Kweli Tanzania Daima ni Mdomo wa mafisadi

mudavadi

Member
Apr 19, 2011
53
14
Asubuhi hii nilikuwa nasoma gazeti la Tanzania Daima toleo la leo tarehe 15 Juni, 2011, ambalo limeripoti kwamba Lowassa anarejea leo kutoka Nigeria ambako gazeti hili limeripoti kwamba alikwenda kuhudhuria sherehe ya kuzaliwa kwa Nabii Joshua. Taarifa hiyo ilitoa pia sifa za Nabii huyo kuhusiana na uponyaji wake, utajiri wake na ukubwa na umaarufu wa kanisa lake duniani kote.

Habari hii kwa kiasi kikubwa ilikuwa na nia ya ku-pre-empty habari iliyochapishwa katika toleo la leo la Mwanahalisi ambalo limechambua kwa kiasi kikubwa kile kinachofikiriwa kuwa ni madhumuni ya msafara wa Lowassa na nukuu kutoka kwa watu wake wa karibu. Lilirejea pia mawasiliano kati ya Beatrice Shellukindo na Pindi Chana kuhusu nguvu na dhamira ya Lowassa na maoni ya nabii Joshua kuhusu uwezekano wa Lowassa kuwa rais wa nchi hii 2015.

Kwa muelekeo huu, Tanzania Daima limeendelea kuthibitisha kwamba sasa hivi gazeti hili lnatumika kama maliwato ya kuwatakasa mafisadi na hasa mapacha hawa watatu na wakati huo huo kuwa ni mdomo wao katika masuala mbali mbali yanayohusiana na tuhuma na dhamira zao kisiasa. Sina shaka huu ni utekelezaji wa mpango wa Kibanda kuwa mpagazi wa mafisadi kuelekea uchaguzi wa 2015.
 
Hizo ni ndoto za abunuasi kwa mafisadi kututawala. Lowasa anaota, hawezi kuupata urais hapa tanzania. Hatuwezi kukubali watanzania kutawaliwa na mafisadi; waliyotutendea yametosha!!!!!!!!!! Kwenye urais wasahau kabisa!!!!!!!!!!!!
 
Mkuu tunashukuru kwa kutujuza ya magazetini asubuhi ya leo. Hata hivyo sijui ni kwa nini imekuchukua muda mrefu kujua hili wakati wenye akili zao walilishtukia kitambo.

Swali lililopo ni je, nchi hii inahitaji mtu ambaye anaamini katika uchawi wa ki-nigeria pamoja na miujiza ya kishirikina kuwa mkuu wake wa serikali na dola? Au ameshawishika na andishi la Beatrice Shellukindo? Hivi kesho akiambiwa kwamba ilia aupate urais apeleke viungo vya albino si atakubali kuua ili atimize kiu yake? Tamaa hii iliyopitiliza ndiyo kaburi lake la kisiasa!
 
Hizo ni ndoto za abunuasi kwa mafisadi kututawala. Lowasa anaota, hawezi kuupata urais hapa tanzania. Hatuwezi kukubali watanzania kutawaliwa na mafisadi; waliyotutendea yametosha!!!!!!!!!! Kwenye urais wasahau kabisa!!!!!!!!!!!!

Ndugu yangu inahitaji mtu mwenye akili timamu kujua haya unayoyasema. Lakini wenzetu hawa wanadhani fedha zao chafu zinaweza kununua kila kitu na hata kudai kwamba wao walimuweka Kikwete 2005 na huku wakisahau kwamba walimuunga mkono mtu anayechagulika na aliyekuwa na mvuto kwa wapiga kura wakati huo. Mbona hawakumuunga mkono Balozi Chokala na wakamuwezesha kuwa mgombea kama kweli wao ni king makers.
 
Maskini mfa maji! Sasa huyo Nabii kwa nini hakumkinga ili kashfa hizi zisimuandame? Absalom Kibanda ameamua kujilipua na kufa na jahazi linalozama. Shauri yake mwenyewe.
 
Maskini mfa maji! Sasa huyo Nabii kwa nini hakumkinga ili kashfa hizi zisimuandame? Absalom Kibanda ameamua kujilipua na kufa na jahazi linalozama. Shauri yake mwenyewe.

Hivi Mbowe katika harakati hizi anasimamia wapi na anataka kusema hajui hili na yeye ni mmiliki wa gazeti? Hivi angekuwa hafurahishwi na mwelekeo wa gazeti lake angekaa kimya? What about Chadema?
 
waache wafu wazike wafu wenzao kwani hawatambui kuwa kwao its game over siku nyingi sana.
sitashangaa 'mstaafu' huyu akianza kupiga propaganda kuwa alialikwa kwenda na ni yeye pekee nchi hii aliitwa.
 
Hili ni gazet la uhakika haliwezi kutumiwa na mafisadi.

Unamaanisha Lowassa siyo fisadi? Unajua unachokiongea au umekurupuka mzee. Gazeti ndo lishaandika na habari hizo kwa kweli zinambeba Lowassa. Sasa conclusion ni nini hapo?
 
Hivi Mbowe katika harakati hizi anasimamia wapi na anataka kusema hajui hili na yeye ni mmiliki wa gazeti? Hivi angekuwa hafurahishwi na mwelekeo wa gazeti lake angekaa kimya? What about Chadema?
Acha mawazo mgando ya kiccm mbowe si mwandishi wa habari,na hana chembechembe za kimagamba!Kumiliki chombo cha habari si kuwaingilia wahariri na kuwapangia cha kuandika!!!
 
Asubuhi hii nilikuwa nasoma gazeti la Tanzania Daima toleo la leo tarehe 15 Juni, 2011, ambalo limeripoti kwamba Lowassa anarejea leo kutoka Nigeria ambako gazeti hili limeripoti kwamba alikwenda kuhudhuria sherehe ya kuzaliwa kwa Nabii Joshua. Taarifa hiyo ilitoa pia sifa za Nabii huyo kuhusiana na uponyaji wake, utajiri wake na ukubwa na umaarufu wa kanisa lake duniani kote.

Habari hii kwa kiasi kikubwa ilikuwa na nia ya ku-pre-empty habari iliyochapishwa katika toleo la leo la Mwanahalisi ambalo limechambua kwa kiasi kikubwa kile
kinachofikiriwa kuwa ni madhumuni ya msafara wa Lowassa na nukuu kutoka kwa watu wake wa karibu. Lilirejea pia mawasiliano kati ya Beatrice Shellukindo na Pindi Chana kuhusu nguvu na dhamira ya Lowassa na maoni ya nabii Joshua kuhusu uwezekano wa Lowassa kuwa rais wa nchi hii 2015.

Kwa muelekeo huu, Tanzania Daima limeendelea kuthibitisha kwamba sasa hivi gazeti hili lnatumika kama maliwato ya kuwatakasa mafisadi na hasa mapacha hawa watatu na wakati huo huo kuwa ni mdomo wao katika masuala mbali mbali yanayohusiana na tuhuma na dhamira zao kisiasa. Sina shaka huu ni utekelezaji wa mpango wa Kibanda kuwa mpagazi wa mafisadi kuelekea uchaguzi wa 2015.

Angalia kwenye red, Mwanahalisi alichoripoti. Na mwisho kwa maelezo ya mwanahalisi ni kuwa Joshua na Lowasa wana uhusiano wa karibu, na sasa kuhudhuria birthday ya Joshua ni obvious. Au ulitaka wasiripoti birthday walipoti nini kama alienda kwenye birthday? Au kama unajua alichofuata haikuwa birthday tuambie kuwa tanzania daima wamedanganya. Siwapendi mafisadi lakini bado binadamu tusiwachukie na kuwapa adhabu ya kifo.
 
hizo ni ndoto za abunuasi kwa mafisadi kututawala. Lowasa anaota, hawezi kuupata urais hapa tanzania. Hatuwezi kukubali watanzania kutawaliwa na mafisadi; waliyotutendea yametosha!!!!!!!!!! Kwenye urais wasahau kabisa!!!!!!!!!!!!

ndooto we baki na ndoto ita nyota yako iliochukuliwa na wakina manji lowasa chenge...ukikaa kimya utaishia kumpisha na kingora ndugu yangu na huyu akiingia nakwambia akuna cha mape sijui nnape wa makelele na wenzake woote na imagine hiyo serikali sio mchezo
 
Hivi Mbowe katika harakati hizi anasimamia wapi na anataka kusema hajui hili na yeye ni mmiliki wa gazeti? Hivi angekuwa hafurahishwi na mwelekeo wa gazeti lake angekaa kimya? What about Chadema?[/QUOTE
Hivi kweli Mbowe na CHADEMA wanapaswa kutoa msimamo wao kuhusu maswala ya imani ya Lowassa?
Binafsi sipo tayari kumuona Lowassa akirudi madarakani.
Lakini jamaa wa watu kama anataka asichomwe kwa madhambi aliyotufanyia muacheni afanye kila analoliamini.
 
Unamaanisha Lowassa siyo fisadi? Unajua unachokiongea au umekurupuka mzee. Gazeti ndo lishaandika na habari hizo kwa kweli zinambeba Lowassa. Sasa conclusion ni nini hapo?
watenda unakurupuka Ulimakafu kasema gazeti haliwezi kutumiwa na mafisadi wewe unakurupuka na kusema Lowassa si fisadi hebu msome tena, mbona magamba mnatapatapa sana mwisho mnapoteza hata radha.
Hili ni gazet la uhakika haliwezi kutumiwa na mafisadi.
 
Tanzania Daima si ndilo gazeti lilombomoa lowasa na Richmond au?sindo gazeti la CHADEMA??Je limeanza kupalilia ufisadi??Kwanini huyo mwandishi asifukuzwe kazi??Kama ikionekana ana kainteresiti??
 
Hivi Mbowe katika harakati hizi anasimamia wapi na anataka kusema hajui hili
na yeye ni mmiliki wa gazeti? Hivi angekuwa hafurahishwi na mwelekeo wa gazeti lake angekaa kimya?
What about Chadema?

Jamani, kwani Mbowe ndiye mhariri wa gazeti? Mbona mnakurupuka kumlaumu mtu pasipo
kujua majukumu ya gazeti yapo chini ya mhariri! isitoshe Mbowe haingilii kabisa kazi za wahariri ili
mradi waandike habari zenye ukweli na zilizofanyiwa utafiti. Nadhani kama kuna lawama basi
angetupiwa Absalom Kibanda (mhariri) na si Mbowe.
 
Hata Rais wa sasa wa Ghana alikuwepo kwenye sherehe hizo na yeye anaamini aliukwaa Urais kwa msaada wa huyu "Mtume na Nabii TB Joshua"! Kulikuwa na watu wengine wengi tu maarufu hapa Afrika akiwe mo Winnie Mandela. EL naye anautaka msaada wa nabii huyu.
 
Ya mfa maji hayo ndugu yangu!!!!!!!!!!watanzania wa jana si wa leo!!!!!!!utayasadiki yangu ifikapo mwaka 2015!!! Je yawezekana kuzoa maji yaliyomwagika???????????
 
Absolom aliwahi kupewa mtaji wa milioni mia tatu na mtuhumiwa huyo ili aanzishe ofisi ya gazeti lake na maandalizi yalifanyika lakini sijui ni nini kilitokea, kwani Absolom alishafanya maandalizi ya awali kuondoka Tanzania daima lakini ghafla, ikawa kimya na harakati za kuondoka zikasimama.
Sa labda ni moja kati ya mbinu za kivita kuwa huwezi ukaondoka na kumuacha mshindani wako akiwa imara, ni lazima umnyong'onyeshe ili mtakapoanza kungombania soko usikabiliane na ushindani mkali........
Mwiny details zaidi anaweza kuturushia.
 
Back
Top Bottom