Tenda wema uende zako usingoje shukrani

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,331
33,142
TENDA WEMA UENDE ZAKO USINGOJE SHUKRANI.

Daktari aliingia hospitalini kwa haraka sana baada ya kuitwa kwa shughuli ya Upasuaji wa haraka, alipokea simu haraka, na kuvaa nguo za kazi na kuelekea moja kwa moja kwenye chumba cha upasuaji.

Wakati akielekea kwenye chumba cha upasuaji alimkuta Baba wa mtoto anazunguka huku na huku karibu na chumba huku akimsubiria Daktari. Baada ya kumuona tu, Baba mtoto akapayuka: Kwanini umechelewa kuja?

Hufahamu kama maisha ya Mtoto wangu yapo hatarini? Hivi unayajua majukumu yako?

Yule Daktari alitabasamu na kumwambia; Samahani sana, Sikuwa Karibu na Hospitali na nimejitahidi kuja kwa haraka sana baada ya kupokea simu kutoka hapa hospitalini Na kwakuwa nimeshafika ningekuomba upunguze Jaziba na hasira ili nifanye shughuli yangu

Punguza hasira?! Hivi ingekuwaje Mwanao ndiye angekuwa chumba cha upasuaji sasa hivi, ungeweza kupunguza hasira? Kama mwanao ndie anakufa sasa hivi ungefanyaje?Yule Baba aliongea kwa hasira sana.

Yule Daktari alitabasamu tena na kumjibu ningesema kama vitabu vinavotuambia tuseme, tumeumbwa kwa vumbi na tutaondoka kwa Vumbi, Jina la Mwenyezi Mungu Litukuzwe Daktari hawezi kurefusha maisha ya

Binadamu. Nenda katulie na umuombee mwanao, sisi tutajitahidi kadri kwa uwezo tulionao kwa Baraka za Mwenyeezi .Mungu
Kutoa Ushauri kwa vitu visivyo wahusu ni rahisi sana Alinong;ona Yule Baba mwenye motto.
Upasuaji ulifanyika kwa Masaa kadhaa mara tu baada ya kumalizika Daktari alitoka akiwa anafuraha, Asante

Mungu! Mtoto wako tumeweza kumponya! Kama una swali lolote utamuuliza Nurse!! Bila ya kumsikia Baba Mwenye mtoto kujibu chochote aliondoka kwa haraka kwenye eneo la upasuaji.
Kwa nini ni Mkorofi sana huyu Daktari? Yaani Hawezi hata kusubiri kidogo nimuulize maendeleo ya Mwanangu alimjadili akiwa na nurse baada ya Daktari kuondoka.

Nurse akamjibu, huku akitokwa na machozi: Mtoto wake alifariki jana kwenye ajari ya gari, alikuwa katika mazishi ya Mtoto wake wakati tunampigia simu aje Hospitali kwa ajili ya Upasuaji wa Mtoto wako. Amefanikiwa kuyaokoa

maisha ya Mtoto wako, kwahiyo ameondoka kuwahi mazishi ya mtoto wake.

HEKIMA:


USI MUHUKUMU MTU YEYOTE…. SABABU HUYAJUI MAISHA YAO NA KIPI KILICHO


WAKUTA KWENYE MAISHA YAO.

TENDA WEMA KADRI UWEZAVYO BILA YA KUJALI HALI ULIYONAYO
 
TENDA WEMA UENDE ZAKO USINGOJE SHUKRANI.

Daktari aliingia hospitalini kwa haraka sana baada ya kuitwa kwa shughuli ya Upasuaji wa haraka, alipokea simu haraka, na kuvaa nguo za kazi na kuelekea moja kwa moja kwenye chumba cha upasuaji.


Wakati akielekea kwenye chumba cha upasuaji alimkuta Baba wa mtoto anazunguka huku na huku karibu na chumba huku akimsubiria Daktari. Baada ya kumuona tu, Baba mtoto akapayuka: " Kwanini umechelewa kuja?

Hufahamu kama maisha ya Mtoto wangu yapo hatarini? Hivi unayajua majukumu yako?"

Yule Daktari alitabasamu na kumwambia: " Samahani sana, Sikuwa Karibu na Hospitali na nimejitahidi kuja kwa haraka sana baada ya kupokea simu kutoka hapa hospitalini….. Na kwakuwa nimeshafika ningekuomba upunguze Jaziba na hasira ili nifanye shughuli yangu"

" Punguza hasira?! Hivi ingekuwaje Mwanao ndiye angekuwa chumba cha upasuaji sasa hivi, ungeweza kupunguza hasira? Kama mwanao ndie anakufa sasa hivi ungefanyaje?"Yule Baba aliongea kwa hasira sana.

Yule Daktari alitabasamu tena na kumjibu: " ningesema kama vitabu vinavotuambia tuseme, " tumeumbwa kwa vumbi na tutaondoka kwa Vumbi, Jina la Mwenyezi Mungu Litukuzwe". Daktari hawezi kurefusha maisha ya

Binadamu. Nenda katulie na umuombee mwanao, sisi tutajitahidi kadri kwa uwezo tulionao kwa Baraka za M.Mungu"
" Kutoa Ushauri kwa vitu visivyo wahusu ni rahisi sana" Alinong'ona Yule Baba mwenye motto.
Upasuaji ulifanyika kwa Masaa kadhaa mara tu baada ya kumalizika Daktari alitoka akiwa anafuraha, " Asante

Mungu! Mtoto wako tumeweza kumponya!" Kama una swali lolote utamuuliza Nurse!!" Bila ya kumsikia Baba Mwenye mtoto kujibu chochote aliondoka kwa haraka kwenye eneo la upasuaji.
" Kwa nini ni Mkorofi sana huyu Daktari? Yaani Hawezi hata kusubiri kidogo nimuulize maendeleo ya Mwanangu" alimjadili akiwa na nurse baada ya Daktari kuondoka.

Nurse akamjibu, huku akitokwa na machozi: " Mtoto wake alifariki jana kwenye ajari ya gari, alikuwa katika mazishi ya Mtoto wake wakati tunampigia simu aje Hospitali kwa ajili ya Upasuaji wa Mtoto wako. Amefanikiwa kuyaokoa

maisha ya Mtoto wako, kwahiyo ameondoka kuwahi mazishi ya mtoto wake."

HEKIMA:

"USI MUHUKUMU MTU YEYOTE…. SABABU HUYAJUI MAISHA YAO NA KIPI KILICHO WAKUTA KWENYE MAISHA YAO.
" TENDA WEMA KADRI UWEZAVYO BILA YA KUJALI HALI ULIYONAYO"


haya mafundisho mazuri sana kwa afya kati yetu na majiran zetu, ubarikiwe mkuu
 

Kwa hii dunia tunayoishi kumpata daktari mwenye utu wa kiwango hicho ni ndoto labda kwa majuu.

Kwa bongo ni kitu cha kufikirika tu.
 
Kwa hakika baadhi ya dhana ni ovu kubwa !! Usiweke dhana bila kupata dalili za kuhukumu.....! Ahsante kwa fundisho Dr.Mz"mkavu Ubarikiwe
 
Back
Top Bottom