea shilingi bilioni 700 kutoka Barrick baada ya makubaliano baina ya timu ya serikali iliyoundwa na Rais wa serikali ya awamu ya tano Hayati Dkt. John Magufuli kufikia makubaliano ya pande zote na Barrick kuhusiana na madai ya shilingi trilioni 360.
Kitu muhimu sana ni Watanzania have the right to information the basis ya kumsamehe mwizi wetu!.

Kama deni hilo ni bonafide genuine, serikali inapoamua kusamehe, it got to give reasons. Na baada ya hapo TRA watoe taarifa kuwa wamelifuta deni hilo.

Haya mambo akina sisi tuliyasema sana humu, kama mwanzo tulizuia makinikia kwasababu tulihisi tunaibiwa kwasababu hatujui kilichomo!.

Tukafanya uchunguzi tutathibitisha ni kweli tumeibiwa!. Tukapiga hesabu tulichoibiwa, baba mtu mbio kaja na ahadi wamekubali kila kitu na ili kuonyeshea nia njema wakahidi kishika uchumba cha Dila milioni 300!.

Mwisho wa mazungumzo tukasamehe deni lote, na kuruhusu makinikia yaondoke huku mpaka leo mpaka kesho, bado hatujui kilichomo!.

Kama tulizuia makinikia kwasababu tunaibiwa kwa kutojua kilichomo, tukathibitisha tunaibiwa!, Tumeruhusuje makinikia bila kujua kilichomo?, kwanini tulizuia?!

More explanation on this is needed.
P
 
Duh! Sikuwa nafahamu kuwa makinikia yameruhusiwa kuondoka bado tukiwa hatujui kilichomo. Kwahiyo issue ya makinikia ilikuwa ni usanii. Kama sivyo, Kuna watu wamekula mlungula.

Hii nchi ngumu sana aisee!
 
Duh! Sikuwa nafahamu kuwa makinikia yameruhusiwa kuondoka bado tukiwa hatujui kilichomo. Kwahiyo issue ya makinikia ilikiwa ni usanii. Kama sivyo, Kuna watu wamekula mlungula.

Hii nchi ngumu sana aisee!
Kuna vitu vingine kiukweli...
  1. Yaani wewe uzuie makinikia kwa hoja tunaibiwa kwasababu hatujui kilichomo
  2. Kisha wewe uunde tume mbili kuchunguza
  3. Matokeo ya tume zote mbili yakathibitisha tunaibiwa.
  4. Ukakasirika sana na kuahidi kamwe makinikia hayataondoka na kuanzia sasa yatachenjuliwa nchini.
  5. TRA wakaleta tax bill inayotosha kumnunulia Noah kila Mtanzania.
  6. Baba wa mwizi wetu akatua nchini kwa mazungumzo na kuahidi kishika uchumba cha dola milioni 300
  7. Mazungumzo ya tax bill yakaanza
  8. Mazungumzo yakaisha mkakubaliana kusamehe deni lote!.
  9. Pia makinikia yakaruhusiwa kuendelea kutoka huku hatujui kilichomo
  10. Hakuna issue yoyote ya kuchanjua makinikia nchini!.
Mwacheni baba wa watu apumzike kwa amani huko peponi alipo.

Hii ni hatari kuliko hatari yenyewe...

Unajua ukiwa unafanya jambo hutakiwi kuwa na mihemko au kukurupuka..

Issue ya makinikia ilikuwa aibu ya nchi
 
Hii ni hatari kuliko hatari yenyewe...

Unajua ukiwa unafanya jambo hutakiwi kuwa na mihemko au kukurupuka..

Issue ya makinikia ilikuwa aibu ya nchi

Usiefahamu mambo utasema hivi.

Ila Ulikua ushujaa usio wa Kawaida kupata walau 16%

Mwizi alikubali yaishe huku akitoa Ofa kadhaa ikiwemo Maabara, Ujenzi wa Barabara 2 , na Pia Kuanza kulipa Kodi stahiki , Kampuni iwe na Ofisi hapa ( Zamani ilikua London)

Ni Vigumu sana kuelewa nini maana ya Majadiliano
 
Mkuu...

Unajua shughuli za migodi zilifungwa kwa karibu mwaka mmoja na miezi kadhaa kwa ajili ya ripoti hii ya kusadikika?

Unajua maelfu ya watu walikaa nyumbani hasa kanda ya ziwa.. Shughuli nyingi za kiuchumi zilisimama.... (multiple effects zilitokea)?

Unajua hata kama ripoti inatengenezwa.. Inatakiwa angalau asilimia 40 iwe na uhalisia? Hivi unajua maana ya kodi sh tril 360 ? Yaani kiufupi tuseme miaka 18 hizo kampuni zimevuna madini zaidi ya tril 5000? Ili sisi tuweze kudai tril 360...
Unajua tusijitoe ufahamu kwa neno UZALENDO.. ambalo lilitumika kijinga wakati huo...

Hiyo asilimia 16 tusingeweza kupata kwa majadiliano mpaka tufunge shughuli za migodi miezi 15....? Unajua Serikali ilipoteza kiasi gani cha PAYE kwa maelfu ya wafanyakazi kukaa nyumbani.?
 
Back
Top Bottom