Kweli CHADEMA wanapendwa hivi au Macho yangu!?

kama mnafikiri mnakubalika kafanyeni mkutano jangwani au k/ndege(moro) hapo muone aibu yake..mnafikiri kila sehemu ni Arusha au Moshi.
 
haaaaa!!! kaka safiiiiiiiiii sana jamani tujipange kukomboa nchi yetu chadema wameonesha njia wengine tufuate:heh:
 
kama mnafikiri mnakubalika kafanyeni mkutano jangwani au k/ndege(moro) hapo muone aibu yake..mnafikiri kila sehemu ni Arusha au Moshi.

huna ulijualo ww ila nakuapia muda ukifka na akili yako ikafunguka utajilaumu sana! kama sivyo bas unanufaika na ccm!
 
Haya ni mabadiliko ambayo ni Mungu ameamua kuyaleta hivyo CDM wasijipe masifa. Wanatakiwa kuendelea kuwa wakweli na kuwa makini wasije kuiharibu chama. Jambo kubwa liinalotokea sasa ni kuwa CCM imeanza kuondoka katika mioyo ya watu na wakati huohuo CDM imeanza kuingia ndani ya mioyo. Ogopa sana watu wakipenda au wakichukia. CCM ina kazi kubwa sana na hawataweza kukinusuru chama chao iwapo wataendelea na propaganda kama kawaida. Wananchi wa leo hawataki propaganda wanataka kitu halisi. Kama umeahidi kujenga daraja usipotimiza wananchi wanakumbuka na huwezi kuwadanganya. Tanzania inaenda kupona sasa.
 
Kiukweli kabisa ccm hawana chao 2015 na wenyewe wameanza kuliona hilo nawaomba tu vijana wenzngu wahakikishe inapotokea suala la kujiandikisha wakati wa kurekebisha daftari la wapiga kura wajitokeze kwa wing ili wote tuwe na shahada za kupigia kura ili 2015 tukamalizep huu utawala wa kisultan ndani ya ccm.
 
Nimeipenda sana hii. Welcome Millya, change your mind and attitude fight for the real freedom and not magambas' well being.
 
huwa napenda sana maneno ya viongozi wa chadema wanaposema maneno haya
WAO WANA PESA SISI TUNA MUNGU.


Mkuu, hapa waongeze kwa kusema hivi "WAO WANA PESA, SISI TUNA MUNGU NA WATU!!!"
 
Hiyo ni kali na Bado,Kwani watu wameamua kufanya kweli hakuna wa kuwazuia.

Mimi napata shida kujua itakavyokuwa siku wananchi wakiamua kwa pamoja kuwaadhibu viongozi wa ccm na kuasi utawala wao...hapatatosha
 
Michango ya namna hii inawezekana Mwanza, Arusha na Mbeya Kwa wajanja. lakini sio huku Morogoro, wala Dodoma.
 
:)hata wazee nao wanakipenda cdm ni waganga tu wakienyeji ndio hawakipendi cdm.

yuuuuuuuwiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii natamani upendo na maombi kwa cdm nchi nzima toka pemba mpaka mpanda, mtwara mpaka longido, moshi mpaka mbeya kila eneo cdm 2015 m4c lazima wataelewa tuuuu nchi hii tulipewa na mungu na waasisi walikuwa waaminifu tatizo hawa wenye mivto
 
ukweli ni kitu kinachoweza kufunikwa kwa muda tuu! lakini wakati hufika ambapo ukweli hujitokeza na mapingamizi yake huwa kama uopepo usio na nguvu. hiyo ya mwanza ni changamoto kwa miji mingine hasa ya kusini mwa tz ambayo imekumbatia ccm kupindukia. ukweli miji ya wasomi imefunguka kutosha na sera za chadema hupenya akilini moja kwa moja. tufunguke, tuachane na uozo!
 
Imetokea jana kwenye Dala dala la Kutoka Airport kwenda Buhongwa (MWANZA), Kama kawaida ya konda ndani ya dala dala anadai chake (Nauli), kabla hajamaliza kudai nauli gali likakata mafuata kiaina (likawa linazimika zimika), ikabidi dereva aingie sheli kuongeza mafuta.

Hatujajua kinachoendelea akainuka mama mmoja kwa asila na kumkoromea konda na dereva, akisema: Mambo ya kutembea na Mafuta ya vidumu mnatuchelewesha kwenye vikao na ntaenda kupigwa faini kwa kuchelewa Tsh. 5,000/=: Mara jirani yake akadakia, Kikao cha nini? Mama akajibu: Kikao cha chama, kwa mshangao wa wengi, kila mmoja alidhani labda kikao cha wakinamama au SACCOS: Mama akadakia tena: Kwenye kikao cha chama cha CHADEMA!

Nkiwa bado nashangaa abiria wote wakadakia: Kama ni kikao cha CHADEMA, tutakuchangia iyo faini, nilidhani kama utani! Kwanza yule konda akamwambia yule mama: wewe ni mjanja, akamrudishaia nauli yake, nkiwa naendelea kushangaa, konda akaanza kukusanya michango kwa ajili ya yule mama. Amini usiamini alichangiwa Tsh. 32,500/=. Chakushangaza zaidi hata watoto wa shule walimchangia yule mama.Nilibaki kushangaa mwanzo mwisho!

Naanza kuisi mabadiliko, kweli hapa Mwanza si mchezo.

Ni mimi nisiyekuwa mwanachama wa chama chochote kwa sasa.

Tag this post to Nape
 
Watanzania tumechoka, wengi wapo kimya kwa sababu, either wananufaika na mfumo ulioko moja kwa moja au wanadhani serikali nzima kuanzia mtendaji wa kijiji kuja wafanyakazi wa halmashauri hadi wizarani ni ccm, nadhani wanajiuliza kama cdm itachukua nchi watendaji hao wote watatoka wapi? Poleni sana watanzania wenzangu mnaoteseka bila kujua chanzo cha mateso yenu. Umaskini wetu watanzania upo kichwani zaidi. Mungu ibariki Tanzania!!!!!!
 
Hii nilishawahi kukutana nayo kwenye daladala nikitokea uswazi kwangu vingunguti........basi kuna jamaa akawa anaiponda chadema alkua siti ya nyuma abiria gari zima wakasimama kama vile wanataka kumnyofoa wagawane viungo vyake vya mwili!! Almanusura wamtolee dirishani dereva akamua asimame na kumwamuru konda amrudishie jamaa nauli yake ashuke ili amani ipatikane.....
Chadema hatushikiki!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!




ila nahisi sasa ivi wataing'oa hii post maana yangu waliing'oa fasta
 
Back
Top Bottom