Kwenu wanaume ...Hii imekaaje ?


Ni kweli uliyosema chimunguru
Je mnajua kama nyinyi wanaume ndo msingi wa family
na Je mnajua kama nyie mkituwekea Security tutaheshimika na familia zenu
Lakini pale mnapojitenga na sisi ndo mwanzo wa kufikia mama mkwe anasema lolote juu ya mkwewe na mbaya zaidi kama mawifi wapo ndo wanazidi kupigilia msumari
Hatari
 
Mwanaume mjinga, ametudhalilisha agh!

Mama si akae na mume wake anataka nini kwenye ndoa za mwanaye

Kuna mipaka kwenye kila kitu, haki za mama kwa mtoto inaishia kwenye mahusiano mema, kusaidiana na kama hayo

Lakini kufikia kuingilia ndoa, kushauri kwa kejeli na dharau, anajuaje mambo ya kizazi? atajuta si huyo mwanamke akipata watoto

Kuna kisa kama hicho kiliwahi kutokea baadaye mwanamke akajaliwa watoto wawili wawili..mama mkwe akaanza kuona aibu..shame on her! zaidi huyo mtoto wake ni pre-mature na mpuuzi
 

Thanks Tumaini hii habari imeniumiza na kuniboa sana mie
 
Mwanaume hawi mwanaume kwa kuwa na pesa nyingi, kwa kuwa na kazi nzuri, kwa kuwa na watoto na mke... anaanza kuwa mwanaume siku atakayomwambia mama yake "hapana". - M. M. Original

Of course.. you can quote me
 

thanks Mwanakijiji hapo pana ukweli wote labda huyu anaogopa akitishiwa kupewa radhi ..
 
Huwenda mwanaume ndo kasuka hou mpango mzima haiwezekani umjibu mwenzio meseji sent- manyanyaso mengine? FL1 Huyo rafiki yako wameshakwenda kucheck hospital yeye na mumewe kama hawana tatizo lolote?

MJ1 nimewaza kama wewe hili deal limechorwa na huyo baba na ndo maana mkewe alipomwuliza akamjibu hivyo,imeniuma sana,hii ni ile type ya mwanaume ambae hawezi kuamua chochote kwenye ndoa yake mpaka aamuliwe na ndugu zake,namwonea huruma sana huyo dada,na mpaka mama mkwe anathubutu kumwambia kuwa kama anataka kuondoka njia iko wazi it means tayari wameshamtafutia mtoto wao mtu mwingine wa kuishi nae,je huyo jamaa alishawahi kwenda kwenye vipimo? na je wamehakikisha kuwa huyo dada ndo mwenye tatizo? maana unaweza kuta mwanaume ndo mwenye tatizo lakini anaetupiwa lawama ni dada wa watu.
Chonde chonde tusiruhusu wazazi wetu watuingilie kwenye ndoa zetu kihivyo,FL1 nampa pole sana huyo rafiki yako na nimejisikia vibaya sana kwa jinsi ambavyo mume wake anashindwa kumtetea mkewe badala yake nae anashiriki katika vitendo vya kumwumiza moyo mke wake.
 
Huyo mama itakapo kuja kujulikana mwanae risasi zake hazifanyi kazi sijui atasemaje?
 
kwamba ni risasi za plastic au zinatoka na gamba lake?????
tehe tehe teheheeeeeeeeeee

Hehehehe risasi zimekuwa butu hazipigi zimeota kutu kabisa sielewi mama na mwanawe wataficha wapi nyuso zao.
 
Na trend mpya siku hizi wanaume wakikorofishana na wake zao wanarudi kwa mama zaoooo! Wonders will never cease!
 
Mwanamme hana MSIMAMO na ndoa yake, na akiendelea hivyo, ndoa itasambaratika very soon. Je huyo mwanamme ana uhakika gani kuwa yeye si tatizo la kukosa mtoto? Tusiwahukumu wanawake wakati wanamme hawajapima na kuwa na uhakika wa kusema Meseji sendi...
 

Naye angempa kubwa tu huyo mama mkwe ili watoke bila bila. Wakati mwingine usipokuwa strong hawa ndugu wanaweza kukuharibia ndoa, na especially ukiwa na mume weak kama huyo anayeendeshwa na mama yake.Mwambie ajisimamie.
 


Inaweza kuwa huyo mwanaume ndo hana uwezo wakumpa mimba mkewe
 
Ndivyo mijanume mingi ya Afrika ilivyo,haina msimamo na inafikiri ndoa ni kuwa na watoto hivyo mtoto akikosekana basi lawama kwa mwanamke...ni wanaume wachache sana husimama upande wa wake zao...Afrika ukiolewa maana yake na ndugu wa mume nao wanakuoa..wanakuwa na haki ya kuingilia mambo yenu...shit!!!
 
Ndo maana kila wakati nasema watu wengi wanaoana for all wrong reasons...kuna watu wanaoana kwa umri umefika,wengine pressure toka kwa wazazi,wengine kwa kuwa washkaji wake washaoa naye anaamua kuoa,wengine ili wapate watoto,wengine financial situations,etc etc ila mi nadhani sababu pekee ya kuoa ilitakiwa iwe mapenzi (love). Ivi unadhani uyo dada angekuwa ameolewa na mtu wanayependana angeambiwa ivyo?
Lakini mimi simlaumu sana huyo mume kwa kuwa inawezekana alishaweka wazi sababu yake ya kuoa ni kupata watoto na uyo mdada akakubaliana nae...mkataba ni mkataba tu,mdada amevunja kipengele cha mkataba alafu analalamika?NI HAYO TU!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…