Katika maongezi yake hayo atawafikia watanzania wangapi ambao ni wapiga kura? Achana na wale wa mitandaoni wengine wakiwa inje ya nchi.Huyu jamaa TAL katika hotuba yake anahutubia kwa Kiswahili na then kwa Kiingereza - maana yake unajua ni nini? Anataka dunia nzima ielewe mambo yale mabaya ambayo pengine yanafanyika Tanzania. Ukweli baya moja tu huweza kuchafua sana sifa ya mtu. Kwa mfano mchukue tu hata askofu ambaye siku zote ana maadili mema na anawaongoza watu vizuri kiimani, siku ikitokea kambaka muumini wake basi stori itakuwa kubwa sana ya kusemwa ubaya wake huo kulik stori ya mema ambayo ameshayafanya. TAL anavuta hisia kubwa sana kimataifa hasa tokana na tukio lake la kucharazwa risasi. Nasikitika sana why JPM hakuwahi kusema jambo kulaani kitendo kile na hata kuelekeza kuwa TAL arudi nyumbani na atampatia ulinzi. Hili linaenda kuharibu sana. Dunian kote hata uwe na uwezo mkubwa kiasi gani watu hujali ubinadamu kwanza. Ona ya George Floyd huko Marekeni - nani aliamini kama watu wanaweza kuwa vile. Nani anaamini hata wanajeshi na Polisi wenyewe kwa kitendo kile wamekilaumu. Mtu asikudanganye ubinadamu ni kila kitu - ni zaidi ya madaraja, njia za treni, barabara, shule bure na hata chakula! TAL alikosewa kuzingatiwa ubinadamu wake na Serikali hii - kwa kweli hili lina gharama. Maneno yake ya kesho yanaleta historia isiyo ya kawaida.
Huyu bwana tukubali tukatae atabadilisha watu sana. Uchaguzi wa Mwaka huu utakuwa mgumu kuliko yote iliyopita. Najua hataongelea kulipiza kisasi ila ataongelea tu ubinadamu unavyobinywa na umaanani unavyowekwa kwenye vitu. Mwenyewe kwa binafsi yangu huwezi kunipa kitu kwa matusi nikakubali hata kama wewe ni tajiri kiasi gani! Kukosekana kwa ubinadamu kumetuharibia CCM, ndiyo maana hata mafly ova ya TAZARA na Ubungo hayajatupa msosi wowote ule na zaidi yake yamezuia nyongeza ya mishahara ya walioko kazini.
Kwa ujumla hakuna jipya hapo na wala haisaidii chochote kwenye uchaguzi mkuu.