Mchana huu wakati tunapata chakula,wanamama na baba mmoja wanafanya kazi ofisi ya umma wanalalamika kuwa diwani waliye naye anawatendea uhuni wa kuwafunikia mchanga na vumbi kwenye barabara yao, na kutoa mfano wa kata ya diwani wa cdm, kuwa wao mambo yao sasa safi lakini wao wanajuta.Hitimisho wakasema wao sasa wameamua kujiunga na cdm na uchaguzi ujao imekula kwao.Nikawaambia nyie sio ni wale walochukua kanga na kitambaa?"Aka hatufanyi ujinga huo tena",walisema.Na wakamsifia Tundu Lissu kwa hoja zake bungeni.Kwa hiyo mabadiliko yana kuja kama unaona hata kina mama wanashituka.