mwananyaso
JF-Expert Member
- Feb 19, 2017
- 2,884
- 3,195
Alipopewa nafasi ya kuzungumza kutoa nasaha zake kuelekea kufungwa kwa mkutano mkuu wa CCM, aliongea mengi ya kuwaasa wanachama kujenga mshikamano, kadhalika alimtia moyo mwenyekiti mpya dhidi ya dhoruba ndani ya chama.
Kauli ambayo napenda kwa aliemuelewa atusaidie ni kwasababu huyo ni mzee wa kiswahili, kama Makamba senior, ambaye ndani ya hizi siku mbili kavulunda sana.
Jakaya Kikwete alisema hivii, CCM ijikite kwenye mafunzo ya wanachama wake, kwa sababu chaguzi zinaleta viongozi wapya kadhalika wazamani kupigwa msasa wa kukijua chama.
Akasema wakukisaidia chama kwenye mafunzo yupo Mzee Yusuf Makamba, Mzee Mkama, na alipomfikia Bashiru Ali akasema sijui kama na yeye atakuwa tayari, Bashiru alisimama kwa unyeyekevu kuashiria kukubali.
KWANINI KWA BASHIRU ALI KASITA, NA KUMUULIZA KAMA YUKO TAYARI?.
Akili yangu inaniambia ndani ya CCM kuna fukuto kali sana, ishara ni kura walizopata watoto pendwa, zinatia shaka