Ni upumbavu kujadili kabira fulani eti ni bora au ni duni zaidi ya kabila fulani ,
Kimsingi huu ni upumabavu,na ni ukabira pia kama sio ubaguzi.
Ni sawa na anae sema lugha fulani ni bora zaidi ya lugha fulani.
Kimsingi hakuna kabila lililo bora zaidi ya jingine na ni sambamba na lugha ,hakuna lugha bora zaidi ya nyingine,sawa na kwa binadamu pi,hakuna alie bora zaidi ya mwingine.
Kila kabira linajitosheleza kwa kadri lilivo,kila kabila lina usitaraabu wake na ushamba wake,kama huwezi kuamini nitajie kabila lako nielezee ubora wake na upungufu wake
Hakuna kinacho jitosheleza chenyewe ,mpwayungu una silika za kike kike sana we jamaa,na kiundani una kiubaguzi fulani na vitabia vya kujimwambafai.
Nimetembea Tanzania nzima na nje ya nchi hii ,kalibia watu wote wa makabira ya Tanzania nimekaa nao na kushirikiana nao latika shughuri mbali mbali za ujenzi wa Taifa.Hakuna kabila bora zaidi ya jingine .