''Tenda Wema Nenda Zako Usingoje Shukurani'': Kumbukumbu za Kanali Ayubu Simba

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,925
30,273
‘’TENDA WEMA NENDA ZAKO USINGOJE SHUKURANI’’: KUMBUKUMBU ZA KANALI AYUBU SIMBA

Rafiki na ndugu yangu Hamisi Hababi leo asubuhi kaniletea kitabu cha maisha ya Kanali Ayubu Simba.

Hababi alipata siku moja katika mazungumzo yetu kuniambia kuwa maarifa yapo katika vitabu.

Siku hizi nimekuwa na tabia nikikipata kitabu hukisoma mwanzo kisha huwaeleza watu yale niliyokutananao mwanzo tu wa kitabu kisha nikimaliza kukisoma ndiyo nakifanyia pitio yaani ''book review.''

Sijasubiri nimekianza kitabu na mwanzo tu wa kitabu nimepambana na jambo ambalo si la kawaida.

Utangulizi wa kitabu umeandikwa na binti yake Kanali Ayubu Simba, Dkt. Mayasa Simba ambae ndiye khasa mwandishi wa kumbukumbu hii ya baba yake.

Dkt. Mayasa inaelekea ndiye aliyeshika kalamu akawa anamskikiliza baba yake.

Dkt. Mayasa ni daktari wa binadamu na ni mmoja kati ya watu ndani ya familia ya Kanali Simba waliokuwa wakimtia hima aandike maisha yake ili jamii inufaike na uzoefu wake katika kutumika taifa lake.

Mwanzo tu katika utangulizi nimekutana na majina na majemadari hodari wa kupanga mbinu za mapigano katika medani ya vita.

Hapa nikajua hakika namsoma mwanajeshi.

Mwanzo kabisa Kanali Simba anamtaja, Sheikh Omar Mukhtar mzalendo wa Libya aliyejulikana kwa jina la ‘’Simba wa Jangwani,’’ aliyepigana na Wataliani akijitahidi kuwatoa nchini kwake.

Kitabu kinamtaja Jenerali Von Nguyen Giap na ushujaa wake dhidi ya Wamarekani wakati wa Vita Vya Vietnam.

Kanali Ayubu Simba anaeleza katika kumbukumbu zake kuwa alipokwenda Vietnam aliomba fursa akutane na shujaa huyu na walikutana.

Kanali Simba kanishangaza kwa jinsi alivyoingia katika kapu la majemadari wakubwa ulimwenguni na kutoka na majina ambayo mengine dunia haipendi kukumbushwa majina yao mfano wa Benito Musolini, Adolf Hitler lakini hapo hapo amewataja pamoja na hawa mDedan Kimathi kiongozi wa Mau Mau na majemadari wa mataifa makubwa duniani kama Field Marshall Benard Law Montgomery.

Kanali Simba kawataja wanasiasa Waafrika waliopigania uhuru wa nchi zao mfano wa Nelson Mandela na Oliver Tambo kwa kuwataja wachache.

Lakini Kanali Simba kanishangaza kupita kiasi.

Kanali Ayubu Simba kaweka jina la Kleist Sykes katika orodha ya wazalendo walipigania uhuru wa Tanganyika.

Hili si jambo la kawaida.
Kanali Simba kanishtua.

Anasema yeye alikuwa jasuji wa serikali pamoja na kuwa mwanajeshi.
Waandishi waliopita katika ujasusi hakika wanaponyanyua kalamu kaa vizuri.

Huwa na mengi ambayo hayakupata kufahamika.
Kitabu hiki sina shaka kina mengi ya kusisimua.

328681850_507485521558762_3181572765193302462_n.jpg
 
Wadiz,
Kanali Ayubu Simba anasema katika kumbukumbu zake kuwa yeye alikuwa kachero wa serikali.

Hii nimependa.
Mwanajeshi na kachero.
Hio nzuri sana, TISS wengi ni military personnel, japo with time kwa sasa wale scout na UVCCM pia wakapewa U TISS ni aibu sana
 
‘’TENDA WEMA NENDA ZAKO USINGOJE SHUKURANI’’: KUMBUKUMBU ZA KANALI AYUBU SIMBA

Rafiki na ndugu yangu Hamisi Hababi leo asubuhi kaniletea kitabu cha maisha ya Kanali Ayubu Simba.

Hababi alipata siku moja katika mazungumzo yetu kuniambia kuwa maarifa yapo katika vitabu.

Siku hizi nimekuwa na tabia nikikipata kitabu hukisoma mwanzo kisha huwaeleza watu yale niliyokutananao mwanzo tu wa kitabu kisha nikimaliza kukisoma ndiyo nakifanyia pitio yaani ''book review.''

Sijasubiri nimekianza kitabu na mwanzo tu wa kitabu nimepambana na jambo ambalo si la kawaida.

Utangulizi wa kitabu umeandikwa na binti yake Kanali Ayubu Simba, Dkt. Mayasa Simba ambae ndiye khasa mwandishi wa kumbukumbu hii ya baba yake.

Dkt. Mayasa inaelekea ndiye aliyeshika kalamu akawa anamskikiliza baba yake.

Dkt. Mayasa ni daktari wa binadamu na ni mmoja kati ya watu ndani ya familia ya Kanali Simba waliokuwa wakimtia hima aandike maisha yake ili jamii inufaike na uzoefu wake katika kutumika taifa lake.

Mwanzo tu katika utangulizi nimekutana na majina na majemadari hodari wa kupanga mbinu za mapigano katika medani ya vita.

Hapa nikajua hakika namsoma mwanajeshi.

Mwanzo kabisa Kanali Simba anamtaja, Sheikh Omar Mukhtar mzalendo wa Libya aliyejulikana kwa jina la ‘’Simba wa Jangwani,’’ aliyepigana na Wataliani akijitahidi kuwatoa nchini kwake.

Kitabu kinamtaja Jenerali Von Nguyen Giap na ushujaa wake dhidi ya Wamarekani wakati wa Vita Vya Vietnam.

Kanali Ayubu Simba anaeleza katika kumbukumbu zake kuwa alipokwenda Vietnam aliomba fursa akutane na shujaa huyu na walikutana.

Kanali Simba kanishangaza kwa jinsi alivyoingia katika kapu la majemadari wakubwa ulimwenguni na kutoka na majina ambayo mengine dunia haipendi kukumbushwa majina yao mfano wa Benito Musolini, Adolf Hitler lakini hapo hapo amewataja pamoja na hawa mDedan Kimathi kiongozi wa Mau Mau na majemadari wa mataifa makubwa duniani kama Field Marshall Benard Law Montgomery.

Kanali Simba kawataja wanasiasa Waafrika waliopigania uhuru wa nchi zao mfano wa Nelson Mandela na Oliver Tambo kwa kuwataja wachache.

Lakini Kanali Simba kanishangaza kupita kiasi.

Kanali Ayubu Simba kaweka jina la Kleist Sykes katika orodha ya wazalendo walipigania uhuru wa Tanganyika.

Hili si jambo la kawaida.
Kanali Simba kanishtua.

Anasema yeye alikuwa jasuji wa serikali pamoja na kuwa mwanajeshi.
Waandishi waliopita katika ujasusi hakika wanaponyanyua kalamu kaa vizuri.

Huwa na mengi ambayo hayakupata kufahamika.
Kitabu hiki sina shaka kina mengi ya kusisimua.

328681850_507485521558762_3181572765193302462_n.jpg
Hawa ndiyo vijana wa Nyerere ambao hawakulishwa wala kumeza fitina ya udini na ukabila
 
Hivi bado yuko hai huyu Kanali?
 
Back
Top Bottom