IronBroom
JF-Expert Member
- Jun 12, 2008
- 521
- 36
Rafiki yangu mmoja kanijia jana akiwa mwingi wa mawazo na majonzi tele
Kisa nini..Ni mwaka wa tatu sasa ameolewa hana mtoto ,Mama mkwe kapiga simu saa tano usiku kwa mwanae wakiwa wamelala
anauliza mkeo yuko hapo ? jamaa kasema ndio ..basi akaambiwa weka loud spika ili huyo anayejiita mkeo apate vidonge vyake
Mama mkwe bila haya kaanza kuporomosha mvua ya maneno akilalamika kama hajaolewa kuja kumchuna mtoto wao wamemsomesha ili awatunze wao na sisi yeye mke mgumba ..
Mbaya zaidi anamwambia ..hajaolewa ili awe sanamu ndani ya nyumba ..la sivyo wangenunua sanamu wakaweka ndani wanachotaka amzalie watoto kama hawezi njia iko wazi aondoke ..!
Mke kulalamika kwa mmewe ..
Mme anamjibu hii ni message send ..
Wanaume kwa nn mnaruhusu ndoa iingliwe na ndugu mke anyanyaswe kiivyo ?
kwa nini msitoe suport ili mke awe na uwezo wa kujitetea?
shock!!!!
FL
FL1,
Wengine ni suruali tuu...kuruhusu ndoa kuingilkiwa kiasi hiki...hamna mme hapo.