Kweli sikio la kufa..... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kweli sikio la kufa.....

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mpasuajipu, Jan 9, 2011.

 1. Mpasuajipu

  Mpasuajipu JF-Expert Member

  #1
  Jan 9, 2011
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 838
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  CCM: Maaskofu vueni majoho
  Imeandikwa na Mwandishi Wetu, Arusha; Tarehe: 8th January 2011 @ 23:50 Imesomwa na watu: 74; Jumla ya maoni: 0


  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Arusha kimewataka maaskofu wote na viongozi wengine wa dini mkoani hapa, kuvua majoho ya kazi yao na kutangaza kuingia katika siasa.

  Katibu wa CCM wa Mkoa wa Arusha, Mary Chatanda alisema hayo jana mbele ya waandishi wa habari wa Jiji la Arusha na kuwataka maaskofu hao kuacha kuingilia mambo ya siasa yasiyowahusu ya Meya wa Jiji la Arusha.

  Chatanda alisema, kitendo cha maaskofu kusema hawamtambui Meya wa CCM Arusha, Gaudence Lyimo kimewashtua na hakiwezi kuachwa hivi hivi.

  Alisema viongozi wa dini wanapoingilia masuala ya siasa ni ukiukwaji wa majukumu yao hivyo bora wavue majoho yao na kuingia kwenye ulingo wa siasa kama alivyofanya Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa.

  Chatanda ambaye ndiye anatajwa kuwa chanzo cha mgogoro wa uchaguzi wa umeya wa Arusha, hasa kutokana na kupiga kura kama diwani wa Arusha, ilhali alichaguliwa kama Mbunge mkoani Tanga, alisema masuala ya kisiasa waachiwe wanasiasa wenyewe.

  Chatanda ambaye alikuwa pamoja na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha, Onesmo Ole Nangole alisema kazi ya maaskofu ni kuelekeza njia za imani na kuwataka waumini kuwa wacha Mungu na si kushabikia siasa.

  “Sisi kama viongozi wa CCM wa Mkoa wa Arusha tumesikitishwa na kauli za maaskofu hao na tulitegemea kabla ya kutoa tamko lao wangetuita sote na tukatoa maelezo yetu na hapo ukweli wangeupata lakini kusema uchaguzi haukuwa halali si sawa.”

  Hata hivyo, alisema yeye kama Mbunge, alipangiwa na chama chake kuwa Arusha na hivyo, ataendelea kuwa diwani wa CCM Arusha hadi hapo itakapoamuliwa vinginevyo na chama chake.

  Akizungumzia makundi ndani ya CCM ambayo pia yanampinga hasa kutokana na kumtuhumu kusababisha CCM kushindwa Jimbo la Arusha, alisema wanaCCM hao hawajui wanalosema hivyo wanapaswa kusamehewa.

  Juzi Maaskofu wa Makanisa ya Kikristo mkoani Arusha walitoa tamko la pamoja la kutomtambua Meya wa Jiji la Arusha aliyeteuliwa na CCM na kuweka bayana kwamba hawatampa ushirikiano meya huyo.

  Walitoa tamko hilo wakati walipokuwa wanalaani hatua ya Polisi mkoani Arusha, kutumia nguvu kupita kiasi katika kuvunja maandamano ya amani ya Chadema na hivyo kusababisha vifo vya watu watatu na kujeruhi wengine zaidi ya 20.


  Hivi huyu mama anafikiri atakaa hapo milele?
   
 2. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #2
  Jan 9, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  We Maria Sa-chatanda fikiri kwanza kabla hujaongea, unafikiri wenzako waliokaa kimya ni wajinga? Uliyesababisha mtafaruku huu wote ni wewe halafu leo unajidai kusimama na kukemea manabii wa Mungu?
  Jina lako linaonyesha ni mkristo, na kama ni mkristo kweli unajua nini maana ya Mungu kuongea na wanadamu kupitia manabii wake.
  Nakushauri katubu mara moja vinginevyo utakuja kumbuka ninayoandika mimi hapa leo, si kukutisha bali ndio ukweli. Huna uchungu na damu iliyomwagika Arusha kutokana na uzembe wenu wa uruho wa madaraka na pesa?

  Kwa taarifa tu baada ya uchaguzi wa mwaka jana ambao vyama vya upunzani vimepata viti vingi bungeni na halmashari, ruzuku ya serikali imepungua ccm. Ndio maana wamekuwa wanahaha kuchukuka umeya miji ya Arusha na Mwanza kwa vile miji hiyo ina mapato makubwa baada ya dar ili kuteka pesa za kujazia pengo la ruzuku iliyopungua. Ndio maana hawajali hata mauaji yaliyotokea Arusha.

  Wakati maiti na majeruhi wamejazana hostpitalini Arusha na mali za watu zimeharibika Rais Kikwete anafanya tafrija Ikulu, na makamu wake anajipumzisha kwenye mbuga za wanyama na wake zake pamoja na watoto wakati yuko pua na mdomo na kulikotokea mauaji.

  Hiyo ndio siasa ya kisanii ya MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA KWA KASI ZAIDI
   
 3. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #3
  Jan 9, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,811
  Likes Received: 36,882
  Trophy Points: 280
  Damu yote iliyomwagika Arusha itakuandama vizazi na vizazi.
   
 4. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #4
  Jan 9, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Hivi kwa uelewa wa CCM, Siasa maana yake ni nini?

  Siasa maana yake ni mfumo mzima wa kufanya maamuzi katika jamii fulani katika masuala yanayohusu maendeleo ya jamii hiyo kijamii, kisiasa na kiuchumi.

  Maaskofu na Mashehe ni sehemu muhimu sana ya jamii yetu ambao maamuzi yaweyeyote ile inawagusa uzuri au vibaya.

  Umuhimu wao unatokana na ukweli kwamba hawa ni viongozi wa jamii ile ile ambayo siku zote maamuzi yanawahusu. Isitoshe, mtu kablaa hajawa ASKOFU au SHEHE kwanza ni RAIA WA TANZANIA.

  Hivyo basi viongozi wa dini ambao kazi yao kuu ni KUELIMISHA JAMII JUU YA UADILIFU NA KUHAKIKISHA WAKATIO WOTE KWAMBA UADILIFU UNATENDEKA na watu wote kamwe hawawezi kuenguliwa kutoa maoni yao juu ya maswala ambayo moja kwa moja yanakiuka misingi ya utawala wa kisheria (Uchaguzi wa Meya wa CCM Arusha kiuchakachuaji) na vile vile kupotoka kimaadili tofauti na taifa letu tulivyolelewa mpaka kwanza (1) Viongozi wa CCM waache Utawala Dhalimu, (2) Viongozi wa Dini kwanza waondolewe Haki zao za Uraia, au (3) CCM na serikali yake wahakikishe ya kwamba na wao hawana uhusiano wowote wala muingiliano na vikundi vinavyoongozwa na viongozi wa dini nchin.

  Pia, ieleweke kwamba uzuri au ubaya wa serikali katika jamii fulani huamuliwa kutokana na viwango vya uhuru katika kushirikisha jamii katika maamuzi yake, kuhojiwa, kukemewa na vikundi mbali mbali kama vile vyama vya siasa, asasi za kiraia na asasi za kidini.

  Kwa msingi huu hao viongozi ambao hupendelea kutaka viongozi wa dini wakae kimya wakati nao ni walipa kodi na wenye haki sawa kuhoji nyendo zote za serikali ni vema kwanza wakamtake Dr Benson Banna elimu ya siasa na uwajibikaji katika mazingira mapya ya siasa za ushindani.

  La sivyo kuna matamshi mengine ambayo baadhi ya viongozi wetu wanapoendelea kuyatoa kwenye vyombo vya habari, msomaji wa habari hizo hujikuta kutamani kuelewa umri wake na enzi alizoenda shule.

  Tofauti na hapo, HUU WIMBO WA VIONGOZI WA DINI KUTOZUNGUMZIA SIASA NI NDOTO TAMU ZA ALINACHA tu.
   
 5. monge

  monge Member

  #5
  Jan 9, 2011
  Joined: Apr 10, 2010
  Messages: 30
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyu mama ana AMNESIA AU KACHANGANYIKIWA.
  Anajuwa kabisa yeye ni miongoni mwa chanzo cha hii karaha na mauaji yote yalotokea ,lakini bado ana jeuri
  ya kufungua kinywa chake na kutoa kauli za kebehi kiasi hiki kwa watu waliotumia uhuru wao wa kikatiba wa kuongea
  na kutoa maoni yao! Ama kweli sikio la kufa halisikii dawa!
   
 6. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #6
  Jan 9, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Kweli nimeamini sikio la kufa halisikii dawa. Kifo cha ccm kinabisha mlangoni.
   
 7. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #7
  Jan 9, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Hawa wanaojidai viongozi wa kanisa ndio walioletaa chokochoko mpaka tukaona mauwaji ya kutisha huko Rwanda, sasa wameanza Tanzania. hawa ni wafuati wa shetani na si Mungu.
   
 8. monge

  monge Member

  #8
  Jan 9, 2011
  Joined: Apr 10, 2010
  Messages: 30
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ya rwanda na ya Tanzania hata hayafanani!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 9. M

  Malunde-Malundi JF-Expert Member

  #9
  Jan 9, 2011
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,287
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Shetani zomba ishia hapo naona unaanza kashfa sasa. CCM na polisi ndio mashetani wanaokula damu za watu. Pum..fu
   
 10. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #10
  Jan 9, 2011
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,584
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Chatanda uvae wewe joho maana inaelekea unayajua sana majukumu ya maaskofu.
  Labda huko hutapata nafasi ya kusababisha vifo vya watu.
   
 11. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #11
  Jan 9, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Hayfanani? kifo ni kifo, au hukuona Arusha juzi imetokea nini?
   
 12. whistle blower

  whistle blower Member

  #12
  Jan 9, 2011
  Joined: Jan 5, 2011
  Messages: 84
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  [QUOTE=zomba;1465401]Hawa wanaojidai viongozi wa kanisa ndio walioletaa chokochoko mpaka tukaona mauwaji ya kutisha huko Rwanda, sasa wameanza Tanzania. hawa ni wafuati wa shetani na si Mungu.[/QUOTE]

  Historia ya Ruanda huijui, uliza ili uambiwe ndio utoe mchangao wako, jamani kuuliza c ujinga. Mambo ya kuongeangea bila data nakuamuru uacha. Vurugu za Ruanda zipo tangu kuingia kwa mkoloni Yaani Mbelgiji alipoingia Ruanda.
   
 13. Malafyale

  Malafyale JF-Expert Member

  #13
  Jan 9, 2011
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 11,214
  Likes Received: 3,626
  Trophy Points: 280
  Mauaji yenye mlengo wa kidini yapo kwa kila dini;kwa mfano kule Algeria kila siku tunasikia wana mgambo wenye msimamo mkali wameua mamia ya watu kwa kuwakata makaromeo au hata indonesia kila siku tunaona wanauana kwa chokochoko za kidini na sina uhakika kama majority ya sehemu hizo nilizozitaja ni wanaokwenda makanisani!

  Ningekuelewa kama tu ungesema chokochoko za kidini sio nzuri kuliko ulivyo point out dini moja tu na kuonyesha kuwa ndiyo wamesababisha machafuko mengi barani Africa!
   
 14. V

  Vancomycin Senior Member

  #14
  Jan 9, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 171
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Tukiweza pambana na adui ujinga then waliobaki rahisi
   
 15. Nsiande

  Nsiande JF-Expert Member

  #15
  Jan 9, 2011
  Joined: Jul 27, 2009
  Messages: 1,649
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Hawajidai kuwa ni viongozi wa kanisa bali NI viongozi wa kanisa, tena viongozi wa juu
  Justify your second statement ! Mtu kusema hamtambui mtu mwingine automatically anakuwa mfuasi wa shetani?
  Zomba with your 50+ yrs kama ulivyojipambanua mwenyewe, nadhani bado hujaelewa nafasi ya viongozi wa kiroho kwenye siasa
   
 16. m

  mams JF-Expert Member

  #16
  Jan 9, 2011
  Joined: Jul 19, 2009
  Messages: 616
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Kama hajafurahishwa na hiyo kauri ya watu wa dini basi angefurahi zaidi kama alivyotaka angeambiwa hao CDM watulie. Vyombo vyote vikiwamo vya dini vina haki ya kuusemea ukweli pale inapobidi. Na sio kufurahia tu pale wanaposema JK ni chaguo la Mungu. Huyo mama, kiustaarabu alipaswa kujiuzuru hata kabla ya naibu Meya!
   
 17. Mumwi

  Mumwi JF-Expert Member

  #17
  Jan 9, 2011
  Joined: Jan 9, 2011
  Messages: 592
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Maaskofu na viongozi wa dini mbalimbali wanaruhusia kukemea serikali na viongozi mbali mbali wanaokwenda kinyume na sheria za nchi.
   
 18. mwankuga

  mwankuga JF-Expert Member

  #18
  Jan 9, 2011
  Joined: Aug 30, 2010
  Messages: 329
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  Vipi jamani,huyo dada ameolewa?maana ni vema akaendelea kuboresha ndoa yake kuliko kuingilia mambo ya siasa ambayo hayawezi.Ni mbunge wa viti maalum!wengi tunajua jinsi wanavyopatikana hasa wa CCM,WENGI NI ASUSA ZA WAKUBWA.
   
 19. Mo-TOWN

  Mo-TOWN JF-Expert Member

  #19
  Jan 9, 2011
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,629
  Likes Received: 140
  Trophy Points: 160
  BIG UP sana Uwezo tunao! inaonyesha ni kwa kiasi gani CCM Arusha na viongozi wao walivyokuwa na uelewa mdogo kuhusu siasa na wadau ktk siasa. Kama hamjui au hamtaki kujua kwa makusudi ni kwamba Viongozi wa dini za kikistru wameongea juu ya swala na uchaguzi wa umeya Arusha kama wadau wowote wale ambao ni sehemu ya jiji la and for that matter mtu yeyote ni sahihi kuongelea swala hilo ali mradi anaguswa kwa nana moja au nyingine na shughuli za jiji la Arusha.

  Get it you f**ls. Halmashauri haziendeshwi kwa manufaa ya vyama au wanasiasa. Muelimisheni pia Katibu mkuu wenu ambaye kilaza of all time.
   
 20. Mumwi

  Mumwi JF-Expert Member

  #20
  Jan 9, 2011
  Joined: Jan 9, 2011
  Messages: 592
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mi niko Arusha sijawahi kumwona Jana nilimwona first time runingani sijui kaolewa au bado sitaki hata kumwona mmwagaji damu huyu
   
Loading...