Kwenda benki CRDB ni mateso, nimekoma

Justine Marack

JF-Expert Member
Jul 31, 2014
228
693
Leo nimekwenda Benki CRDB kuchukua pesa yangu mwenyewe, lakini nimeteseka kama vile nimeenda kuomba pesa Bure.

Foleni watu 100 muhudumu Mmoja tu. Wengine movement haziishi, mara atoke mara arudi anageuzageuza makaratasi.

Watu wamenuna mpaka saa kumi Bado Kuna zaidi ya watu 90 ambao nyuso zimekosa matumaini.

Mbaya zaidi linakuja jamaa na misevu linavunja foleni mpaka mbele dirishani wanaanza kupiga stori wanakenua nusu saa.

Naapa sirudii tena CRDB Bora nizichimbie chini. Bado makato yanauma na nyie mnatuvuruga.
 

Dabil

JF-Expert Member
Sep 30, 2021
4,040
9,038
Komesha ni pale Mlimani city..
Lazima upoteze masaa 2 mpaka 3...
Kuna vitu lazima uende bank.
Niwakumbushe wadau siyo kila kitu Sim banking au ATM inaweza kufanya...
Mfano online payment kwa visa card kuregister lazima uende kwao link ya kwenye website ikigoma.
 

Dabil

JF-Expert Member
Sep 30, 2021
4,040
9,038
Huwa naona crdb ya Lumumba wahudumu wapo wengi,na kuna madirisha mengi pia.

Ila CRDB ni kimeo kwenye huduma ukienda bank. Unakuta wateja zaidi ya 100 dirisha moja ndo inakuwa wazi, shame on them. Halafu wahudumu wanavyoringa utadhani ile hela ndo ya kwao.
 

Similar Discussions

16 Reactions
Reply
Top Bottom