Fundisi Muhapa
JF-Expert Member
- Nov 25, 2013
- 4,422
- 2,115
Ungetaja hizo faida ili tudadavue. Na usisahau sio lazima limilikiwe na serikali.Kwanza unatakiwa ufahamu faida za nchi kuwa na Airline company yake,
Fastjet hawajawahi kupata faida tangu waanze biashara hapa Tanzania halafu unasema kwamba serikali iwekeze huko,baada ya ATCL kufufuliwa ndio kumewazindua Fastjet wakafanya redundancy na kuondoa zile ndege kubwa
Ungetaja hizo faida ili tudadavue. Na usisahau sio lazima limilikiwe na serikali.
Umeamua kuchagua FJ. Nilitaja mbili.
We jamaa unajua hayo ulotaja yote except Ethiopia yanajiendesha kwa hasara? Rwandair ni tangu waanze hakuna faida.Airline company za nchi nyingi za Africa zinamilikiwa na serikali (South Africa Airways,Ethiopian Airways,Kenya Airways,Rwanda Air) ungetupa mifano ya hizo private company ambazo zimefanya vizuri
Hapa kwetu hakuna Airline ambayo zinaendeshwa vizuri (FN,PW,ATCL ) ingawa kama uendeshaji ungekuwa mzuri ATCL wangekuwa na advantage lakini hawaitumii last month Fastjet walibakiwa na ndege moja ikabidi wakodi nyingine 2 na wamefanya redundancy ya wafanyakazi
Tunajenga Terminal 3 inafunguliwa Dec 2017 ambayo itasaidia kuongeza idadi ya abiria,wenzetu Kenya,Rwanda,SA,Ethiopia wanatumia vizuri mashirika yao kuzitangaza nchi zao kiutalii sisi tumelala kuna wazungu wanajua Mt Kilimanjaro iko Kenya tuna vivutio vingi sana lakini havijulikani sana kimataifa.
Mashirika mengi ya serikali bado yanaendeshwa kwa mfumo wa kizamani solution ni kubadilisha mfumo ili yaweze kujiendesha kwa faida .TBC,TTCL,Posta,TRL,Dawasco,Utalii haya ni baadhi ya mashirika ambayo inabidi kubadisha mfumo wa uendeshaji na sio kubinafsisha
Nilikuuliza swali la msingi hadi sasa hujajibu,taja hayo mashirika binafsi yaliyopata faida hapa Africa ?We jamaa unajua hayo ulotaja yote except Ethiopia yanajiendesha kwa hasara? Rwandair ni tangu waanze hakuna faida.
Kuhusu kutangaza utalii, hata wakati ATC inafanya kazi Kilimanjaro ilijulikana ipo Kenya!!
Lakini zaidi kuhusu utalii, ufaransa wana utalii mkubwa sana na hawamiliki na kuendesha shirika la serikali!! Marekani nako hivyohivyo.
Ndo dunia inakokwenda. Sio kujikunyata kulilia ndege wakati zinawashinda.
Hakuna cha customer care wewe. Hizo ndege za 330,000/ per trip ukitaka hata maji tu ya Dastan ya 500 mls unalipa shs 3,000/, ukitaka Kilimanjaro beer unalipa shs 10,000/, ukiwa na begi la kilo 5 unalilipia shs 23,000/ na hakuna cha smile face wala nini. Na hakuna mteja anayenunua hayo mavitu yao. Lengo la mteja ni kufika salama huko anakokwenda, customer care ataipata nyumbani kwake siyo kwenye ndege!!Sasa kwanini nauli hayo mashirika mengine nauli ipo 330,000/=bado watu wanalipa nauli nakupanda?ATCL waboreshe Customer Care hicho ndicho watu wanangalia sana wanapochagua huduma fulani hili wakipata hiyo huduma waweze kuridhika.
Rwandair kujiendesha kwa hasara ilikua haiepukiki, lakini shirika lile linakua kwa haraka walianza kujizatiti na kukamata soko la West Africa hivi sasa KQ na ET wamepoteza abiria wengi na wamechukuliwa na Rwandair. Polepole airport yao Kanombe inakua kama Jomo Kenyata-Nbi au Bole-Adis.We jamaa unajua hayo ulotaja yote except Ethiopia yanajiendesha kwa hasara? Rwandair ni tangu waanze hakuna faida.
Kuhusu kutangaza utalii, hata wakati ATC inafanya kazi Kilimanjaro ilijulikana ipo Kenya!!
Lakini zaidi kuhusu utalii, ufaransa wana utalii mkubwa sana na hawamiliki na kuendesha shirika la serikali!! Marekani nako hivyohivyo.
Ndo dunia inakokwenda. Sio kujikunyata kulilia ndege wakati zinawashinda.
Kuhusu hao binafsi kupata faida au hasara hainihusu. Ya serikali inanihusu maana ni kodi yangu inatumika vibaya. Na kwa hapa PW wameanza hasara baada ya ubia wao na KQ. Again, hainihusu coz ni wao na biashara zao. Cha msingi serikali iwawekee usawa wapambane.Nilikuuliza swali la msingi hadi sasa hujajibu,taja hayo mashirika binafsi yaliyopata faida hapa Africa ?
Then usifananishe Tanzania/Africa na France hao wako dunia nyingine
Umewahi kujiuliza kwa nini licha ya hayo mashirika(SA,KQ,WB,MS) kutoingiza faida kwa nini hizo nchi bado zina hayo mashirika na bado yanapata support ya serikali ?
Airline industry inaingiza faida nyingine indirectly ukiacha faida ya mashirika ya ndege.Mkiwa na Airline itawabidi mjenge viwanja vya kimataifa kuna ndege toka nje zitakuja zitalipa kodi,wasafiri watakaa hotelini na ni fursa ya kutangaza utalii uliopo. Mafanikio ya Ethiopian Airline ni moja ya chanzo cha mapato ya uchumi wa Ethiopia
Wakati huo ni pesa za walipa kodi zinalisustain. Ndege ni anasa my friend. Hao Rwanda illiteracy ni zaidi ya 25% unanambia ndege imekamata ruti za west?Rwandair kujiendesha kwa hasara ilikua haiepukiki, lakini shirika lile linakua kwa haraka walianza kujizatiti na kukamata soko la West Africa hivi sasa KQ na ET wamepoteza abiria wengi na wamechukuliwa na Rwandair. Polepole airport yao Kanombe inakua kama Jomo Kenyata-Nbi au Bole-Adis.
Nilichokiandika ni kwa uzoefu wangu. Nimeshasafiri sana na rwandair nimefanya kazi Rwanda kwa vipindi tofauti tofauti. So I personally know how the said airline helps to promote/advertise the country internationally. Sisi kila siku tunaimba kubana matumizi tu. Ni lazima tujitangaze kimataifa, tutangaze fursa na vivutio vinavyopatikana nchini kwetu. Mashirika ya ndege yanayomilikiwa na serikali si jambo la ajabu sana kupata hasara lakini yana sustain. Tembea ujionee ndugu.Wakati huo ni pesa za walipa kodi zinalisustain. Ndege ni anasa my friend. Hao Rwanda illiteracy ni zaidi ya 25% unanambia ndege imekamata ruti za west?
Ya msingi kwanza ndugu. Ndege zinajiletaga zenyewe. Kweli Africa tuna safari ndefu sana. Sijui kwanini tunang'ang'ania hivyo yanayotuangusha in the name ya chakwetu.
Tunaenda mbele na kurudi nyuma ukiulizwa maswali unaruka ruka,unatoa ushauri bila kutoa mifano.Nafanya kazi na watu wa airline ET sio wala rushwa au wapiga kelele kama sisi hapa ni wazalendo ndio sababu kubwa ya wao kufanikiwa.Faida ya kuwa na airline company sio lazima iwe directly nimekueleza pamoja na hizo airline kupata hasara lakini hakuna nchi inayofikiria kufuta shirika lake hao KQ pamoja na kubinafsisha still wanaingiza hasara mwaka wa 4 mfululizoKuhusu hao binafsi kupata faida au hasara hainihusu. Ya serikali inanihusu maana ni kodi yangu inatumika vibaya. Na kwa hapa PW wameanza hasara baada ya ubia wao na KQ. Again, hainihusu coz ni wao na biashara zao. Cha msingi serikali iwawekee usawa wapambane.
Halafu hao Kenya Airways wenyewe hata si serikali 100%. Ndo uone majirani ni wajanja wamehedge risk zao. Busara ya wahenga kutoweka mayai yote kapu moja unahusika. Zaidi ya 70% ya KQ sio serikali!!
Hiyo habari ya airline kuwa na faida zingine ni uongo wanaotengeneza wasimamizi uchwara wa hizo govt operated commercial airlines ili waendelee kufuja. Faida ya biashara iko bottomline. Mengine tafuteni kingine kiyalete.
Btw, kujenga viwanja vingi vya ndege ni demand km ipo. Sio kisa una ndege. We jamaa bana. Marekani hawaown mandege ya serikali na wana viwanja ile mbaya. Kadhalika, tulijenga Songwe International wakati ATCL imejifia. Your argument quashed just like that.
Halafu hii habari ya kusema tusijifananishe na Ufaransa na kadhalika wanapenda sana kutumia watawala wa awamu hii.
Kuna nini? Mnaogopa nini kujipima na walioweza? Mnang'ang'ania mikakati ya waliofeli badala ya kuiga waliofaulu? Pathetic. Kisa wao wazungu ndo hawafai kuigwa? Eti mmeenda kuchukua uzoefu Rwanda. Watu hawajawahi tengeneza faida tangu waanze operations. Kweli??? AIBU!!!!!!
Jamaa, amkeni bana. Dunia haitusubiri eti tutapata faida zingine kwa serikali kufanya biashara ya ndege. Zipi? Sasa mnatafuta suluhisho la utendaji mbovu. Mkimaliza hilo mtakuja kuchelewa malipo ya supplier. Then ufisadi utatamalaki na kupeleka ndege mazishini badala ya ruti husika n.k. n.k
Mkitoka hapo mnarudi nacho serikali haifai kufanya biashara mnauza tena shirika. Do it now ndege zingali mpya.
Umezungumzia Ethiopian kukukuza uchumi wa kwao. Sikatai. Tena ndo airline pekee kubwa Africa ina faida. Sasa kilichowanyima kwenda kujifunza kwao mkaenda kwa failures Rwandair ni nini? Inarudi kulekule, ATCL wameshindwa kabla hawajaanza.
Nipo hapa nakusubiri belo.
Basi wasibowasiboreshe huduma zaoHakuna cha customer care wewe. Hizo ndege za 330,000/ per trip ukitaka hata maji tu ya Dastan ya 500 mls unalipa shs 3,000/, ukitaka Kilimanjaro beer unalipa shs 10,000/, ukiwa na begi la kilo 5 unalilipia shs 23,000/ na hakuna cha smile face wala nini. Na hakuna mteja anayenunua hayo mavitu yao. Lengo la mteja ni kufika salama huko anakokwenda, customer care ataipata nyumbani kwake siyo kwenye ndege!!
ina maana fn wana ndege ndogo kama pangaboiKwanza unatakiwa ufahamu faida za nchi kuwa na Airline company yake,
Fastjet hawajawahi kupata faida tangu waanze biashara hapa Tanzania halafu unasema kwamba serikali iwekeze huko,baada ya ATCL kufufuliwa ndio kumewazindua Fastjet wakafanya redundancy na kuondoa zile ndege kubwa
Watumbuliwe tu mbafu zaoKwenye domestic flights, routes za Dar - Mwanza ndizo zenye wateja wengi na zinalipa. Mashirika ya Precion air na Fast jet kila moja lina route tatu za Dar- MZA yaani saa 2 asubuhi, saa 6 mchana na saa 2 usiku. Trip za asubuhi na saa 6 ndizo hot cakes zenye wateja wengi na bei yake ni kubwa. Trip ya usiku siyo hot, kwa maana mkazi wa Mwanza kufika Dar usiku kama hana makazi Dar ni usumbufu na gharama zaidi ya usafiri toka airport kwenda kusaka hotel za kulala.
Cha ajabu tangia ATCL waanze kutoa huduma hii wao wameamua kufanya route moja tu ya usiku, tena usiku wa saa 3 na nusu, yaani kufika Dar saa 5 usiku. Zile route nzuri wamewaachia washindani wao. Bei za ATCL ni nusu ya bei za washindani wao, hivyo wakaona waachie hizo route maana washindani wao hawangepata wateja au ingebidi nao wateremshe bei.
Sasa kwa nini wasitumbuliwe?
Nadhani ni bei nafuuu kuliko hizo nyingine. Kwa maana nyingine, wao wanaona watu watawachukua hata kama saa nane usiku mradi bei ni ya chini.Fafanua kidogo kwenye bei.
Una maana Atcl bei yao ni kubwa mara mbili kuliko precision air na fastjet au?
Kwani umesahau kama precision ni ya wachaga mkuu?Magufuli akitumbua viongozi kama hao wafuasi wa Chadema wanalalamika.
mweeeeeLabda wamepanga trip za usiku kuepuka joto ili ndege za ATCL zisipate pancha wakati wa kutua
Kwenye domestic flights, routes za Dar - Mwanza ndizo zenye wateja wengi na zinalipa. Mashirika ya Precion air na Fast jet kila moja lina route tatu za Dar- MZA yaani saa 2 asubuhi, saa 6 mchana na saa 2 usiku. Trip za asubuhi na saa 6 ndizo hot cakes zenye wateja wengi na bei yake ni kubwa. Trip ya usiku siyo hot, kwa maana mkazi wa Mwanza kufika Dar usiku kama hana makazi Dar ni usumbufu na gharama zaidi ya usafiri toka airport kwenda kusaka hotel za kulala.
Cha ajabu tangia ATCL waanze kutoa huduma hii wao wameamua kufanya route moja tu ya usiku, tena usiku wa saa 3 na nusu, yaani kufika Dar saa 5 usiku. Zile route nzuri wamewaachia washindani wao. Bei za ATCL ni nusu ya bei za washindani wao, hivyo wakaona waachie hizo route maana washindani wao hawangepata wateja au ingebidi nao wateremshe bei.
Sasa kwa nini wasitumbuliwe?