Kweli Tanzania Daima ni Mdomo wa mafisadi

Kweli Tanzania Daima ni Mdomo wa mafisadi

Tanzania Daima si ndilo gazeti lilombomoa lowasa na Richmond au?
sindo gazeti la CHADEMA??Je limeanza kupalilia ufisadi??Kwanini huyo mwandishi asifukuzwe kazi??
Kama ikionekana ana kainteresiti??

Kwa hiyo, wewe ungekuwa mwandishi na Lowasa akakutafuta ili kukueleza ukweli wake
usingeuandika eti kwa sababu ni fisadi? Rudi kwanza kwenye maadili na misingi ya
uandishi uangalie ni kifungu gani kinachomzuia mwandishi (Betty Kangonga) kuandika
habari za Lowassa. Tusishabikie tu mambo eti kwa sababu hatumpendi Lowassa, tuipime habari
kuona uongo na ukweli wake.
 
Absolom aliwahi kupewa mtaji wa milioni mia tatu na mtuhumiwa huyo ili
aanzishe ofisi ya gazeti lake na maandalizi yalifanyika lakini sijui ni nini kilitokea, kwani Absolom alishafanya
maandalizi ya awali kuondoka Tanzania daima lakini ghafla, ikawa kimya na harakati za kuondoka zikasimama.
Sa labda ni moja kati ya mbinu za kivita kuwa huwezi ukaondoka na kumuacha mshindani wako akiwa imara,
ni lazima umnyong'onyeshe ili mtakapoanza kungombania soko usikabiliane na ushindani mkali........
Mwiny details zaidi anaweza kuturushia.

Kuna ukweli fulani katika hayo uliyoandika ingawa pesa hizo zilitoka kwa Rostam na si Lowassa,
hata gari anayoendesha kanunuliwa na Rostam, lakini Kibanda ana misimamo yake ambayo haitabiriki
na ndo maana imekuwa ngumu kumnunua kijumla...
 
Hata Rais wa sasa wa Ghana alikuwepo kwenye sherehe hizo na yeye anaamini aliukwaa Urais kwa msaada wa huyu "Mtume na Nabii TB Joshua"! Kulikuwa na watu wengine wengi tu maarufu hapa Afrika akiwe mo Winnie Mandela. EL naye anautaka msaada wa nabii huyu.

Nina uhakika huyu mzee kaenda kule akitaraji atasaidiwa kupata urais wa Tanzania 2015...lakini nina amini kuwa uwezekano wa yeye kuingia kaanani ni sawa na hakuna kutokana na yale aliyoyafanya wakati ni waziri kiranja.
anachoweza kufanya ni kutubu dhambi zake na atulie kijijini kwakwe bila kujihusisha na siasa kwani ndoto yake ya kutuongoza itabaki kuwa ndoto daima.
 
Mkuu tunashukuru kwa kutujuza ya magazetini asubuhi ya leo. Hata hivyo sijui ni kwa nini imekuchukua muda mrefu kujua hili wakati wenye akili zao walilishtukia kitambo.

Swali lililopo ni je, nchi hii inahitaji mtu ambaye anaamini katika uchawi wa ki-nigeria pamoja na miujiza ya kishirikina kuwa mkuu wake wa serikali na dola? Au ameshawishika na andishi la Beatrice Shellukindo? Hivi kesho akiambiwa kwamba ilia aupate urais apeleke viungo vya albino si atakubali kuua ili atimize kiu yake? Tamaa hii iliyopitiliza ndiyo kaburi lake la kisiasa!
Nabii TB Joshua sio mchawi. Yeye ni kama akina Kakobe, Mwingira, Mzee wa upako wa kwetu hapa. Ni kijana mdogo wa mwaka 1963, June 12. Ametajirika sana kwa utapeli huu wa kidini.
 
Asubuhi hii nilikuwa nasoma gazeti la Tanzania Daima toleo la leo tarehe 15 Juni, 2011, ambalo limeripoti kwamba Lowassa anarejea leo kutoka Nigeria ambako gazeti hili limeripoti kwamba alikwenda kuhudhuria sherehe ya kuzaliwa kwa Nabii Joshua. Taarifa hiyo ilitoa pia sifa za Nabii huyo kuhusiana na uponyaji wake, utajiri wake na ukubwa na umaarufu wa kanisa lake duniani kote.

Habari hii kwa kiasi kikubwa ilikuwa na nia ya ku-pre-empty habari iliyochapishwa katika toleo la leo la Mwanahalisi ambalo limechambua kwa kiasi kikubwa kile kinachofikiriwa kuwa ni madhumuni ya msafara wa Lowassa na nukuu kutoka kwa watu wake wa karibu. Lilirejea pia mawasiliano kati ya Beatrice Shellukindo na Pindi Chana kuhusu nguvu na dhamira ya Lowassa na maoni ya nabii Joshua kuhusu uwezekano wa Lowassa kuwa rais wa nchi hii 2015.

Kwa muelekeo huu, Tanzania Daima limeendelea kuthibitisha kwamba sasa hivi gazeti hili lnatumika kama maliwato ya kuwatakasa mafisadi na hasa mapacha hawa watatu na wakati huo huo kuwa ni mdomo wao katika masuala mbali mbali yanayohusiana na tuhuma na dhamira zao kisiasa. Sina shaka huu ni utekelezaji wa mpango wa Kibanda kuwa mpagazi wa mafisadi kuelekea uchaguzi wa 2015.

Nakushauri ukazane sana kusoma gazeti la uhuru na mzalendo. Naona yanakufaa kwa uwezo wako wa kutafsi yaliyomo katika magazeti. Je hizo sherehe zilikuwepo kweli, je Lowasa alialikwa. angalia source of infomation. Inaweza ikawa ni fact au tetesi. Mwanahalisi na Tanzania Daima ni magezeti ya thinkers, usitichanganye.
 
Imani ya mtu ibaki imani ya mtu. Naunga mkono gazeti la Tanzania Daima kwa kuandika ukweli wa taarifa. Mwanahalisi limeandika kama taarifa lakini ukweli unabaki kuwa ile siyo taarifa ni makala anayofikiria mtu. Tutofautishe taarifa (toka kwa reporter au mwandishi) na makala. Makala mwandishi anaweka mpaka na hisia zake, kwa taarifa mwandishi anaweka taarifa jinsi ilivyo pamoja na source!
Tanzania Daima limekuwa tu libaya kwa sababu limeandika habari za Lowassa? na Kwa sababu huwa pia linaandika habari zisizofungamana na upande wowote kisiasa?
 

Nina uhakika huyu mzee kaenda kule akitaraji atasaidiwa kupata urais wa Tanzania 2015...lakini nina amini kuwa uwezekano wa yeye kuingia kaanani ni sawa na hakuna kutokana na yale aliyoyafanya wakati ni waziri kiranja.
anachoweza kufanya ni kutubu dhambi zake na atulie kijijini kwakwe bila kujihusisha na siasa kwani ndoto yake ya kutuongoza itabaki kuwa ndoto daima.
Watu wa karibu naye wanasema EL hajakata wala hatakata tamaa katika kuusaka Urais. Yeye huwa anasema hajawahi kushindwa kwa kila alilolitaka. Kwa kuwa ana mtandao mkubwa na pesa nyingi, anaweza. EL anaamini na wapambe wanamwambia WATANZANIA wanamkubali sana.
 
Angalia kwenye red, Mwanahalisi alichoripoti. Na mwisho kwa maelezo ya mwanahalisi ni kuwa Joshua na Lowasa wana uhusiano wa karibu, na sasa kuhudhuria birthday ya Joshua ni obvious. Au ulitaka wasiripoti birthday walipoti nini kama alienda kwenye birthday? Au kama unajua alichofuata haikuwa birthday tuambie kuwa tanzania daima wamedanganya. Siwapendi mafisadi lakini bado binadamu tusiwachukie na kuwapa adhabu ya kifo.

Asante mkuu!!
 
naona sasa Watanganyika mnahama kutoka kwenye uraisi kwa fedha kwenda kwenye uraisi kwa uchawi wa KiNigeria.

Mola awaepusha.
 
If at All Lowassa vie for presidency, I will give him my vote. I see him as a performer out of the whole CCM possible candidates who cannot speak their opinions and cannot follow through their directives. It is only Lowassa who is not soiling names of others in the media. It is the person who is thinking on his own. It is the person that I am sure if he will become a president even Kigoma will have a University!!! He can follow through, he can't be given the same reports every time he visit the district or region. He is the person who do not want ..the so called.. reasons why not done... he is the person who wants to hear...we have done to this level... and we expect to complete by..... and he will take that deadline with him and he will make a personal call if that has been achived. We want someone who can take us to the next level, we are tired with the tyrany of this current system where the rulers act mediocally!!!!!
We want a person who can become accountable when is told he has contravened the law regardless be it malicious or not!!!
We have fouling him of Richmond until the US come to clear that Richmond plant under Symbion is one of the best!!! None of our activists are talking of what Clinto has said in Dar? Why are the generators branded world class now, while our law makers said they were substandard and wasn't value for money?!!!
This is due to the fact that....these were framings..... and now have been put clear forward by Mrs. Clinton!!!
Tanzanians lets wake up, these mediocal politicians are taking us for granted!!!! We need to show them we know, if not on the ballot box then on international arena!!!!
I oppose chaos now and forever!!!
 
Mi navyoona Lowasa ni bora zaidi kuliko hata JK kiutendaji. JK anatuangusha jamani , Lol jamaa anashindwa kuwapa jampa jampa watendaji watupe utendaji bora na siyo bora utendaji kama ilivyo sasa idara nyingi za serikali rushwa nje nje iwe mahakani, hospitali, uhamiaji, polisi ndo basi tena.
 
Watu wa karibu naye wanasema EL hajakata wala hatakata tamaa katika kuusaka Urais. Yeye huwa anasema hajawahi kushindwa kwa kila alilolitaka. Kwa kuwa ana mtandao mkubwa na pesa nyingi, anaweza. EL anaamini na wapambe wanamwambia WATANZANIA wanamkubali sana.

Acha hao watu wake wamtie ujinga aje aaibike mwisho wa siku na wanafanya hivyo ili wapate kula
 
mbona gbasi la kigogo fulani lilikutwa na bangi wakamkamata dereva na tingo wasimkamate mwenye gari?
shenzi kibuyu.
 
Nabii TB Joshua sio mchawi. Yeye ni kama akina Kakobe, Mwingira, Mzee wa upako wa kwetu hapa. Ni kijana mdogo wa mwaka 1963, June 12. Ametajirika sana kwa utapeli huu wa kidini.
Wildcard acha kutoa maneno machafu mdomoni mwako? Prophet T.B Joshua he is a real man of God, na me namuheshimu sna na hata nchini kwao wanamheshimu sana. Mwambie Mungu wako akusamehe kwa sababu usloljua ltakusumbua! Syo tapeli wala Muongo kama ulvyosema. Roho wa bwana akubariki.
 
Back
Top Bottom