Kwenda south africa kwa basi

Kwenda south africa kwa basi

SSH2025_2030

JF-Expert Member
Joined
Jul 9, 2012
Posts
9,661
Reaction score
9,814
Wadau nimepanga kwenda South Africa kwa basi kutafuta maisha huko naona Bongo hapaelewek maana nimefanya biashara ya TAXI naona inabana BODA BODA, BAJAJ huku TRA na MANISPAA wanabana kwa sasa nimejichanga nina 1000 USD natumaini zitanisaidia huko niendako. Msaada ninaoomba ni kuwa nipande basi za wapi kufika South Africa?
 
Wewe unataka kwenda kuteseka,tumia hiyo hela kujiajiri.
 
Wadau nimepanga kwenda South Africa kwa basi kutafuta maisha huko naona Bongo hapaelewek maana nimefanya biashara ya TAXI naona inabana BODA BODA, BAJAJ huku TRA na MANISPAA wanabana kwa sasa nimejichanga nina 1000 USD natumaini zitanisaidia huko niendako. Msaada ninaoomba ni kuwa nipande basi za wapi kufika South Africa?

Dola 1,000 ununue BODABODA mpe kijana akuletee hesabu; wewe endelea na udereva taxi wako. Unakokimbilia ni moto mkali zaidi. Usijidanganye kwa story za vijiwe Mkuu
 
Wadau nimepanga kwenda South Africa kwa basi kutafuta maisha huko naona Bongo hapaelewek maana nimefanya biashara ya TAXI naona inabana BODA BODA, BAJAJ huku TRA na MANISPAA wanabana kwa sasa nimejichanga nina 1000 USD natumaini zitanisaidia huko niendako. Msaada ninaoomba ni kuwa nipande basi za wapi kufika South Africa?

Nakushauri hizo HeLa ujipange hapa hapa! Wenzio walioko kule wanatamani kurudi home, utaishi kama swara kwenye pori la simba! Kama unataka kwenda sikuzuii, kwanza usiingie SA na Dollar, nunu Rand hapa, utapata shida hiyo nchi haithamini Dollar ukienda bank maswari kibao mpaka address unakoishi, panda tawfiq la zimbabwe mpaka Harare, utafika jioni usiku kuna mabasi ya moja kwa moja mpaka Johannesburg.
 
kwan SAUZ kuna maziwa na asali?...au huko hakuna TRA?
 
Ukifika utupe kilisha nyuma(feedback) all the best mkuu.
 
bongo hapa unaona tabu na umeshaweza kukusanya dola 1000 kwel ni tabu? Jipange vzr usikate tamaa anza biashara nyngne huku ukiendelea na hyo ilyokuwesha kupata hzo dolal,nchi za watu huna mwnyej huna pa kuanzia utaishia jela km si kuchezea shaba.
 
Hizo hela peleka kwa mzee wa transfoma aziombee uwe tajiri
 
Direction hii hapa mkuu..

Nenda Ubungo tafuta office za Falcon au Taqwa (chagua moja) waambie unaenda Lusaka..

Hilo bac litakufikisha mpak Lusaka, ukifika Lusaka shuka (basi linaenda Zimbabwe)

Ukishuka stend (wenyewe wanapaita INTER CITY ni kama uionavyo Ubungo Terminal yetu) tafuta office za Shalom Bus, waambie unaenda JOBURG naul ni 450000kwacha..

Utapanda bas hilo litakufikisha JOBURG..

Maelezo mengine ni pm maana hapo kuna mambo ya kugonga passport sijakueleza na ishu nyingine..
 
Hiyo hela hadi ufike huko SA itakuwa ishapungua kama nusu hivi...
 
Badirisha hizo dola kuwa Rand, panda basi hadi Tunduma, hakikisha unapofika Tunduma uwe na Tsh laki 1 ambayo utaibadirisha kuwa Kwacha, panda basi kutoka Nakonde kwenda Lusaka, panda basi kutoka Lusaka kwenda Jhb ni Rand 700+-. Kama utaingia South na R5,000. na mwenyeji wako akikushauri vizuri, mambo yanaweza kuwa mazuri tu. Mwisho kaa ukijua South maisha magumu usipime, ila ni chuo kizuri cha maisha. Karibu sana.
 
wasiliana na dk.isaac maro wa clauds fm njia panda atakuunganisha na mtu mmoja anaitwa kinega...utaenda sauzi afrika safi kabisa..
 
kwenda south africa kwa 1000 usd? mbona majanga mkuu!

hio pesa nadhani ni kwa ajili ya meals and accomodation kwa wiki nne.

baada ya hapo utarudi jf kuomba nauli nakwambia.
 
Duh watu tumejiajiri kwa dola mia tano wewe una buku umeshindwa kuendeleza libeneke bongo kwa dola buku,kwa kweli pole sana.
 
SA!!!!!?? bora baki kwenu ulime tu
Tafuta pesa mwanaume hutakiwi kukataa tamaa mapema hivyo,huko utabaguliwa mpaka ukome
Tafuta pesa siku ukipata utaenda kutembea nchi unayotaka
 
Usijaribu kwenda south Africa utajuta kuzaliwa ongeza bidii kwenye kazi iyo pesa iongeze kwenye mzunguko wa utafutsji soon utakuwa success
And never loose hope
 
Back
Top Bottom