Kweli tenda wema nenda zako, usingoje shukurani

Komeo Lachuma

JF-Expert Member
Oct 31, 2014
5,321
11,386
Nipo kwa sister hapa naaangalia angalia michongo ya kazi hapa Town. Tulikuja Mjini kutafuta pesa siyo kuangalia magorofa. Mimi mtoto wa kiume lazima nijitume. Kama matunda yangu yapo basi lazima niyachume.

Kuna siku hapa nliandika namna ambavyo nlimsaidia shemeji kwenye issues zake za ndoa kwa kumwonya sister aheshimu ndoa. Nikategemea shem ataona mchango wangu hapa home maana naona kama huwa ananiona mi kula kulala.

Kumbe napokuwa nmekaa hivi natafakari maisha na jinsi nitakavyokuja kuwa na bonge la Kampuni. Siyo kwamba nakaa bure tu. Ni vile hawezi ona mawazo yangu.

Jana nimemwambia basi angalau anitoe buku 5 za voucher maana bundles nazo zimepanda kinyama na data nliyojiunga inaelekea kuisha. Nlijua kabisa shem kasikia.nina uhakika maana nliongea kwa sauti kubwa tu.

Akanitizama akaondoka akaingia room kwake.hili jambo limenikera sana. Mpaka muda huu namwazia hivi ananionaje mimi? Somutaimu mtu anaweza kukudharau kumbe hakujui tu. Mimi nina mawazo makubwa sana. Si wa yeye kunitizama na kuingia room kwake.

Nikimtizama hata kwenye mkono hajai.nina uwezo wa kumtandika makofi mpaka akalazwa hata week. Kwa nini anifanyie mazarau?na anasahau siku ile nimempambania kwa sister ili apewe tendo la ndoa. So now anapata anasahau juhudi zangu?

Kukaa kwa watu samutaimu kunataka moyo wa uvumilivu sisi wenye hasira tunamwomba sana mola zisije waka kwa watu tukatembeza kipigo tuonekane wabaya. Kweli baniani mbaya kiatu chake dawa. Nimewaza jana suala hili hawa binadamu kwa nini wanasahau kwa haraka wema?

Haya yote ni maisha. Kuna siku yataisha. Leo hii mimi wa kufanyiwa hivi kweli? Binadamu tupendane na kuheshimiana.
 
Nipo kwa sister hapa naaangalia angalia michongo ya kazi hapa Town. Tulikuja Mjini kutafuta pesa siyo kuangalia magorofa. Mimi mtoto wa kiume lazima nijitume. Kama matunda yangu yapo basi lazima niyachume.
Wewe huna akili kabisa,tafuta kwako hapo sio kwako
 
  • Thanks
Reactions: THT
Hivii unayoandika ni kweli auu alafu unawesaje mwambia dada ako ampe papuchi mumewe
 
Samutaimu uwe unaweka picha ya vitu hivyo vikubwa unavyowaza...
 
Wewe kweli hamnazo.....piga kazi katafute hiyo elfu tano ya vocha....hata ningekuwa mimi siwez kukupa elfu tano ya vocha....wakati ndani tunahitaji tule....pambana mtoto wa kiume
 

Similar Discussions

3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom