Kwenda south africa kwa basi

Kwenda south africa kwa basi

Mkataa kwao ni mtumwa
Naona ndugu yetu anapenda maisha ya kichokoraa kweny nchi ya watu bt kama wasemvyo wahenga mtto akililia wembe we mpe
 
Unapanda basi la taqwa mpaka harare...ukifika hapo nenda Tanzanian club utakuta kuna wabongo wenzako kibao..ila usimwani mtu hapo maana wengine sio waaminifu...then muone mangi yupo hapo anauza nyama choma mueleze.....

Angalizo: kuna mtoto wa kitanga alikuwa kama wewe hivyo anataka kwenda Johannesburg ila siku chache alirudi harare analia saaaana...sijui yalimkuta yapi uko....akawa anaombaomba pale ili apate japo nauli ya kurudi....
 
mimi nataka kwenda kutembea tu,jburgh na pretoria,kwa muda usiozidi wiki mbili tu,naombeni ushauri niwe na kiasi gani cha fedha kwa maisha ya wastani?
 
Unaenda kuangalia kaburi la mandela au?kaza ndala maisha yako popote na c s.afrika
 
Wadau nimepanga kwenda South Africa kwa basi kutafuta maisha huko naona Bongo hapaelewek maana nimefanya biashara ya TAXI naona inabana BODA BODA, BAJAJ huku TRA na MANISPAA wanabana kwa sasa nimejichanga nina 1000 USD natumaini zitanisaidia huko niendako. Msaada ninaoomba ni kuwa nipande basi za wapi kufika South Africa?
Kama una professional ya kuuza unga na ujambazi nenda tu utapiga pesa ndefu, lakini kama huyawezi hayo nakushauri baki nyumbani endelea kuchakalika Mungu atakuonesha njia na uwepo wake. Naijuwa South Africa vilivyo kwa maisha ya kufanya kazi na mshahara wa kila ijumaa na jumatatu pesa imekwisha hata ukae miaka 100 huwezi kutengeneza pesa ya kurudi nayo nyumbani.

South African ni nchi nzuri sana ya kwenda kwa matembezi na utaenjoy.
 
Nakushauri hizo HeLa ujipange hapa hapa! Wenzio walioko kule wanatamani kurudi home, utaishi kama swara kwenye pori la simba! Kama unataka kwenda sikuzuii, kwanza usiingie SA na Dollar, nunu Rand hapa, utapata shida hiyo nchi haithamini Dollar ukienda bank maswari kibao mpaka address unakoishi, panda tawfiq la zimbabwe mpaka Harare, utafika jioni usiku kuna mabasi ya moja kwa moja mpaka Johannesburg.


Mkuu hapa umempoteza, ilikuwa utaje route ili akizungukaaaa, akigeuka yupo kahama, akigeuka boda ya Kyela akifika Tunduma $1,000 inakuwa ishaisha badala la kupoteza muda kwenda huko!

Ni hayo tu!
 
Komaa mkuu hiyo hela km una Akili mbona unaizalisha na unaweza kutoka tu km una malengo lakini.
 
Back
Top Bottom