Nami nilitaka kumwambia hivihivi na muda mzuri wa kuuona ni jioni.Ata ukiwa Arusha unaweza kuuona.
Rais amejificha kwenye Mlima.Amakweli hii nchi ya ajabu sana....
Yaani watu tunatafuta Rais wewe unatafuta Mlima...[emoji44][emoji848]
Zanzibar inaonekana ukiwa usawa wa mlima Kilimanjaro?Ukiwa unapita na plane kwa juu from dar to arusha...ndege huwa znaambaa ambaa pembezon mwa bahar had arusha..bas structure znavoonekana yaan utaipenda dunia..vile vile kama kwwnye vitab.milima.tributaries..rivers etc..yaan huk mlima huwa unaonekana vzur had raha..ka zanzibar unakaona kalee..yaan kote
Unaonekana ukiwa angle zip moshi ili nijipange sku moja au popoteMlima hua hauonekani kila siku Kapteni. Kuna siku mawingu yanaufunika wote, siku zingine unaona kilele kikiwa ndani ya mawungu, ukibahatika unakura siku kitu kipo mubashara kabisa chote unauona mlima mwanzo mwisho.
Arusha kwel mkuu ? Kila sku naangaza macho naambulia meruMbona Hapa hapa Arusha unaoekana vizuri tu..mimi nikiwa chumbani kwangu nauona safi kabisa kupitia dirishani..huku Moshono tanganyika parkers...kila siku hasa hali ya hewa ikiwa clear.
Arusha yap....karbu na maghorofa ya jeshi baada ya kuvuka reli unauona kili live bila chenga.Arusha kwel mkuu ? Kila sku naangaza macho naambulia meru
Wakuu salamu,
Ni hivi leo asubuhi baada kuwa off na kikazi ninachofanya hapa Arusha nikajisemea moyoni sasa ngoja niende Moshi nasikia ni fasta kutoka A Town ili nijionee Mlima Kilimanjaro kwa macho yangu.
Mzee mzima nikajikoki na ten yangu huyo kwenye coaster ili njia nzima mimi macho yangu yapo kodo kwenye madirisha nikijua tu nitaona mlima hola, mara KIA hapa nikasema sasa lazma itakuwa nakaribia kuuona mlima hadi moshi mjini Hola, nikazunguka zunguka bado sikubahatika mpka jioni.
Badala ya kuona mlima Kilimanjaro nimeambulia kula matunda tu na kurudi zangu Arusha.
Mpaka sasa sielewi kabisa mlima haonekani ukiwa Moshi Mjini sasa nitauonea wapi mie au mpka nirud kwenye atlas kweli.
Nipeni uzoefu niende maeneo gani tena niweze kuuona Mlima Kilimanjaro.