Orosso
JF-Expert Member
- Aug 3, 2022
- 931
- 2,262
Habari zenu wana jamvi.
Nimeshuka jamvini na swali kama linavojieleza katika kichwa cha habari.
Lengo kuu ni kuona namna gani michango ya wanajamvi inaweza saidia kufikisha ujumbe kwa wahusika na kufanya marekebisho katika dosari zinazojitokeza kila siku katika kutimiza majukum yao.
Tunafaham kuwa moja ya majukumu ya msingi ya sekretarieti ya ajira (PSRS) ni kusimamia na kuratibu mchakato mzima wa upatikanaji wa ajira kwa sekta ya umma. Kutimiza lengo hili, uwajibikaji na uwazi vinahitajika kwa kiwango cha juu mnoo kuhakikisha kunakuwepo na usawa kwa washindani katika kupigania fursa hizo.
Kwa muda mrefu kumekuwepo na malalamiko yanayoashiria kupungua kwa kiwango cha uwajibikaji na uwazi hasa linapokuja swala la watu kuitwa kazini. Malalamiko haya yanazidi kushika kasi hasa kipindi hiki ambacho kunashuhudiwa msululu wa saili zinazoendelea kujaza nafasi zilizo wazi serikalini.
Tumeshuhudia pia, matangazo ya waliofanikiwa kuitwa kuhudhuria sahili hizo kwa maana, sahili za mchujo na mahojiano yakitoka kupitia tovuti ya utumishi.
Changamoto inakuja panapohitajika uwazi zaidi namna inayofaa kutangaza majina ya walioshinda sahili hizo na hivyo kuitwa kazini. Hapa pamekua na changamoto hasa kwa siku hizi za karibuni.
Kwa siku hizi za karibuni tumeshuhudia taasisi za kiserikali kupitia tovuti zao, zikiwa za kwanza kutangaza majina ya watu walioshinda sahili na kuitwa kazini, je, kwanini katika hatua hii ya tatu ndo taasisi hizi ziwe zinatangulia kutangaza washindi na kuita watu kazinin? Ipi nafasi ya sekretarieti ya ajira katika kuwajibika na uwazi katika hatua hii muhimu katika mchakato wa kutoa ajira sekta ya umma nchini?
Kuthibitisha hili, Chuo kikuu huria kilitangulia kutoa majina ya walioshinda sahili na kuita watu kazini katika tovuti yake ya chuo, ndipo baadae sekretarieti ya ajira ikafuatia. Hali kama hiyo ikajirudia katika tovuti ya chuo kikuu Mzumbe, walitoa majina ya walioshinda sahili na kuitwa kazini, ilhali mpaka muda huu hakuna tangazo katika tovuti ya sekretarieti ya ajira. Nini chanzo cha mkanganyiko huu na nini itakua hatma ya tabia hii kwa sahili zote zinazoendelea hasa katika hatua ya mwisho, hatua ya "placement"?
Ni wazi tunahitaji kuona uwajibikaji na uwazi wa hali ya juu katika hatua zote za mchakato wa upatikanaji wa ajira, kwa maana kama ambavyo tangazo la kazi linavotolewa katika tovuti ya sekretarieti, kuita watu watu kwa usahili, pia, tunaomba majina ya sahili hizi zitolewe kupitia tovuti ya sekretariati.
Tunahimiza uwajibikaji na uwazi ili kuweza kuweka usawa na kuondoa malalamiko dhidi ya namna mchakato wa upatikanaji ajira unavohitimishwa.
Ahsanteni.